SoC02 Nitunze, nithamini ili niishi kwa amani na furaha

Stories of Change - 2022 Competition

Ndelenoah1

New Member
Jul 28, 2022
3
2
Habari za muda huu mpendwa, nipende kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kutumia muda wako na kuisoma makala hii "NITUNZE NITHAMINI ILI NIISHI", ni makala iliobeba sauti ya mtu (watu) wanaoishi na maambikizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi ikiongea na jamii kwa ujumla wake.

Makala hii imekwenda kuzungumza na makundi mawili yanayohusika moja kwa moja na maangalizi watu wanaoishi na maambikizi ya virusi vya ukimwi, makundi hayo ni

(i) Wauguzi wanaohusika watu wanaoishi na maambikizi ya virusi vya ukimwi
(ii) Jamii wanaoishi watu wenye maambikizi ya virusi vya ukimwi

(I)WAUGUZI
Wauguzi ni watu wanaohusika na matibabu pamoja na uwangilizi wa karibu Sana,sauti inaposema "NITUNZE, NITHAMINI,ILI NIISHI", neno 'NITUNZE' linatulenga moja kwa moja Wauguzi kwa asilimia kubwa japo inapobidi hata Jamii tuna wajibu wa kuwatunza. Ili mtu mwenye virusi vya ukimwi (VVU) aendelee kuishi na kuwa na afya Bora ,Kama wauuguzi tunapaswa kubeba jukumu la kumtunza kwa kuwajibika katika mambo yafuatayo

1. Kufuatilia zoezi zima la kumeza dawa ,Kwakuwa mtu mwenye virusi vya Ukimwi anatikiwa ameze dawa kila siku hivyo wauguzi tunapaswa kumsaidia mtu huyo kila siku ,Kama nilivyosema hapo juu Wauguzi wamegawanyika katika makundi mawili ,vile vilena kazi zao katika zoezi hili lipo katika makundi mawili

(I) Wauguzi katika vituo vya afya ,tunawajibu wa kuhakikisha mtu huyu anahudhuria kliniki tarehe sahihi ya kuchukua dawa kwa kufanya nae mawasiliano kila ifikapo tarehe husika

(II) Wauguzi wa nyumbani (watu tunaeishi nae kwa ukaribu)tunawajibu wa kuhakikisha mtu huyu anakunywa dawa kila siku katika muda sahihi.

2. Kufuatilia zoezi zima la matibabu na vipimo,kwa sababu mtu mwenye amaambukizi ya virusi ya ukimwi anapaswa kupata vipimo Mara kwa Mara Kama vile kipimo Cha kuangalia wingi wa virusi kila baada ya mda Fulani, kitu ambacho kama binadamu unaweza kuchoka, hivyo kama Wauguzi tunawajibu wa kuwatia moyo na kuwafanya wahudhurie vipimo hivyo kila vinapohitajika.

3. Wauguzi tunawajibu wa kuhakikisha mtu huyu anapata chakura bora(lishe bora)ili afya yake iendelee kuimarika

Pia sauti imeweza pazwa kwa kundi lingine ambalo ni Jamii kwa ujumla wake Kwenye sauti tunayoisikia "NITINZE ,NITHAMINI,ILI NIISHI"

Kundi hili kubwa la waathirika wa virusi vya ukimwi linapaza sauti na kuhitaji kuthaminiwa kwa kila eneo

Jukumu la kuwatunza kuwathamini ni la jamii kwa ujumla wake ,japo katika jamii yetu kumekuwa na shida sana katika kuyatimiza hayo.

Wanajamii tanawanyanyapa sana watu hawa ,tunawadharau sana watu hawa, na kuwasababisha wakashindwa kuishi kwa amani, jambo ambalo linasababisha wengi wao kupoteza matumaini ya kuishi ,ndio maana wamepaza sauti yao na kuomba mambo hayo yatendeke katika jamii ili waweze kuishi kama watu wengine.

Kumbuka, Ugonjwa wa ukimwi hauzambazwi kwa kugusana ,kusalimiana ,kukumbatiana au kuongea na mtu mwenye ugonjwa wa ukimwi ;Hivyo basi kama mwana jamii usimnyanyapae mgonjwa wa Ukimwi kwa kukwepa kuongea nae ,kusalimiana nae ,kukumbatina nae ,kucheza nae.

Mbali na kuyatekeleza hayo yote ili kuwafanya wenzetu waishi kwa amani na furaha ,pia kama jamii tunawajibu wa kuendelea kuingua serikali katika suala zima za kupambana na ugonjwa wa Ukimwi na Virusi Vya Ukimwi kwa kutekeleza yale yote yanayoshauriwa ili kuepuka maambukizi mapya na ongezeko la wagonjwa wa ugonjwa huo.

Tekezeleza ombi la wenzetu
(Sauti ya wagonjwa wa Ukimwi na Virusi Vya Ukimwi )"NITUNZE ,NITHAMI I, ILI NIISHI ".Huku ukiyaepuka yafuatayo ;

1. Epuka ngono zembe,hii ni njia kuu ambayo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa katika ueneza ugonjwa wa Ukimwi ,watu wengi hasa kundi kubwa la vijana limejikuta likiongeza takwimu ya wagonjwa wa Ukimwi kwa kufanya ngono zembe;
unaweza iepuka ngono zembe kwa kutumia kinga(kondom),kubaki na kuwa na mweza au mpenzi mmoja,ukiweza acha kabisa suala la ngono.

2. Kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda mtoto,kama mama unaeishi na Virusi vya Ukimwi unawajibu wa kumlinda mtoto wako ili asiweze kupatwa na Maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi ikiwa ni kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa.Mtoto anaweza kukingwa kwa kufuata ushauri wote tunaopewa na wauguzi wetu ikiwa ni kabla ya ujauzito ,kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua

3. Matumizi ya damu salama ,hiki ni kitu muhimu sana hasa kwa wauguzi tunapaswa kuwa makini wakati wa kumuongezea damu mgonjwa yeyote ,pia kwa wanajamii wote tuepuke utoaji wa damu kwa njia zisizo za salama .

Kwa kuongezea matumizi ya vifaa vya ncha kali ,hii ni hasa kwa watoaji wa tiba asili ,ni vyema tukaepuka matumizi ya. Vitu vyenye ncha kali ambavyo havijathibitishwa kwa matibabu na kwa vilivyothibitishwa basi iwe mgongwa mmoja kwa kifaa kimoja .kwani vifaa vyenye ncha kali ueneza kwa urahisi sana magonjwa yanayoenea kwa njia ya damu na kwa njia ya majimaji

MWISHO: Wanajamii kwa ujumla tunapaswa kuelimishana sisi na kuonyana sisi kwa sisi pindi tunapoona mmoja wetu anaenda kinyume na ushauri wa wataalamu wetu wa afya ili tuweze iweka Tanzania salama.

Pia kwa wazazi "samaki mkunje angali mbichi"Ni vyema elimu tunazotizotoa watoto wakishafikia ujana tukawapa mapema kabla ya ujana kwani dunia imebadirika ,itapendeza ukamfundisha mtoto wako mdogo nini maaana ya Ukimwi ,njia zinazoeneza ,na namna anavyoweza ziepuka na aweze kuiweka Tanzania salama ,

PAMOJA TUNAWEZA, TOKOMEZA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI NA UKIMWI

"TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA".

Makala hii "Nitunze ,nithamini ili nishi"imeandaliwa na
Mr amani
SONGEA,
RUVUMA,TANZANIA
 
Tumepokea taarifa mkuu .

Hili ni Jambo muhimu Sana ambalo wanajamii wamelipuuza Sana siku hizi,huenda tumeshauzoea ugonjwa au hofu imepotea baada ya kuwepo hivi vidonge vinavyo fubaza virusi.

Kikubwa ni kujali afya zetu na za wenzetu pia,play safe guys.
 
Back
Top Bottom