Nishani Zimetolewa Pre-maturely?? Zingesubili 2014i!!!!

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,396
12,979
Binafsi nimeshangazwa na njisi sherehe ya miaka 50 wa Tanganyika (Tanzania Bara) zilivyotumiwa kutoa tuzo au nishai mbalimbali. Nimejaribu kufuatilia kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili kujuwa haswa hizo nishani ni za nini lakini nashindwa kupata majibu kamili. Hii inatokana na kwamba sherehe hii ni ya Uhuru wa Tanzania bara lakini kuna mlolongo wa waheshimiwa kibao kutoka Bara na Visiwani ambao wamepata hizo nishani ingawa wengi wao hawakushiri kabisa katika harakati za kudai Uhuru.

Pia utoaji wa hizo nishani kwa watu wa pande zote mbili (Bara na Visiwani) inaonyesha kuwa either ilikuwa ni timing kwa faida za kisiasa au ni kutokana na utata uliopo kwenye mfumo wetu wa Muungano ambapo mambo ya Muungano yanashindwa kutenganishwa na ya Bara.

Inawezekana kabisa kuwa nishani zinaweza kutolewa siku yeyote ila ninachotaka kuuliza, je hizo nishani kama kweli ni za maswala yanayohusu Muungano hazikutolewa pre-maturely?? Nahoji hivyo kwa vile miaka minne ijayo (2014), tutakuwa na sherehe za miaka 50 ya Muungano ambapo ndipo nilitegemea kuwa Nishani/Tuzo zote zinazohusiana na maswala ya muungano zingetolewa wakati huo. Je, kutakuwa na nishani tofauti au waliosahaulika leo kama akina Chifu Adam Sapi Mkwawa na Abdul Jumbe watakumbukwa siku hiyo??

By the way, hivi Bomani na yule Jaji Mkuu enzi za Nyerere (jina limenitoka), Msuguri, ………..wamepata nishani???
 
Back
Top Bottom