nisaIdien tofauti kati ya ZINAA na UZINZI

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,149
Jamani wenye kujua kiswahili vyema embu nisaidien nini zinaa nini uzinzi....
Thx
general ni dhambi
 
Manenohayo yana maana moja isipokuwa asili tofauti. Uzinzi ni neno lenye asili ya kiswahili (kibantu) lenye maana ya ugoni. Zinaa lina asili ya Kiarabu likimaanisha jambo lilelile.
 
Manenohayo yana maana moja isipokuwa asili tofauti. Uzinzi ni neno lenye asili ya kiswahili (kibantu) lenye maana ya ugoni. Zinaa lina asili ya Kiarabu likimaanisha jambo lilelile.

Uzinzi na ugoni japo vinahusiana ni vitu tofauti.
Uzinzi ni kitendo cha kufanya ngono isiyo halali kwa maana ya watu wasiohalalishwa ( mke na mume). Ugoni ni kitendo cha fumanizi katika mazingira ya uzinzi.
Uzinzi ni kitenzi ( verb) Zinaa ni nomino ( noun)...kama sijakosea.
 
vina maanisha kitu kimoja, kulala na mwanamke ambaye si wako. labda ungekuja na issue kutofautisha zinaa/uzinzi na uasherati...ningekuwambia uasherati ni kufanya mapanzi kabla ya kuoa...Mungu anasema, waasherati na wazinzi hawataurithi uzima wa milele.
 
Je kulala na mwanaume asiye wako si Zinaa au uzinzi?
 
Uzinzi ni kitendo cha kulala na mwanamke/mme ambaye si wako kihalali. Zinaa ni matokeo ya uzinzi. Kwa mfano,zinaa inaweza kuwa ugonjwa.
 
Back
Top Bottom