Nirudiane au nisirudiane na mpenzi wangu wazamani?

Yaani nimefikiria sana mateso uliyopitia plus twins on the top. You are a super woman ever. Binafsi ndia naichukulia kama no Wito lakini kaatika Wito huo kama mmoja wao amevunja or Kwenda kinyume na maandiko honestly I don't baby sitting nothing . Yote yanavumilika but not Uzinzi and Abuse . Dear move on with your life. Nenda kawasikilize because ni wazazi nenda na huyo mchumba wako Wa sasa ili asijisikie vibaya. Wasikilize watakachoongea hadi mwisho . Wakimalimaliza waambie wazazi nashukuru kwa mliyooyaongea but now what I want is my Divorce as mnavyoona I moved on with my life after your son abounded me with my kids. Nimeshasamehe yote mliyonifanyia but I can't him back nataka talaka yangu for now that's it. Dada simamia msimamo wako. Na hii iwe fundisho kwa baadhi ya wanaume walio ughaibuni , waliooa bongo na watoto MTU umeshajijua una Familia why usishee na mama watoto wako the Truth uliyoikuta huko mkashauriana kwa pamoja either urudi home Tz or ubaki ughaibuni kwa muda ili utengeneze makaratasi ili uweze kufanya maisha bila kuuumiza Familia zao walizoziacha Tz. Wengi baadhi yao wanachanganywa na hao wazungu kwa ulimbukeni wakiwaona wazungu ni Mali kumbe hamna kitu matokeo yake walichokifuata hawakipati ahadi walizoahidiwa are empty wanaishia kurudi home with nothing . Hapo sasa ndio wanaanza kuyafuta Yale matapishi waliyotapika before wanasahau kuwa kuna different seasons ya kuyafanya Yale matapishi yawe bado mabichi or yawe yamekauka. So too bad kwa baba watoto wako matapishi aliyoyatapika yalikauka na kuzolewa now ni Gold . Kwa sababu you shine now he can see you . Hebu naomba ujiulize dear kama asingerudishwa aka Fanya business na huyo mzungu wake angekukumbuka? The answer is no . So darling move on with all blessings . Even God hates sexual immortals. Aliivunja ndoa mwenyewe . Thanks.

Kule umepita lkn!
 
Unajua maana ya never never never... Kama unajua hutaki kumrudia sasa kikao cha kumrudia unaenda kufanya nini?
Wambie wewe ni mtu mzima mwenye maamuzi yako, hauhitaji vikao vya familia kukusaidia maamuzi.
 
Kuna wanaume hawaelewi thamani ya penzi. Unamkuta mtu ni wa kawaida na maisha ya kawaida lakini akipata kidogo unageuka dodoki. Nafikiri dada ulionesha msimamo hukumrudisha huyo mwanaume katiri. Siku hizi kuna mapenzi ya majitaka sana
 
.. alikupa mbegu basi .. kwanza unaishi na mume tayari mama unataka kuwa na wanaume wawili acha hizo bwana... mwambie umeshaolewa tayari kumbuka una watoto watakuonaje mama yao anapigwa huku na kule bila hata aibu. mwambie mumeo hiyo ndoa kiroho imeshavunjika kilichobaki ni amakaratasi tu lakini kimwili na kiroho nimeshaungana na mwingine na unamfurahiha huyo mume mpya ambaye hakuna any formal thing... marriage si kwenda kwa mchungaji na kuvalishana pete hiyo ni sign tu .. lakini ndoa hutoka moyoni between you two.....

achana na formality just be real... labda kama uniambie kuwa wewe hujui unataka nini maishani mwako? wakati unafurumushwa na mzungu alikuwepo hawakuona umuhimu wa kuweka kikao leo mwanao amerudi maisha yame mfuck ndiyo anarudi kwako (familia ya aliyekupa mbegu ni zaidi ya wabinafsi, mafedhuli, wauwaji na wachawi ) ..... tena usiende kabisa huko ukristo ulikutokea wamempa talaka na wewe dai talaka what so special to him now?

mfyuu nimechukia mwambie wakafungue kampuni na mzungu wake khaaa... WE HUONI KAMA NI MABINAFSI HAYO MAWAKWE YAKO YA MTOA MBEGU

Ha ha ha miss chaga uko vizuri
 
Well said naamini dada atazingatia hili! Akienda ndiyo ataishia.kutishiwa na ishu za,wazazi kumpigia magoti mara kumlilia nwishowe afanye sympathetic decision! Dada usiende please! Waambie kama ni ishu ya watoto wala huhitaji vikao maana tayari umewalea hadi umri huo bila kikao!


Unajua maana ya never never never... Kama unajua hutaki kumrudia sasa kikao cha kumrudia unaenda kufanya nini?
Wambie wewe ni mtu mzima mwenye maamuzi yako, hauhitaji vikao vya familia kukusaidia maamuzi.
 
Wana JF,

Natumaini mnaendelea vizuri na maisha yenu ya kila siku.Nimekuwa msomaji mzuri sana wa posts za watu humu ndani kwa muda mrefu sana na nisiposema nimefaidika nitakuwa muongo,nikaona na mimi nijiunge nipate nafasi ya kusema yale machache ninayoyajua kuchangia discussions za humu ndani. Huu ni uzi wangu wa kwanza kuanzisha humu.

Mimi ni mwanamke niko kwenye late thirties, nilipata ujauzito nikiwa na miaka 18 ndio nimemaliza tu form 4 nikisubiri matokeo niendelee form 5, kijana aliyenipa ujauzito alikuwa anafanya kazi ya kuuza kwenye duka la muhindi Fulani huku akisubiri kwenda chuo kikuu.

Wazazi wa pande zote wakaamua tufungishwe ndoa ya haraka haraka na sisi hatukupinga kwa sababu tulipendana sana sana.Mwaka 1998 tukabarikiwa na mapacha wa kike na wa kiume tulifurahi sana na maisha yakaendela vizuri huku kila mmoja akitafuta nafasi ya kujiendeleza kimasomo.

Mume wangu akapata scholarship ya kwenda kusoma Australia, alipata wafadhili walioahidi kumsomesha degree ya kwanza na ya pili ingebidi ajitegemee. Tulifurahi sana nilimshukuru Mungu nikamruhusu aende tena bila kinyongo kwani nilijua huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mazuri ya familia yetu changa.

Mawasiliano yalikuwa sio kama wakati huu internet caf? ndio ilikuwa habari ya mjini lisaa la kutumia huduma ya mtandao iliweza kufikia elfu 5.Nilijitahidi sana kufanya mawasiliano naye angalau mara moja kwa wiki na yeye pia alifanya hivyo huku nikidhani mapenzi yetu yangedumu na angerudi tuendeleze maisha pamoja.

Alipoanza mwaka wa pili mawasiliano kwa upande wake yalipungua na nilipouliza niliambiwa masomo magumu na muda mwingi anatumia kusoma akifeli ingekuwa aibu na muda uliopotea.Sikupinga hilo na sikulalamika. Kuna wakati ulipita mwezi hajajibu email. Nilianza kupatwa na wasiwasi lakini nilivumilia na nikampa moyo afanye bidii kwenye masomo yake.

Miaka Minne ikaisha na akarudi nyumbani ila sikupewa taarifa. Habari nilizipata kwa mdogo wake wa kike ambaye tulikuwa marafiki sana kuwa amerudi akiwa na muke wa kizungu. Sikuamini masikio yangu nikafunga safari kwenda kwa wazazi wake ambako ndiko alikofikia na huyo mke wake mpya.

Nilipofika sikuwakuta, wazazi wake walinitimua kama mwizi huku wakiniambia sitaki mtoto wao awe tajiri. Ameshapata mzungu na walikuwa na mpango wa kufungua kampuni. Niliumia sana nikajaribu kila niwezalo kumrudisha mume lakini haikuwezekana, nikarudi kwa wazazi wangu na mapacha wangu mwaka 2003.

Baada ya kuona maisha yalikuwa yananiendea kombo. Nilishindwa kufanya kazi zangu na stationery shop yangu ikafungwa kwa kukosa uangalizi. Kwa kifupi nilichanganyikiwa. Wazazi wangu na wadogo zangu walinifariji na kunisaidia sana 2004 nikaanza biashara ya Stationery tena nikiomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii nifaniikiwe ili walionitupa na kunidharau waone mafanikio yangu.

Shangazi yangu akanifundisha biashara ya mbao na hapo ndipo nilipouona mkono wa Mungu. Mambo yangu ya kifedha yakabadilika na mpaka sasa silalamiki. Nikaamua kujiendeleza kimasomo na sasa nina kadegree. Watoto wangu nao wako vizuri wameingia kidato cha tano mwaka huu.

Mwaka 2011 nikutana na mbaba mgane na tukaanzisha mahusiano, mpaka sasa tuko kwenye mahusiano. Watoto wetu wamekubaliana na hali halisi na tunaishi nyumba moja ingawa hatujafunga ndoa. 2014 nikaomba talaka kwa mume aliyeniacha kwa sababu ya mzungu akakataa huku akidai ndoa ya kikristu haivunjwi.

Sasa amerudi sijui nini kimempata na wala sitaki kujua anataka turudiane. Nimekataa kabisa, wazazi wake wamekuja kunibembeleza na kinisihi nimsamehe kijana wao na msimamo wangu ni ule ule. Jumamosi hii kuna kikao nyumbani kwa wazazi wangu, wameomba waje kwenye mazungumzo na mimi niwepo.

Hapa ndio nahitaji ushauri wenu. Niende peke yangu, niende na huyu mpenzi wangu wa sasa au nisiende kabisa. Msimamo wangu ni ule ule siwezi kurudiana.

Hii kitu ilikwendaje? Tunaomba feedback Wide Open EYES
 
Last edited by a moderator:
Dada wamekushauri wengi sana. Ninaandika kwa herufi kubwa makusudi. Kisa chako kinasikitisha kwani ni cha kawaida ila hakizoeleki. Ndoo alichoimba lwambo makiadi kwenye mario. Ndoo ndicho walichoimba vijana wa africa magharibu wimbo premior agauo.
Hapa dada. Unahitaji muda japo wa saa 1. Uwe peke yako sehemu iliyotulia fanya tafakuri na kama ni mtu wa dini sari kwanza. Kisha sikiliza sauti toka ndani yako inakuambia nini? Halafu fuata hilo. Kama itakutuma kurudiana, usisahau tu kutoa sharti la kibinadamu kuwa mpime afya kwanza.
Kila la kheri, mungu akutangulie
 
.. alikupa mbegu basi .. kwanza unaishi na mume tayari mama unataka kuwa na wanaume wawili acha hizo bwana... mwambie umeshaolewa tayari kumbuka una watoto watakuonaje mama yao anapigwa huku na kule bila hata aibu. mwambie mumeo hiyo ndoa kiroho imeshavunjika kilichobaki ni amakaratasi tu lakini kimwili na kiroho nimeshaungana na mwingine na unamfurahiha huyo mume mpya ambaye hakuna any formal thing... marriage si kwenda kwa mchungaji na kuvalishana pete hiyo ni sign tu .. lakini ndoa hutoka moyoni between you two.....

achana na formality just be real... labda kama uniambie kuwa wewe hujui unataka nini maishani mwako? wakati unafurumushwa na mzungu alikuwepo hawakuona umuhimu wa kuweka kikao leo mwanao amerudi maisha yame mfuck ndiyo anarudi kwako (familia ya aliyekupa mbegu ni zaidi ya wabinafsi, mafedhuli, wauwaji na wachawi ) ..... tena usiende kabisa huko ukristo ulikutokea wamempa talaka na wewe dai talaka what so special to him now?

mfyuu nimechukia mwambie wakafungue kampuni na mzungu wake khaaa... WE HUONI KAMA NI MABINAFSI HAYO MAWAKWE YAKO YA MTOA MBEGU

Nakuunga mkono...Sion haja ya yeye kwenda kwenye icho kikao....Kama una AMAN NA FURAHA NA HUYO MWANDAN MPYA BAS..we tulia naye maana siku ukifulia watakufukuza tena....
 
Back
Top Bottom