Nipotoka, nilipo na ninapo tarajia kwenda

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,425
9,818
Nimezaliwa miaka ya 90 mwanzoni, jijini Dar es salaam katika kata ya Sinza. Baba alifariki kipindi nina mwaka mmoja hata sura yake siikumbuki nimeziona picha zake tu na mama alifariki wakati nipo form 1. Nafahamiana na ndugu kadhaa wa upande wa baba na mama lakini sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Chekechea nimesoma shule inaitwa nyota ya bahari ni shule ya kanisa ipo mwenge opposite na kanisa katoliki la mtakatifu Maximillian Kolbe. Darasa la kwanza nilianza shule ya msingi mapambano ipo Sinza, nimesoma mpaka darasa la 3 kuanzia la 4 nikaamishiwa Iringa, tosamaganga nilikua nasoma bweni.

Darasa la saba nilifaulu kwa daraja la juu nikapangiwa kuendelea form 1 katika shule ya sekondary azania iliyopo Dar es salaam. Nilivyofika form 3 nilipatwa na tatizo la kushindwa kusikia vizuri hali iliyopelekea kuyumba sana katika masomo, form 4 sikufanya vizuri, nikaenda kusoma certificate ya procurement and logistics management katika chuo cha uhasibu tanzania(TIA) ambapo niliendelea mpaka bachelor degree. Mwaka 2016 ndipo nilipoingia rasmi mtaani.

Ikumbukwe baada ya mama kufariki nikiwa form 1 sikuwa na ndugu wa kunilea hapa mjini ivyo nilipewa msaada na familia ya jirani yetu. Majirani mtaani walinipenda sana kutokana na sifa ya tabia nzuri pamoja na kufanya vizuri darasani. Ndipo familia moja pale mtaani ikajitolea kunilea. Walikua wazee fulani hivi mume na mkewe walinilipia hela ya kukaa hostel pale azania pamoja na kunikaribisha niwe nafikia nyumbani kwao kipindi cha likizo.

Kuanzia certificate mpaka nimemaliza bachelor degree aisee hata sielewi niliweza vipi nimeunga unga hapo kati msaada wa ndugu, kubet, kuuza baadhi ya mali alizoacha mama mpaka nikamaliza na mwaka 2016 ndipo nikaingia mtaani kama nilivyosema uko juu. Ikumbukwe wale wazee waliochukua jukumu la kunilea walifariki kwa ajali mwaka 2010, waliacha watoto ila hawakuweza kunihudumia kama wazazi wao kitu pekee walichonisaidia ni kuniacha niendelee kuishi palepale lakini mambo mengine nijipambanie mwenyewe.

Baada ya kumaliza chuo nikaanza kutafuta ajira, miaka miwili badae familia ya pale nilipokua naishi ikakubaliana waiuze ile nyumba, kwaiyo hapo sasa mimi natakiwa kutafuta makazi mengine, nikafikiria niende wapi. Nikarudi kijijini alipozaliwa mama Songea kuishi na mama mdogo

Nimekaa pale kijijini nikafikiria nini nifanye, nikagundua pale hakuna michezo ya game tv yaani play station, xbox n.k na mimi nilikua nalo game la play station 2, nikatafuta tv na benchi nikaweka kwenye banda pale pale home kucheza nusu saa jero. Nikawa napata pata hela za kusaidia pale home msosi na kuweka akiba kidogo

Baada ya siku kwenda zikaanza kujitokeza changamoto, nikawa naletewa kesi wanafunzi hawaendi shule wanakuja kushinda kwenye ps wazazi nao wanasema watoto wanaiba hela nyumbani kuja kucheza ps baada ya vuta nikuvute sana mjumbe akaja kuniambia nifunge biashara na biashara ya ps ikafia hapo. Nikatulia tena kufikiria next move.

Nikaongea na ndugu yangu aliyepo Iringa ili kumuomba sehemu ya kuishi niende kujaribu maisha uko akanikaribisha nikafunga safari mpaka Iringa. Nilianza na vibarua vya viwandani maeneo ya ipogolo baada ya wiki tu nilishindwa kutoka kihesa mpaka ipogoro kila siku kazi kuanzia saa 1 asubuhi mpaka 12 jioni alafu malipo shilingi 3000 kwa siku hapo nauli na hela ya kula aisee kazi ikanishinda

Katika pitapita mifandaoni nilikutana na jamaa hapa jf akaniahidi kunipa connection ya kazi za viwandani nikifika Dar. Nimekataa Iringa ramani hazisomeki nikaona nije Dar ile kufika Dar nikamcheki yule jamaa aliniahidi connection akanipiga siasa tu uzuri nilikua nishajiandaa kisaokolojia kwaiyo nikampotezea.

Nimetokea Iringa hapa Dar nilifikia kwa mshkaji wangu. Siku zimeenda katika mawazo ya kujitafuta nimekaa nikawaza ni kitu gani nakijua vizuri ili niamishie juhudi zangu zote uko. Nikavuta kumbukumbu mambo yote ambayo nikiyafanya huwa napata pongezi kwa watu. Nikaandika orodha ndefu nlbaada ya mchujo mkali nikaoata jibu.

Kwanza kabisa kubet. Watu wananiambiaga niwape mikeka ya kubet na mara nyingi huwa inatiki wengine wananipaga shukrani wengine wananitosa nikafikiria kwanini nisitafute mtaji mzuri niwe najilipua mimi mwenyewe

Nikatafuta vidili vya deiwaka nikapata mtaji wa kubet nlianza na 50k siku nyingine nashinda siku nyingine napigwa ila angalao betting inanipa hela ya kula.

Ndoto yangu ni siku moja kuingia kwenye sekta ya michezo mfano kuuza vifaa vya michezo maana nina passion sana michezo sana sana mpira wa miguu.
 
Kijana wewe shughuli unazoziweza ndio zile zile ambazo waafrika wanaziweza, ambazo hazihitaji kutumia akili wala nguvu nyingi, hongera kwa kuwa kwenye kundi ambalo waafrika wengi ndio wapo..
 
Kama ulichoandika ni sahihi basi umejimaliza mwenyewe maana hakuna kitu kinarudisha nyuma watu Kama Uzinzi

Tatizo lako la kutosikia vizuri ungelitumia postively ungekuwa unaandika makala mbalimbali Kama survivor (Mwathirika) wa kutosikia na ungepiga pesa na kuibadilisha kesho yako.
 
Kama ulichoandika ni sahihi basi umejimaliza mwenyewe maana hakuna kitu kinarudisha nyuma watu Kama Uzinzi

Tatizo lako la kutosikia vizuri ungelitumia postively ungekuwa unaandika makala mbalimbali Kama survivor (Mwathirika) wa kutosikia na ungepiga pesa na kuibadilisha kesho yako.
Asante kwa ushauri nitajaribu kuufanyia kazi
 
Back
Top Bottom