Nipeni ushauri nataka kulima kibiashara niende mkoa gani?

Hapn ndio maan natak Kujua A B C
chakufanya rafiki yangu nunua mazao kipindi yanapatikana kwa wingi uyahifadhi... kwaajili ya kuuza kipundi cha njaa...!

hii itakufanya upate mzigo wa kutosha... na muda mwingine kipindi cha njaa mzao hufika mpaka asilimia1 100.... ya bei halisi uliyo nunulia... kimbembe hapo ni store yA kuhifadhia.

ila kwenye swala la kilimo labda ufanye cha umwagiliaji uchimbe visima... kisima kimoja kinaweza kughalimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 20...!

ukitegemea mvua una feli...!​
 
Nenda Morogoro eneo linaitwa Mvuha na faida za eneo hili kwa uchache ni hizi:
1. Unaweza kwenda na kurudi siku hiyo hiyo kama unatokea Dar au Dodoma
2. Ardhi bado mbichi kabisa huitaji mbolea kufanya kilimo
3. Unaweza kulima mazao ya aina nyingi mfano: Mpunga, Mahindi, Ndizi, Ufuta, Mtama, Mbaazi, Nyanya, Tikiti Maji, na Vitunguu maji
4. Unaweza kufanya ufugaji kwa large scale malisho ya mifugo yapo kwa wingi
5. Fursa za biashara ziko nyingi sana
6. Rahisi kupata eneo kubwa na binafsi namfahamu mtu ambaye anauza heka 50 zenye hati kabisa

NB: Nimewekeza pia huko
 
Habari zenu wakuu.

Natak nifanya kilimo Biashara lakini nahitaji eneo kubwa Sana. Je, mnanishauri nianzie wapi kwa wazoefu au wenye uelewa.

Nahitaji ekari Zaidi ya 50.
Nenda ifunda-Iringa, utapata ardhi unayotaka, mvua za uhakika na hata ukitaka mashamba yenye vyanzo vya maji utapata. Naishi Arusha ila ntakwenda huko tarehe 12 au 13 au 14 mwezi wa 4 nina shamba huko. Kama upo interested twende ukatembee upaone na ntakulink na wazoefu zaidi ya maeneo hayo. BUT PLS DONT CARRY MUCH MONEY WITH YOU nipo allergic nazo😃😃😃
Na yeyote alie interested anaweza kunijoin muhimu uwe na hela yako ya kukuwezesha kusafiri kulala kula na pocket money ya mizunguko kwny mashamba.
 
chakufanya rafiki yangu nunua mazao kipindi yanapatikana kwa wingi uyahifadhi... kwaajili ya kuuza kipundi cha njaa...!

hii itakufanya upate mzigo wa kutosha... na muda mwingine kipindi cha njaa mzao hufika mpaka asilimia1 100.... ya bei halisi uliyo nunulia... kimbembe hapo ni store yA kuhifadhia.

ila kwenye swala la kilimo labda ufanye cha umwagiliaji uchimbe visima... kisima kimoja kinaweza kughalimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 20...!

ukitegemea mvua una feli...!​
Mkuu unaonaje umeweka stock ya gunia labda 500 za mpunga ama mahindi, halafu inapita miaka miwili au 3 hamna njaa, au unapata faida ya elf 20 kwa kila gunia?, utakuwa ni uwekezaji sahihi kweli?, angalia muda pesa iliokaa chini na faida iliyopatikana kwa muda huo.
 
broh... kilimo sio mchezo na kueleza kwa uzoefu ukifanya kilimo gharama utakazo tumia ni sawa tu na gharama za kununua... unless otherwise utegemee mvua ambayo ni bahati nasibu siku hizi...!​
 
Nenda Morogoro eneo linaitwa Mvuha na faida za eneo hili kwa uchache ni hizi:
1. Unaweza kwenda na kurudi siku hiyo hiyo kama unatokea Dar au Dodoma
2. Ardhi bado mbichi kabisa huitaji mbolea kufanya kilimo
3. Unaweza kulima mazao ya aina nyingi mfano: Mpunga, Mahindi, Ndizi, Ufuta, Mtama, Mbaazi, Nyanya, Tikiti Maji, na Vitunguu maji
4. Unaweza kufanya ufugaji kwa large scale malisho ya mifugo yapo kwa wingi
5. Fursa za biashara ziko nyingi sana
6. Rahisi kupata eneo kubwa na binafsi namfahamu mtu ambaye anauza heka 50 zenye hati kabisa

NB: Nimewekeza pia huko
Na milima ile ataifanya nini.bora aje huku maeneo ya dakawa dumila maeneo ni tambarale sawa na uwanja wa ndege na aridh inastawisha mazao yote japo ni kwa msimu wa mvua tu
 
Kilimo ni pata potea,utaweka mamilioni ya fedha ukibahatisha kuvuna unakumbana na bei ya soko,mavuno mengi bei inakuwa kiduchu.
Unasema ngoja nipeleke mazao yako nchi ya jiani,mara mkuu wa mkoa wa Arusha kaamka vibaya hakuna kupeleka mazao nje mpaka kibali,kibali lini?
Unapata kibali unakumbana na vigezo na viwango unaambiwa mahindi yako yana WALAKINI...
Bora ununue na kuuza mazao kwanza utengeneze CV ndio uje kujua unalima nini ili kupata nini
 
Umeuliza kizembe sana, siku nyingine usije kutukosea adabu kiasi hicho sisi "much know".

Sasa hausemi unataka kulima nini sisi tutakuelekezaje mzee ?
 
Back
Top Bottom