Nipe ratiba ya mstaafu aliyekaribu nawe

Ndio ni ratiba ya siku nzima kutoka mawio hadi machweo. Nataka kujifunza kitu.

Pia kama mstaafu ni wewe mwenyewe sio mbaya ukashare pia.

Sharing is caring.

Mimi ntatoa ratiba then ntatoa na ushauri.

Morning, Kuamka, kusali, kupata chai
Kufanya mazoezi ya kutembea kwenda kununua gazeti.

Mchana kula chakula na kupumzika
Jioni kwenda kuangalia miradi inaendeleaje Shamba plus mifugo.


Ushauri
Kama umestaafu, usiache kufanya kazi, ukiacha kufanya kazi utaweza kupata magonjwa na kufa mapema Sana.

Ratiba zako baada ya kustaafu ziwe ni zile zile za kuendelea kutafuta hela na kutatua changamoto za watu.

Nasema hivi maana mzee wangu alistaafu akiwa na miaka 60 Ila ameendelea na kazi na yupo around 67 yrs Ila rafiki zake 90% hawapo tena Ila mzee wangu kila siku anazaliwa upya.

Hivyo ukistaafu andaa mradi wowote utakaokuwa unaingiza pesa usikae tu unakula unakunywa na kulala utakufa mapema na magonjwa yatakufata.

Wastaafu wengi hufa mapema kwa hilo tatizo.
 
Nilikuwa nawaza kuandika, makala kwa ajili ya watu ambao wanatarajia kustaafu na ambao wamestaafu ili kutoa, Mambo ya msingi ya kuzingatia.

Nimekuwa nikitoa hii elimu kwa wanajeshi Sana Sana Ila kwa Bahati mbaya bado sijapandisha Uzi JF.

Hapo juu nimeelezea kidogo Ila nikipata muda ntaandika uzi .
 
Kuamka
Kunywa chai
Kwenda kununua gazeti
Kulisoma
Kula cha mchana
Kumalizia kusoma gazeti
Kula cha jioni
Kuangalia taarifa ya habari
Kulala

Japo ni kama jokes lakini huo ndio uhalisia, kuna vitu vya msingi klabisaaa vingi wanakosa kwenye orodha hii, kama kufanya mazoezi, kusimamia vimiradi kidogo, kupanga kukutana na marafiki kwa baadhi ya siku hasa weekends na kikubwa zaidi ibada maana umri wa kustaafu ni changamoto sana ukiwa mbali na muumba wako.
 
Mimi ntatoa ratiba then ntatoa na ushauri.

Morning , Kuamka ,kusali, kupata chai
Kufanya mazoezi ya kutembea kwenda kununua gazeti .

Mchana kula chakula ,na kupumzika
Jioni kwenda kuangalia miradi inaendeleaje ,Shamba plus mifugo.


Ushauri

Kama umestaafu , usiache kufanya kazi, ukiacha kufanya kazi utaweza kupata magonjwa na kufa mapema Sana .

Ratiba zako baada ya kustaafu ziwe ni zile zile za kuendelea kutafuta hela na kutatua changamoto za watu.


Nasema hivi maana mzee wangu alistaafu akiwa na miaka 60 yrs Ila ameendelea na kazi na yupo around 67 yrs Ila rafiki zake 90% hawapo tena Ila mzee wangu kila siku anzaliwa upya.

Hivyo ukistaafu anadaa mradi wowote utakaokuwa unaingiza pesa usikae tu unakula unakunywa na kulala utakufa mapema na magonjwa yatakufata.


Wastaafu wengi hufa mapema kwa hilo tatizo
Madini muhimu sana haya. asante kiongozi
 
Nilikuwa nawaza kuandika ,makala kwa ajili ya watu ambao wanatarajia kustaafu na ambao wamestaafu ili kutoa , Mambo ya msingi ya kuzingatia .

Nimekuwa nikitoa hii elimu kwa wanajeshi Sana Sana Ila kwa Bahati mbaya bado sijapandisha Uzi JF.

Hapo juu nimeelezea kidogo Ila nikipata muda ntaandika uzi .
Andaa kitabu aisee nitakuwa miongoni mwa wateja wako.
 
Naamka saa kumi na mbili asubuhi, naangalia eneo langu lote kama kuna kilichojiri.

Nawasiliana na muumba wangu kwa kutafakari siku iliyopita na kushukuru au kuomba msamaha pale nilipokengeuka.

Nafanya mazoezi mepesi kisha usafi wa kinywa na mwili. Ratiba hii inafuatiwa na kufungua kinywa kwa chai ya moto.

Saa moja na nusu naingia ofisini ambapo napiga kazi hadi saa kumi na mbili juu ya alama.

Baada ya kufunga ofisi nafunga mahesabu na kupata Dinner, naingia mitandaoni kuperuzi matukio hadi saa nne usiku, ambapo nafanya usafi wa mwili na kujiandaa kulala.

Ratiba yangu iko hivyo miaka yote kwa 24/7/365 na sitegemei kuibadilisha. 😂
 
Back
Top Bottom