Nionavyo mimi tuna watu tu lakini nchi na maliasili zake zimeshahamishwa kutengeneza nchi nyingine

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Nianze kwa kusema habarini wakuu ma bibi na bwana ambao wapo humu kuchangia mambo mbalimbali yanayohusu nchi ambayo nchi yenyewe inaonesha imehaishwa sehemu nyingine kutokana na maisha ya maisha magumu ya watanzania

Kwanza nianze kusema kwamba reli ya SGR ni reli ambayo ni mkombozi mkubwa katika sekta ya usafirishaji hapa tanzania kama mradi huu utakamilika kwa wakati, pamoja na kukamilika kwake kitu kikubwa na hatari na cha kushangaza nimekaa nakujiuliza kwanini serikali kupitia kwa waziri wa ujenzi wametangazia umma kuleta mabehewa ya daraja la tatu tofauti na kile tulichotarajia? mimi nimekaa kwenye mradi mda mrefu kwa kuangalia kandarasi inayotekeleza mradi huo katika mabango yao ya mradi wamechora reli ya kisasa kabisa na mabehewa ya kisasa kabisa yakionesha ni mradi unaitekelezwa wa seikali na hawajaishia hapo kazi hiyo wameonesha na nchi mbalimbali walizojenga mradi huo hata mimi nachojiuliza ni lini wanasiasa watasema ukweli kuhusiana na miradi ya watanzania au wanafahamu watanzania hawana uelewa wanavyofikiria?

Mimi naweza kusema huo mradi kama umehujumiwa kwa kutuletea kitu ambacho siyo tulichitarajia ipo siku fedha hizo zitatapikwa na wahusika, serikali kumbukeni kuwa mnaongoza watu wenye akili siyo wanyama au kuku hata mzee Butiku ameshawaambia wiki iliyopita siyo hivo tu serikali ina watu wengi msifikri kama kuna kibaya kimeamuliwa watu wanafrahia wengine wanaamua kukaa kimya kulinda vibarua vyao kwa wakati huo, mmeleta mabehewa ya umeme lakini sisi hatukuhitaji mabehewa yanayovutwa na umeme kuonesha usasa wenyewe la hasha tulichotaka ni usasa wa sgr na mabehewa yake mlichofanya ni sawa na nyumba inayotumia waya wa umeme unahitaji ukubwa wa 2.5 na kutumia ukubwa wa 1.5 mkawasha mkaona hakuna tatizo. kumbukeni kuw fedha hizo ni za watanzania siyo zenu.

Juzi waziri wa kilimo amemhakikishia raisi chakula kipo nachojiuliza hicho chakula kipo kwenye halimashauli zipi mbona watu wanahangaika na bei kubwa za vyakula mitaani haitoshi shule nyingi binafsi zineamua kupandisha kutokana na gharama kubwa za vyakula kuanzia msimu ujao, kumbukeni kuwa mnayomnadanganya mama anakuja kujionea kuanzia mwezi january nadhani hali inaenda kuwa mbaya zaidi, mama mtampa presha na uraisi wake mnashindwa kumwambia ukweli na kumsaidia kwa ukweli malalamiko yanazidi kuongezeka ndani ya jamii wasaidizi wake mnalengo gani au mnaajenda ya siri! mimi nachofahamu kwa nch hii haiwezi tokea raisi kujiuzuru lakini kwa hali navyojionea mama mnamfanya mda wake kumaliza 2025 ikawa bahati nasibu akaamua kabla ya mda kwenda kujipumzikia. Acheni kumsifia na hapendi upuuzi wa namna hiyo za kauli za watu waliovimbewa ndani ya serikali.

Unawezaje kumwambia raisi anaupiga mwingi huku kero zinaonekana ndani ya jamii na ni nyingi umeme, mfumuko wa bei za bidhaa umekuwa mkubwa na hatari kwa watumiaji haitoshi wengine wameamua kutumia clip za bwana yule aliyepita na hapa ndipo watu wanapata hasira na serikali yao hii. Hii nchi ifike mahali mfanye kazi kwa ajiri ya watanzania wanufaike na nchi yao sasa kilichopo ni kama nchi na rasilimali zake zinehamishwa kwenda kwa watu wachache na nchi nyingine, imebaki tu kuwa tuna nchi inaitwa tanzania lakini kiuhalisia kuna wanachi tu ambao wanakaa kwenye aridhi yenye majanga mengi.

Nachojuwa vijana wanaopewa elfu 10000 watakuja na maneno ya dhihaka hapa , nimeona juzi wamepewa pesa na wagombea wao katika nafasi mbalimbali , huko mikoani kidogo wavunjane mikono na miguu kwa vihela vidogo vya kuwapumbaza , kijana wakitanzania jitafakari acha kuburuzwa tetea serikali yako kama inafanya vizuri kosoa serikali yako kama inafanya vibaya, leo utakuwa DC, DAS, RC, RAS, n.k. kumbuka madaraka hayo yanapita umetumiwa unarudi mtaani unaanza kuhangaika kama wengine. msipumbazwe kwa vyeo kwa wanasiasa wanaotengeneza watoto wao kuja kuwatawala kwa kuwapa vyeo ya mda mfupi na wengine kuwa machawa wao. nchi hii ni ya watanzani tunahitaji kuijenga kwa sheria imara ili kuilinda kumbukeni wengi hatujui kesho yetu kwa hiyo ni wazi kuwa katiba mpya ni sasa kwa maisha ya mtanzania na kizazi kijacho.
 
Back
Top Bottom