Nini tafsiri hasa ya neno "uchochezi" au "vitendo vya uchochezi"?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Mtu anaesema mkikamata jambazi pigeni na mtu anaewataka watu wandamane kwa amani kupinga jambo fulani,ni nani kati ya hawa wawili anastahili kuitwa mchochezi?

Mpinzani akitoa kauli kwa wafuasi wake wapige mwizi badala ya kumpeleka Polisi, hatakamatwa kwa kosa la uchochezi?

Maandamano yanayotambulika kikatiba,kisheria utayathibitisha vipi kuwa ni vitendo vya uchochezi?

Tunaposema Katiba ndio sheria mama,huwa tunamanisha nini hasa?
 
Tafsili ya uchochezi kwa kamusi ya Riserekari la maccm ni kudai haki yoyote uliyopewa na katiba ya Jamuhuri ya Tanzania.
 
Kwa sasa hivi maswala yote ya katiba na sheria na katiba yamewekwa kando kidogo, ni mwendo wa matamko ya kukurupuka tu.
 
kwa hili Makonda mumuache ukipiga picha jinsi police walivyouawa majambazi wanapiga risasi gari lililo na police ndani mbele na nyuma kwa kushtukiza na kuua Police wetu wote humo, jamaa walifanya kitendo cha kinyama sana lolote unaweza ukazumgumza kwa mazingira yale ila kwa kuwa sheria zipo zitafuatwa sheria na si kauli ya makonda..
 
Paulo makonda hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi kumi....huyu jamaa ni janga kubwa

Swissyou
Sijui wanaona wanaongoza watu wasiojitambua kiasi kwamba wanaweza kutamka au kufanya lolote mradi tu wew uwe ni mteule wa Bwana mkubwa?
 
Mtu anaesema mkikamata jambazi pigeni na mtu anaewataka watu wandamane kwa amani kupinga jambo fulani,ni nani kati ya hawa wawili anastahili kuitwa mchochezi?

Mpinzani akitoa kauli kwa wafuasi wake wapige mwizi badala ya kumpeleka Polisi, hatakamatwa kwa kosa la uchochezi?

Maandamano yanayotambulika kikatiba,kisheria utayathibitisha vipi kuwa ni vitendo vya uchochezi?

Tunaposema Katiba ndio sheria mama,huwa tunamanisha nini hasa?
Nenda BAKITA mjomba..
Au kama vipi gugo..
Ukishidwa kabisa kamusi mpya haizidi buku 5... itakufaa..
 
Mtu anaesema mkikamata jambazi pigeni na mtu anaewataka watu wandamane kwa amani kupinga jambo fulani,ni nani kati ya hawa wawili anastahili kuitwa mchochezi?

Mpinzani akitoa kauli kwa wafuasi wake wapige mwizi badala ya kumpeleka Polisi, hatakamatwa kwa kosa la uchochezi?

Maandamano yanayotambulika kikatiba,kisheria utayathibitisha vipi kuwa ni vitendo vya uchochezi?

Tunaposema Katiba ndio sheria mama,huwa tunamanisha nini hasa?
Tafsiri ya neno uchochezi kwa watawala walio wengi ni maneno yoyote yanayotolewa na wananchi yanayoikosoa serikali ambayo haitaki kukosolewa.

Lakini wakati huo huo maneno yanayotolewa na watawala hata kama yatakuwa ni ya uchochezi dhahiri, huwa hayaitwi ya uchochezi.

Mfano halisi ni hivi sasa ambapo chama cha Chadema kinaandaa maandamano waliyoyapa jina la Ukuta.

Cha kushangaza sana ni kuwa hata ukikutwa na fulana iliyoandikwa Ukuta ambapo inaweza kuwa kirefu chake kikawa Umoja wa Kuzikana Tanga, lakini Polisi wanakukamata na kukuita mchochezi!

Lakini watu wa upande wa pili wakitoa maneno ya dhahiri ya uchochezi, Polisi huwa wanayaona ya kawaida na hawayaiti ya uchochezi.

Nitatoa uthibitisho mmoja wa wazi kabisa, wakati wa sherehe za Mapinduzi za mwaka huu kule Zanzibar, vijana wa UVCCM walipita na mabango yao mbele ya jukwaa kuu waliloketi viongozi wa kitaifa yakiwa na maneno ya uchochezi wa kutisha yaliyoandikwa CHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA PEKEE......

Cha kushangaza kupita kiasi hatukuona Jeshi la Polisi likiwakamata vijana wale na kuwafungulia mashitaka ya uchochezi, lakini watu wa upande wa pili wakitumia haki yao ya Kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa maoni yao ya kuikosoa tu serikali yao wanaitwa wachochezi!

Halafu wanausalama wetu tukiwaita Policcm, wanaona kama tunawajaribu na wanakuwa 'mbogo' kwelikweli......
 
Mtu anaesema mkikamata jambazi pigeni na mtu anaewataka watu wandamane kwa amani kupinga jambo fulani,ni nani kati ya hawa wawili anastahili kuitwa mchochezi?

Mpinzani akitoa kauli kwa wafuasi wake wapige mwizi badala ya kumpeleka Polisi, hatakamatwa kwa kosa la uchochezi?

Maandamano yanayotambulika kikatiba,kisheria utayathibitisha vipi kuwa ni vitendo vya uchochezi?

Tunaposema Katiba ndio sheria mama,huwa tunamanisha nini hasa?
Hamieni Ulaya. Huko kuna "demokrasia" inayoruhusu vyama vya siasa kufanya maandamano, mikutano ya hadhara na kuikashifu serikali kadri wanavyotaka. Mnatuchosha.
 
Huyo anayesema polisi wawe mahakimu na watesi ndie mchochezi halisi. Wanaodai katiba ifuatwe ni wanaharakati , lakini kwa nia ya kupotosha umma ccm inawaita wachochezi.
 
Tafsiri ya neno uchochezi kwa watawala walio wengi ni maneno yoyote yanayotolewa na wananchi yanayoikosoa serikali ambayo haitaki kukosolewa.

Lakini wakati huo huo maneno yanayotolewa na watawala hata kama yatakuwa ni ya uchochezi dhahiri, huwa hayaitwi ya uchochezi.

Mfano halisi ni hivi sasa ambapo chama cha Chadema kinaandaa maandamano waliyoyapa jina la Ukuta.

Cha kushangaza sana ni kuwa hata ukikutwa na fulana iliyoandikwa Ukuta, Polisi wanakukamata na kukuita mchochezi.

Lakini watu wa upande wa pili wakitoa maneno ya dhahiri ya uchochezi, Polisi huwa wanayaona ya kawaida na hawayaiti ya uchochezi.

Nitatoa uthibitisho mmoja wa wazi kabisa, wakati wa sherehe za Mapinduzi za mwaka huu kule Zanzibar, vijana wa UVCCM walipita na mabango yao mbele ya jukwaa kuu waliloketi waheshimiwa yakiwa na maneno ya uchochezi wa kutisha yaliyoandikwa CHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA PEKEE......

Cha kushangaza kupita kiasi hatukuona Jeshi la Polisi likiwakamata vijana wale na kuwafungulia mashitaka ya uchochezi, lakini watu wa upande wa pili wakitumia haki yao ya Kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutoa maoni yao ya kuikosoa tu serikali yao wanaitwa wachochezi!

Halafu wanausalama wetu tukiwaita Policcm, wanaona kama tunawajaribu na wanakuwa 'mbogo' kwelikweli......

Lakini mkuu pamoja na maelezo yako yooote haya bado hujaeleza tafsiri ya neno "Uchochezi"

Uchochezi ni pale mtu fulani awe mwanasiasa, mwanaharakati au mhamasishaji anapotoa kauli au maneno ya kuudhi au ya kutia hasira ambayo yana lengo la kumfanya msikilizaji (mtu mmoja) au wasikilizaji (kikundi cha watu) kuchukua hatua za kufanya vurugu dhidi ya mtu, kikundi cha watu au mamlaka fulani.

Lakini uchochezi upo wa aina tatu, kwanza ni hiyo ya hapo juu ambayo ni kwa ajili ya kuleta kuvunjika kwa amani.

Pili, ni pale unapochochea bidii ifanyike kwa jambo fulani la kuleta maendeleo au tija.

Na tatu ni kuchochea ili kuleta hamasa ya kuendelea kufutilia kwa makini jambo lolote la burudani au starehe.
 
Umenena vyema sana kuwa uchochezi ni maneno yanayoweza kuleta vurugu kutokana na maudhui yake.

Sasa tujaribu kufanya comparison ya neno Ukuta ambalo kirefu chake ni Umoja wa kupambana na udikteta nchini Tanzania.

Sasa tujaribu kutafakari hivi matamko ya majukwaani ya watawala wetu yanayoisigina waziwazi Katiba ya nchi yetu ambayo watawala hao hao Kabla ya kukabidhiwa madaraka waliyonayo waliapa kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu, je matamko hayo siyo ya uchochezi na yanayoweza kutuletea machafuko nchini?

Sasa ni kwa nini basi wale wananchi wanaotaka nchi yetu iendeshwe kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ndiyo waitwe wachochezi na wale wanaoisigina waziwazi Katiba ya nchi yetu waonekane siyo wachochezi?!

Hivi ni kwa nini wale vijana wa UVCCM waliopita na mabango yao ya ubaguzi yaliyoandikwa kuwa CHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA PEKEE, ambayo ni ya uchochezi wa wazi kabisa, lakini Polisi haikuwakamata na kuwafungulia mashitaka ya uchochezi?

Kwa hiyo wananchi tunapaswa kupaza sauti zetu kwa nguvu zetu zote na kuliambia Jeshi letu la Polisi, liache utendaji wa kazi zake kwa double standard kwa kuwapendelea waziwazi watawala na chama Chao cha CCM na kuwaonea wale wote wanaiokosoa serikali iliyoko madarakani kwa nia njema kabisa ya kuliokoa Taifa letu lisiingie kwenye machafuko.....
 
kwa hili Makonda mumuache ukipiga picha jinsi police walivyouawa majambazi wanapiga risasi gari lililo na police ndani mbele na nyuma kwa kushtukiza na kuua Police wetu wote humo, jamaa walifanya kitendo cha kinyama sana lolote unaweza ukazumgumza kwa mazingira yale ila kwa kuwa sheria zipo zitafuatwa sheria na si kauli ya makonda..

Nonsense, basi hasi kuwa kiongozi. Huyu alimpiga Warioba, siyo mtu huyu.
 
Back
Top Bottom