Nini Majukumu ya Mbunge kwa wapiga kura wake?

wewe ni great thinker ungeweka tittle ingine manake this tiitle inaweza kukudhalilisha. UNGEWAULIZA WATU WA BARIADI (chenge) na Igunga (rostam) kuwa akili zao vipi? UNGEWACONSULT WAROMBO waliomfuta kazi MRAMBA wawaelimishe baadhi ya vichwa ngumu.
 
Wadau kwa heshima na taadhima naomba mnipe majibu kuhusu hii kitu inayoitwa mfuko wa jimbo, Ninachojua kazi ya bunge ni kuisimamia serikali, kutunga sheria na sera, imekuwaje wanawekewa pesa zetu kwenye mifuko yao?

Jamani si kunautaratibu? si kuna bajeti ya serikali kwaajili ya maendeleo? na wao ni wajumbe katika halmashauri wanapanga mipango yote ya maendeleo na madiwani, pamoja na kusimamia shughuli za maendeleo?

Hili sio changa la macho kweli? Ni kazi ya mbunge kujenge zahanati au kituo cha polisi? Sio kazi ya serikali inayosimamiwa na wabunge? Tutakuwaje na sytem ndani ya sytem nyingine kama sio ufisadi huu?
 
Juzi,Regia Mtema alikuja humu na thread ya kushangaa kuwa kuna umasikini wa hali ya juu huko Igunga alipokuwepo RA.However tuli idisscuss hii issue,ama kwa kifupi niliifungulia mjadala.Inaonekana mambo mengine ni hadi watu waone kwa macho.Kusema ukweli nilishajiuliza sana tu kuwa ni kivipi wabunge wako accountable for the development of the people they reperesent.
 
Mbunge wa Rungwe Magharibi Prof David Mwakyusa amekaidi kuhudhuria kuwasikiliza wapiga kura wake walimwandikia barua ashiriki mkutano kujadili mwenendo wa kesi kuhusu mgogoro kati ya wananchi na mamlaka ya maji(TUWASA)akisingizia safari kipi cha maana?pia tangu achaguliwe wananchi wananun'gunika hajaitisha mkutano wa kushukuru na kusikiliza kero zao...anawakilisha nini?
 
Wakuu
Kuna wabunge :-
  • wanasifiwa sababu kipindi cha ubunge wao wanaonekana ndio wamewezesha au wmefanikisha mirai fulani majimboni au wilayani kwao
  • Wanakejeliwa kuwa ubunge wao haujawezesha wilaya au majimbo yao kuwa huduma muhimu za maji, barabara, elimu, nk
  • Wanasifiwa kwa sababu bungeni wanasikika wakihoji, kukosoa au kuomba ufafanuzi wa mambo ya msingi kitaifa
  • Hawasikiki lakini wanakubalika au kupendwa na wapiga kura may be sababu ya uwezo wa kifedha
  • Wanasifiwa na wamechaguliwa sababu ya "usomi" wao wa elimu tu na wananchi wengine wanadharauliwa kuwa hawawezi kuwa wabunge "wazuri" sababu ya elimu yao inayoonekana ndogo.
Sasa maswali
  • mbunge mahairi /asiyefaa anapimwa kwa vigezo gani?
  • Nini hasa majukumu , wajibu na mipaka ya kazi ya ubunge na bunge kama niliyouliza kwenye kichwa cha uzi?
  • je si kuwanyayapaa wakulima kwa kuwbeza watu wenye elimu za form four wanapogombe ubunge?
  • Je wabunge ni watumishi wa umma?
Nawasilisha
 
Imekuwa jambo la kawaida kwa wananchi kuwaomba viongozi wao, hasa wabunge wawasaidie kugharamia miradi ya maendeleo. Mazoea haya yametufanya tusahau majukumu halisi ya wawakilishi wetu na pengine jukumu letu la kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na wajibu wao.

Wabunge wamesahau majukumu yao ya msingi (legislative), badala yake wanajitwika majukumu ya serikali (excecutive). Hali hii pia inasababisha wananchi tusahau vigezo muhimu vya kuchagua viongozi na kutumbukia kwenye mkumbo wa kuchagua viongozi matajiri-ambao nao wanaitumia fursa hiyo vilivyo kuimarisha utajiri wao pamoja na kuulinda.

Ieleweke kuwa sio wajibu wa wabunge kulipia/kugharamia miradi ya maendeleo majimboni mwao. Wabunge wengi wamekuwa wakitoa ufadhili mbalimbali katika majimbo yao, na kusahau majukumu yao ya msingi ya kuwawakilisha wananchi na kuwasilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi na kuisimamia, kuishauri na kuikosoa serikali katika kutoa huduma za jamii na kufanya miradi ya maendeleo.

Aidha, mfuko wa jimbo ambao, wabunge wa upinzania na chama tawala, CCM walisahau tofauti zao na kuupitisha kwa kishindo umekuwa nao ukitumika kama mali ya mbunge na katika kutafuta wema kwa wapigakura, wamekuwa wakiahidi mambo kadhaa huku wakiacha kuwaweka wazi wapigakura. Mwishowe wananchi wanaamini hizo ni huruma za mbunge wao.

Hali hii hakika umetupeleka pabaya kwani umesababisha na unaendelea kusababisha yafuatayo:

Mosi, hali ya wabunge kulipia miradi ya maendeleo kunavuruga utaratibu wa mchakato mzima wa mipango ya maendeleo. Tunazo sera nzuri za kusaidia jamii kuibua miradi ya maendeleo na fursa za hiyo miradi kuweza kugharamiwa. Hivyo wabunge wanapochukua jukumu la kugharamia miradi hiyo, kunafanya wananchi wanakosa imani/hawaoni umuhimu wa kufuata mchakato uliwekwa kwa ajili ya kuwaletea maendeleo na badala yake wanatupia jukumu hilo kwa wabunge.

Pili, hali hii inapunguza uwajibikaji wa pande zote mbili hasa uwajibikaji wa wananchi. Mradi unaogharamiwa na wabunge, unakuwa mradi wa mbunge. Hivyo wananchi wanakosa umiliki wa miradi hii kitu ambacho kinafanya miradi hii isiwe endelevu, na zaidi isiwanufaishe wananchi kwa upana wake.

Wakati mbunge kwa upande wake anashindwa kutumia nafasi yake ya uwakilishi kwa kujenga hoja kwa lengo la kupata fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya wananchi. Hatima yake ni kwamba serikali haioni umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya wananchi kwani mbunge anazo hela na hataki ibainike kwamba serikali/wananchi wanaweza kuendeleza miradi yao wenyewe.

Pia, mwenendo huu wa wabunge husababisha migongano kwenye Serikali za Mitaa; hii hutokea pale panapokuwepo fedha ambazo tayari zimeshatengwa kwa ajili ya miradi husika, ambapo fedha hizo zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja. Wajibu wa mbunge katika hili ni kuwahamasisha wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi hii na kusimamia matumizi ya fedha ya miradi hii.

Tatu, wabunge kugharamia miradi ya maendeleo inachochea hali ya utegemezi ndani ya jamii zetu. Serikali kupitia sera ya ugatuzi wa madaraka inalenga kuijengea jamii utamaduni wa kujitegemea kwa kuitaka jamii ishiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia gharama. Sasa mbunge anapofadhili hii miradi, inafanya wananchi wajijengee utamaduni wa kusubiri kufanyiwa kila kitu. Na ndiyo hali ilivyo sasa kwani mara nyingi wenye fedha ni rahisi kupata madaraka.

Nne, wananchi wanajikuta wanapima viongozi wao kwa ufadhili waliotoa badala ya kutathmini utekelezaji wa majukumu yao kama wabunge. Hii inasababisha watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha kukosa nafasi za uongozi hata kama wanao uwezo wa kuongoza vizuri. Hali imesababisha wananchi wengi kukosa uwakilishi na kuongezeka kwa matatizo makubwa ya uongozi mbovu, ufisadi, rusha na hali ngumu ya maisha huku wachache wakiendelea kunufaika na rasilimali za nchi hii.

Tano, wabunge wanaelemea katika kutafuta fedha za kugharamia miradi ya maendeleo badala ya kufanya majukumu yao ya msingi. Hii imesababisha wabunge kutoonekana majimboni kwa sababu inawabidi watafute mbinu mbalimbali za kupata fedha badala ya kutumia muda wao kutimiza majukumu yao ya msingi.

Badala ya kuwapigania wananchi ili kuwakwamua kutoka hali waliyonayo, wabunge wamejikuta wakipigania maslahi yao binafsi mfano wa sasa wa wanavyopambana kufa na kupona kuhalalisha kupanda kwa posho kwa madai ya kuwa wanatoa hela nyingi kwa wapiga kura kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo. Amenena mtu mmoja kuwa wanatumia fedha za walipa kodi kuwahonga wapiga kura.
 
Nina swali ambalo limekuwa likinitatiza siku nyingi sana hapa nchini nalo ni kuhusu kazi ya Mbunge, hivi kazi ya Mbunge hasa nini (kikatiba) jimboni kwake?

Nauliza hivyo kwa maana mara nyingi nimekuwa nasikia wananchi wengi wanamlalamikia Mbunge wao kwamba hajafanya kitu jimboni kwao kwamba hajajenga Barabara, au hajaleta Maji au sijui hajajenga Daraja, sasa kitu ambacho sielewi Mbunge yeye ana mamlaka gani ya kufanya hayo mambo niliyoyataja?

Kama swala la Miundo mbinu mtoaji na muamuaji Barabara au Maji yawekwe wapi si Serikali, sasa yeye Mbunge ana uwezo gani au mamlaka gani ya kujenga Barabara au daraja jimboni kwake mpaka kustahili kupata lawama zote hizo? naomba mwenye uelewa na haya mambo aweze kunielezea kazi hasa ya Mbunge (Kikatiba ) ni ipi!
 
mbunge kama mwakilishi wa wananvhi serikalini ndiye mwenye mamlaka ya kupeleka kero za wananchi kwa watawala hasa kwenye suala la maendeleo..wananchi kumlalamikia ni haki kabisa kwani ndiye mwenye jukumu la kuwawakilisha na kuwabana watawala watekeleze majukumu yao
 
Nahisi utakuwahuelewi hata maana ya mbunge, majukumu yake ni nini, na anapaswa kufanya nini? Natamani nikupe darasa kidogo lakini nahisi wewe sio mjanja maana ungekuwa mjanja ungeenda hata ku google hilo swali lako
 
Nahisi utakuwahuelewi hata maana ya mbunge, majukumu yake ni nini, na anapaswa kufanya nini? Natamani nikupe darasa kidogo lakini nahisi wewe sio mjanja maana ungekuwa mjanja ungeenda hata ku google hilo swali lako

Funguka tu kama ukipenda hamna haja ya kuleta kashfa kumbuka Duniani hakuna kitu kama swali la kijinga hata wewe unaweza kuwa unajiona unajua kumbe hamna unachojua, na siku zote kwenye majibu pia mtu unapata fursa ya kujifunza ambayo ulkuwa huyajui, kila nchi ina Mbunge na kazi na kazi na majukumu yao hayalingani Dunia nzima, kwa mfano kazi ya Mbunge kama mwakilishi wa wananchi nchi A ni tofauti na nchi B kulingana na Katiba ya nchi husika na ndio maana nikataka kujua kuhusu kwetu kwa hiyo wewe unaweza tu kupotezea wapo watakaoona umuhimu na wataelezea!
 
kazi ya mbuge wa chama gani coz wabumge wa upinzani wanakazi ya kutetea maslahi ya wananchi hasa kuishauri,kuikosoa na kutunga sheria za nchi kwa maslahi ya wananchi lakini wabunge wa CCM kazi yao niku isaidia serikali kujibu hoja za wabunge wa upande wa pili,kwa hiyo nchini kwetu kazi ya mbunge iko hivyo je tukuulize ulichagua wakwenda kukusemea na kukutetea au wakwenda kuitetea serikali?
 
mbunge kama mwakilishi wa wananvhi serikalini ndiye mwenye mamlaka ya kupeleka kero za wananchi kwa watawala hasa kwenye suala la maendeleo..wananchi kumlalamikia ni haki kabisa kwani ndiye mwenye jukumu la kuwawakilisha na kuwabana watawala watekeleze majukumu yao

Na kama baada ya kuwabana watawala bado hawatekelezi majukumu yao, mbunge anapaswa afanye nini? Atafute funds na kutatua kero badala ya serikali?
 
Na kama baada ya kuwabana watawala bado hawatekelezi majukumu yao, mbunge anapaswa afanye nini? Atafute funds na kutatua kero badala ya serikali?

Na hiyo ndio point yangu haswa ambayo mimi nashindwa kuilewa, wananchi kwa mfano wanataka Shule au Barabara ijengwe wanamlalamikia Mbunge wao, Mbunge anapeleka Bungeni malalamiko, Serikali inamwambia hatuna Pesa, Barabara haijengwi, wananchi wanakuja kumwadhibu Mbunge na kumwambia haujatujengea Barabara, sasa huwa najiuliza yeye kama Mbunge afanye nini? Kwani hata tu kusema tu awaambie wananchi wake wachangie haiwezekani bila Serikali kukubali sasa hapo pananichanganya sana kwa kweli!
 
Umeahidi utaifuta CDA tokana na ubabaishaji,lakini sasa wewe ndo umekuwa mbabaishaji.

Shule yako tu inakushnda mizero kibao.

Kweli kuongoza ni kipaji,cjawah hata kuickia sauti yako kwenye vikao vya bunge.
 
Back
Top Bottom