Nini maana ya hili neno "Mikoani"

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,286
1,326
Habari wana wa Nyerere?

Hilo neno huwa linamaanisha nini? Maana watu wakiwa wanaongea utaskia kwa mfano wanasema haya ni mabasi ya mikoani, au...mizigo ya mikoani. Nk.

Tabia hii IPO sana hapa dar, watu wa mji huu ndo utaskia wanasema , nilienda mkoani au niliagiza kutoka mikoani, au unaskia mtu anawabeza wengine kwa kusema " hawa watu wa mikoani" n.k n.k.

Sasa mikoani ni wapi? Na wapi siyo mkoani ? Naomba wanaojua kiswahili watusaidie ktk hili maana huwa halikai vema akilini kwangu pale mtu anaposema mkoani... Najiuliza hapa dar siyo mkoani?

Tafadhali ni kwa ajili ya ufahamu zaidi.

Nawasilisha.
 
Watu wa dar hutumia hiko coz dar ni jiji huwez kuota mkoa so kutofautisha jiji na mkoa ndo kauli hiyo jijin na mkoan
 
Kwa mfano ukiulizwa Tanzania inamikoa mingapi, utajibu nini?

Yote mikoa tu, kuitwa jiji, manispaa, kijiji n.k ni hadhi tu, wataalam wa haya mambo nadhani watakuja kuelezea vizuri
 
Nani Mwana wa Nyerere wewe... Watoto wa Nyerere wote akili zao wanazijua wenyewe....

Star Tv Wakisema Tunapota habari za Mikoani wanaanza na Dar.

Ila Kuna utofauti na Jiji na Mkoa... Hata Pwani ni Mkoa... ila Sio Jiji
 
Unapokua popote pale mkoa mwingine ni mkoani tu..
Uwe dar au tandahimba nje ya mkoa uliopo ni mikoani tuu
 
Kusema haya mabasi ni ya Mikoani ni simply kwamba yanaenda kwenye mikoa nje ya mkoa uliopo wewe
 
Sawa hayo ni majiji lakin dar kitambo na istoshe ndo kila kitu ikulu ipo dar na istoshe kilimo au madin yanatoka mikoan lakin bei inapangiwa dar shekh huon kama dar ndo kila kitu
 
Wakati mwingine matumizi ya lugha hujenga maana kwa minajili hiyo mikoa yooote nje ya Dar-Es-Salaam ni mikoani. Na I am happy asili yangu na ya weeeengi (m 99.99)%wanaoishi Dar-Es-Salaam ni wa mikoani. Angalizo watu wasitumie neno mikoani in a negative way rather ni kutofautisha tu Dar-Es-Salaam na mikoa mingine yooote iliyobaki nadhani hakuna ubaya!
 
Back
Top Bottom