Tanzania imekuwa ni Nchi ambayo mtu yeyote mwenye nafasi anaweza kufanya kitu chochote hata kama kina madhara kwa Taifa. BMK linapigiwa kelele kila kona ya Nchi kwa ajili ya mapesa wanayopoteza kwa kutengeneza Katiba isiyokuwa ya mardhiaono. Cha ajabu kabisa Serikali ya Ccm wanasema Rais kisheria hana uwezko wa kuliepushia Taifa hasara inayopatikana kupita Bmk.
Sakata la IPTL la wizi wa bl 200 Rais hakusema chochote kana kwamba hajasikia chochote. Hii Nchi inatafunwa kwa kila namna lakini husikii Kiongozi wa juu akikemea. Sasa mimi najiuliza hasa kuna sababu gani ya kuwa na Rais kama hawezi kukekemea kuonya au kuliepushia Taifa hasara?.
Hivi karibuni Mh Rais wa Kenya Uhuru Kenyata alisimamia meli iliyokamatwa na madawa ya kulevya ichomwe na kuzamiswa Baharini. Sasa ni kwa nini Rais wetu asichukue maamuzi magumu kama Marais wengine?.
Mimi naamini iko siku Historia itakuja kuwahukumu viongozi wote ambao wamelifanya Taifa hili kama uwanja wa mpira. Mimi nawashauri Watanzania wezangu Tufanye maamuzi magumu kulikomboa Taifa letu kwa njia ya Kura kabla viongozi wezi na wadhalimu hawajaliteketeza Taufa.
Mungu Ibarki Tanzania.