Ningekuwa Rais, hivi ndivyo ningeitengeneza Nchi

mzalendo namba moja

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
390
476
Mambo vipi wana jamvi?

Huu ni mtazamo binafsi tu juu na namna ambayo mimi mzalendo namba moja ingekuwa kama ningepata wasaa huo wa kuitengeneza na kuiongoza (serikali).Nitasema kwa kifupi sana na nitafafanua mawazo yangu kadri tunavyosonga mbele, ruksa kutoa mawazo kinzani, si kwa matusi bali kwa staha na kuvumiliana. Uzi huu haumlengi mtu wala taasisi fulani bali ni mtazamo wangu binafsi wa jumla wa namna serikali zinapaswa kuwa ili ziwe na tija kwa wananchi.

1.WANAWAKE WAPUNGUZIWE KAZI serikalini na kwenye taasisi binafsi ili wapate basi muda wa kutosha wa kulea familia zao hasa kizazi cha watoto ambao kwa kizazi hiki, wanalelewa na watu baki ama wasipate kabisa haki ya malezi ya wazazi kwa sababu ya ubize wa kazi usiokwisha, hivyo iwekwe standard fulani ya malezi na package fulani za fedha na vitu kwa ajili ya kupunguza nahitaji yanayoweza kutokana na malezi yenyewe, malezi yanapaswa kulingana na desturi za nchi hata kama itaonekana kuminya uhuru wa mtu kuwa anavyotaka kuwa ni sawa tu ilimradi watoto wakuzwe kwenye standard na desturi za nchi yetu, hivyo basi sheria kali, na kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kufuatilia hili jambo ni muhimu vikaweko ili kwa atakayekiuka anyanganywe mtoto na apelekwe kwenye vituo maalumu vya kumuwajibisha, wote tunajua taifa huanzia kwenye ngazi ya familia hivyo ngazi hiyo ikiwa na watoto wabovu wasiojali utu wala maadili ni dhahiri kwamba uharibifu wa taifa unakuwa dhahiri pia...mtoto afundishwe utu na maana yake, apate chakula lishe wakati wote wa utoto wake, mtoto afundishwe thamani ya kazi na uzalendo, kwa taifa lake,afundishwe matumizi sahihi ya vipaji na teknolojia, yoote hayo yafanyike mtoto akiwa mdogo ili hatimaye iwe tabia ya maisha yake marefu, model yote ya makuzi ya mtoto kwa walau miaka saba iwe imeandaliwa na ifuatwe kwa msisitizo ili hatimaye kama taifa tuwe na kizazi chenye tija......

IBAINISHWE WAZI KUWA DHAMBI KUBWA KABISA KWA TAIFA NI UBADHILIFU WA MALI YA UMMA NA RUSHWA.

Hapa ninachokimaanjsha ni, ili kutengeneza woga na heshima na usafi kwa mali za umma na kuogopa rushwa ili kuboresha uwajibjkaji wa wananchi na watumishi mbalimbali wa umma, jambo ni moja tu, "adhabu ya kifo cha hadharani kwa muhusika, iwe ni kupigwa risasi, kunyongwa, kuzikwa hai, sindano ya sumu nk" na utaifishwaji wa mali zake, na kizazi chake kimoja kitatumikia kifungo jela na kazi mbalimbali za umma...adhabu hii itaenda kwa wanaotetea ubadhilifu huo kwa makusudi ilhali wakijua ni kosa kisheria, ubadhilifu wa mali za umma uingie hadi katika majaribio mbalimbali ya ukwepajj wa kodi, kama serikali imetoa mazingira safi ya kufanya kazi na biashara hakuna sababu ya watu kukwepa kodi hata kulipa zaidi kama zawadi...

HAKUNA ELIMU YA CHEKECHEA,ELIMU YA MSINGI IWE MIAKA MINNE, MIAKA MINNE IWE KUJIFUNZA UFUNDI NA UJUZI MBALIMBALI KWA VITENDO, MIAKA MITANO KUJIFUNZA UBOBEZI KATIKA TAALUMA MBALIMBALI.

Huku elimu yote ikiwa ni bure, mwanafunzi atajifunza elimu ya maadili kwa wazazi wake Kwa miaka 8 ikiwa ni pamoja na ujuzi wa kujua kusoma na kuandika, kisha atasoma shule ya msingi Miaka minne, kisha kila mmoja kulingana na ulekeo aupendao atajifunza juzi nyingi kadri inavyowezekana na mafunzo ya jeshi ili kuweza kukidhi kupata uwezo wa kujitegemea, kisha miaka mingine mitano au zaidi atabobea katika taaluma fulani kwa mapana zaidi kwa vitendo ili kuwa na base kubwa ya wataalamu watakao lisaidia taifa siku za usoni, huku serikali ikiwa imewekeza katika tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii, wataalam wetu watasaidia katika kutafsiri matokeo ya tafiti zetu katika vitendo ili kuliwezesha taifa kuwa katika upekee wa hali ya juu sana...kwa ufupi mfumo wa elimu usiokuwa na tija nitaufuta mapema mno ili kutoa nafasi kwa mifumo yenye tija kwa wananchi na taifa...

Itaendelea ......
 
Mabeberu wamekaa kama chui mwenye njaa kumrarua rarua kiongozi yoyote wa kiafrika mwenye nia ya dhati ya kuikomboa Afrika. Usifikiri hawa waliopita hawakuwa na mawazo mazuri hususani kwenye elimu.
 
Back
Top Bottom