Ningekuwa mchawi...!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,836
Nimekaa na kuwazua hivi je ni kwanini wachawi ni watu masikini sana na wanaoishi maisha duni yasiyo na mbele wala nyuma?
Nimewaza na kuwazua lakini jibu sijalipata.
Mimi binafsi natamani sana ningekuwa mchawi.
Ningekuwa mchawi ningeifanya mapinduzi ya kisayansi.
Sayansi ya gizani ningeiweka mwangani.
Ungo wangu ningekuwa naupaki pale ubungo,
kipindi cha xmas nauli zikipanda mie navunja bei.
Natangaza nauli elfu tano tu.
Naamini hiyo ingenisaidia sana ku busti kipato cha familia yangu.
Ningewachukua msukule wahandisi wote wakali wa dunia hii na kuwaleta hapa bongo niwatumikishe watujengee viwanda, reli na mitambo kwa gharama ya pumba.
Yaani natamani sana niwe mchawi ili nilikomboe taifa hili maana aliyeliroga kisha kufa,
na sasa tunahitaji mchawi mwenye roho ya uzalendo na taifa letu.
 
Ila huenda mapinduzi unayotaka kuyafanya yakahitaji maalbino zaidi wafe!
 
Siku mtakapoacha ujinga wa kukimbiza MWENGE nchi nzima ndio siku mtakayozinduka!!!
 
uchawi!!!
unaitaji msaada wa maombi kaka.
uchawi si issue wala usitamani.
 
Shehe yahaya wa waislamu anayajua yote haya kwani yeye yupo wazi na uchawi ila tunawaomba wadau wenye contact za huyu sheikh aziweke kwenye mtandao ili mwandishi apate maelezo kuhusu uchawi na hjatimaye atimize kiu yake ya kulikomboa taifa la tz kwa uchawi maana mwandishi anaona wachawi wameshindwa kutumia uchawi wao ipasavyo na ni masikini sana ila nasikia shekh yahaya ni tajiri sana........
 
Back
Top Bottom