Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

Mimi tarehe 14 mwezi huu nilikua na mgonjwa amelazwa nikajilipua kulipa 24 ilikua hiyo hiyo walai Ile siku ninge palalaise kwa maumivu ya moyo kama wasingenikopesha tena.. Ila nililipa 24 nikapewa 30 Safi!

Ila kutokana na sms za wadau humu awamu hii nitalipa endapo Nina excess
Dah mm mpaka leo
 
kama hujui kitu bora kukaa kimya kuliko kudanganya watu.hivi ukikopeshwa sh. 290,000 kwa miezi mitatu na riba ukalipa sh 62,065 hiyoni asilimia 120 kweli? Ni mkopo ambao huwezi kuupata hata huko mtaani. Cha msingi ni uaminifu watu wanakukopesha kukusaidia kutatua shida zako, hawahitaji kukuona bali wanatumia taarifa zako tu na uaminifu wako katika kurejesha mkopo wao ndani ya dakika chache wameshakuingizia pesa kwenye mpesa/tigopesa au aina yoyote ya mobile money unayotumia.

Watanzania tujifunze kuwa waaminifu!
My brother acha jazba halafu tumia ubongo kwa kufikiri. Hiyo riba ya 62,000 kwa mkopo huo kwa mwaka ni asilimia ngapi? Interest Hua inakua calculated kwa mwaka bro. Wewe hapo unaona ni asilimia ndogo kwa sababu huoni mbali. You think in terms of three months. Wise up and think in terms of 12 months and thank me later.
 
Wakuu Sina lengo La kuwadhulumu ila naomba mwenyewe taarifa na hawa jamaa anijulishe nisije kula mkenge Sina pesa ya Akiba nikilipa kama hawatonikopesha tena nitayumba zaidi

Bora hii pesa nielekeze kwenye miradi ili niendelee Kudunduliza nitawalipa hapo mbeleni.
 
Kama una mda mrefu bila kulipa utachukua mda sana tena kupewa mkopo au watarudisha nyuma mkopo wako yaani kama ulikuwa unaweza kukopa 10,000/- wanakupa 5,000/-
 
Wakuu Sina lengo La kuwadhulumu ila naomba mwenyewe taarifa na hawa jamaa anijulishe nisije kula mkenge Sina pesa ya Akiba nikilipa kama hawatonikopesha tena nitayumba zaidi

Bora hii pesa nielekeze kwenye miradi ili niendelee Kudunduliza nitawalipa hapo mbeleni.
Ukikopa deni kumbuka kulipa,kutofanya hivyo ni zuruma.
Umesaidiwa wakati wa shida kwanini usilipe pesa ya watu?
 
Wameajiri masela kwa ajili ya kutuma msg za vitisho,unaweza hisi usiku hauingii ushatiwa kolokoroni.....
 
My brother acha jazba halafu tumia ubongo kwa kufikiri. Hiyo riba ya 62,000 kwa mkopo huo kwa mwaka ni asilimia ngapi? Interest Hua inakua calculated kwa mwaka bro. Wewe hapo unaona ni asilimia ndogo kwa sababu huoni mbali. You think in terms of three months. Wise up and think in terms of 12 months and thank me later.
Kumbuka huo ni mkopo Wa dharula na Wa muda mfupi ambapo ukienda benk hupati, nenda any microfince utakutana na masharti na riba zifananazo na hizo, nenda kwa private lender ndo utakimbia riba zao
 
Back
Top Bottom