Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Melancholic

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
2,230
3,987
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
 
Elimu ya bongo, huwezi maliza mafunzo alaf ukawa competent.

Kwavile ushapata basic knowledge ya ufundi simu, sogea kariakoo au kwa fundi yoyote wa hayo mambo, muombe uwe Msaidizi wake bila malipo, lengo ikiwa ni kupata ujuzi.

Baada ya hapo mambo yatajiset. Ila ukisema uanze kutongoza madem na huku hujajua unatoboaje, mwaka huu pia utaisha ukiwa kwa kaka yako.
 
Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.

Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Kwa jinsi alivyojielezea ni kama kila kitu anasubiri muongozo kwa kaka yake as hana option nyingine yeye binafsi.

Umemshauri vema hapo, aache kushinda home atoke nje connection atazipatia huko
 
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es salaam.

Bac baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa Cctv ila mambo ayakwenda vzr baadae akanipeleka dit nikajifunza ufundi wa simu. Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado auko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.
Basi nikaamua kutulia kwanza home kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau kuna kibinti flani hv nilikitongoza pia kinanipenda sana sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu na tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote naambiwa nafugwa kiukweli hii hali inaniumiza sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: umri wangu ni miaka 30 naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
Mwambie Kaka yako akulipie nusu ya gharama bodaboda..nyingine utalipa mwenyewe taratibu..uanze kazi ya bodaboda..Tena fanya fasta..fanya kazi hii wakati ukijipanga kufanya unayotaka
 
Miaka 30 bado unasubiri kupewa ramani na bro wako, si uingie mtaani upambane.

Hauko serious na maisha.

Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.

Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Vp kaka na wazo langu la kuhama inalizungumziaje?
 
Elimu ya bongo, huwezi maliza mafunzo alaf ukawa competent.

Kwavile ushapata basic knowledge ya ufundi simu, sogea kariakoo au kwa fundi yoyote wa hayo mambo, muombe uwe Msaidizi wake bila malipo, lengo ikiwa ni kupata ujuzi.

Baada ya hapo mambo yatajiset. Ila ukisema uanze kutongoza madem na huku hujajua unatoboaje, mwaka huu pia utaisha ukiwa kwa kaka yako.
✔️✔️✔️
 
Kwa sasa ningekushauri upotezee ishu za madem maana hawatokuwa na chochote cha kuongezea zaidi ya kumaliza hata kidogo ulicho nacho na kuzidisha stress.

Pili Kwa uzoefu uliopata wa mambo ya simu tafuta pahala pa kujishikiza Kwa fundi yoyote wa simu au hata hapo kitaa au chuo chochote kile cha Dar fungua Ka ofisi Ka meza na Kiti Kwa maswala la urekebishaji WA simu zenye tatizo.
 
Miaka 30 bado unasubiri kupewa ramani na bro wako, si uingie mtaani upambane.

Hauko serious na maisha.

Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.

Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Vipi kaka na wazo langu la kuhama unalizungumziaje?
 
Ukisema uuze simu ukapange, hapo ndio utajichanaganya trust me. Bora ukajishikishe kwenye ofisi ya mtu hela uliyouza simu iwe kama nauli na kujikimu, pia ukiangalia maisha ya watu sijui mtu kasonga mbele zaidi yako utajinyonga, maana mazingira ya yeye kufanikiwa na wewe ni vitu tofauti. Cha muhimu Bora usiwe unashinda home halafu achana na madem wa kitaa boss unafeli hapo dharura hazitaisha
 
Kwa sasa ningekushauri upotezee ishu za madem maana hawatokuwa na chochote cha kuongezea zaidi ya kumaliza hata kidogo ulicho nacho na kuzidisha stress.

Pili Kwa uzoefu uliopata wa mambo ya simu tafuta pahala pa kujishikiza Kwa fundi yoyote wa simu au hata hapo kitaa au chuo chochote kile cha Dar fungua Ka ofisi Ka meza na Kiti Kwa maswala la urekebishaji WA simu zenye tatizo.
Ahsante mkuu
 
Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

shida ipo hapo tatizo unataka kuweka heshima kwa huyo demu sioni maendeleo yako kama utomtoaa akili huyo demu
 
Back
Top Bottom