Nina mparachichi ambao huzaa matunda mengi ila una tatizo la kuozesha matunda yake, Nifanyeje?

ashidodi

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
287
334
Ndugu wadau wa kilimo, habari za majukumu

Niende kwenye lengo, ninamparachichi ambao huzaa matunda mengi ila una tatizo la kuozesha matunda yake, uozo unaanzia ndani kwenye mbegu kuja nje ya tunda. Je, nifanye nini ili kuzuia hii hali. Uzao wa tatu sasa lakini tatizo ni lilelile. Naombeni msaada.

Nawasilisha
 
Hata mimi nina mparachichi, mbegu kienyeji ila hauzai. huwa unatoa maua tu na labda utazaa matunda si chini ya 3 na Ni makubwa. Nifanyeje uwe unazaa matunda mengi, maua yanatoka mengi lakini yanaharibika.
 
Dawa za fangasi zina husika.
Aliet ni sh70elf lita moja.
Unatakiwa upige kipindi cha maua
 
Ndugu wadau wa kilimo, habari za majukum
Niende kwenye lengo, ninampatachichi ambao huzaa matunda mengi ila una tatizo la kuozesha matunda yake, uozo unaanzia ndani kwenye mbegu kuja nje ya tunda. Je, nifanye nini ili kuzuia hii hali. Uzao wa tatu sasa lakini tatizo ni lilelile. Naombeni msaada.
Nawasilisha
Kuna dawa za kupiga pindi mti unapotoa maua, na kuna mtego wa kukamata nzi(fruit fly). Nzi hutoboa tunda likiwa changa na kutaga mayai ndani yake. Hii husababisha tunda kuoza.
 
Kuna dawa za kupiga pindi mti unapotoa maua, na kuna mtego wa kukamata nzi(fruit fly). Nzi hutoboa tunda likiwa changa na kutaga mayai ndani yake. Hii husababisha tunda kuoza.
Kunamtu amenishauri nichukue misumari niugongelee mche walau mitano hivi utakaa sawa
 
Back
Top Bottom