Nina damu group O+, Ufafanuzi kuhusu group hii

Hpo kwenye makundi ya damu hakuna shida,(ipo tu kama me ni +ve na ke ni -ve, Ukienda hospitalini ke atachomwa ant-D na yatakwisha).
Kuhusu sababu za kupata watoto wa kike, Kuna "Theories" nyingi katika hili, As far as scientific and biological fact concern kuna hili ambalo limekua likisemwa kwa wingi na kwa salimi nyingi limedhibitika kua ni kweli, kwa ufupi kikubwa ni "timing". Kwa nini timing "ni kwa sababu ya umri wa kuishi mbegu za kiume (XY chromosomes)" inasemekana kwamba mbegu za kiume zinaweza kukaa kwenye via vya mwanamke kuanzia masaa 12-72 lakini hali hiyo inategemea sana mazingira rafiki kwa mbegu hizo, vile vile "Chromosome "X" hustahimili mazingira magumu kuliko "Y", Kwa hiyo wanaofika masaa hayo 72 idadi kubwa waga ni Chromosoms "X". lakini pia Chromosomes "Y" inamwendokasi mkubwa kuliko "X", Kwa maana hiyo "Y" humtangulia "X" kufika kwenye yai ya kike Pale mwanaume apofika kilele. Yai la kike(XX chromosomes) kwa wastani huweza kuishi masaa 12- 24 tangu litolewe kwenye ovari(ovulation).
Kwa mantiki hiyo ni kwamba Mkifanya mapenzi siku 1-3 kabla ya "Ovulation" Mtoto atapatikana wa kike (XX) na mkifanya siku ya Ovulation au mpaka masaa 24 baada ya ovulation hapo mtoto ni wa kiume (XY).

Kuna sababu kama Msongo wa mawazo, Mwanaume kumaliza tendo kabla mwanamke, Idadi ndogo ya mbegu za kiume nk. hizi hupelekea mtoto wa kike kupatikana kwa sababu mazingira ya njia ya uzazi yankua sio rafii kwa "chromosome Y " ambaye hawezi kustahimili hali hiyo ya utindikali mwingi (Acidic) na kumuacha X akipeta.
Vilevile mazingira ya njia ya uzazi ya mwanamke yapokua rafiki (alkaline) kwa "Chromosome Y" basi umahiri wake wa kukimbia haraka humsaidia kuchavusha kama yai la kike likiwepo.

Naomba ieleweke kwamba sababu zote hizi hazina mashiko kama utasahau timing ya ovulation, ili hilo liwezekane basi. NI Vyema mkujadiliana na mkeo ama kufuatilia mzunguko wake kwa karibu sana ili kujua ni siku ipi anakua tayari kupokea mbegu za kiume (Heat) na mimba kutungwa kama mfumo wake utakua vizuri. Kwa wastani wanawake waliowengi wanamzunguko wa siku 28 ijapo wengine hufika 31 Lakini principal ni ile ile kwamba, kipindi cha joto huwafika -3 na +3 ya siku ya kutolewa yai (Ovulation) na kwa mwenye mzunguko wa siku 28, ovulation hutarajiwa siku ya 14 tangu siku ya kwanza mzunguko wake ila kwa wenye 29,30 na 31 Chukua idadi ya siku za mzunguko wake gawanya kwa 2, jibu utakalopata ndio siku yai linatarajiwa kutolewa kisha unaongeza iku 3 mbele na kutoa siku 3 nyuma, kwa kuanzia siku ya 11 -17 ni siku za hatari kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28. hesabu hizo hufanyika kwa hata wnye 29, 30 na 31.
Kuanzia hapo utaunganisha na concept ya timing.

NB: kwa maelezo zaidi na ya kina na sababu zingine tafadhali nendeni hospital au muonane na mtaalamu(Specialist) wa mambo ya uzazi (Gynecologist).
Shukran MKUU mungu akubariki sana
 
Ni kurekebishe kidogo hapo mkuu, Kama huyu bwana angekua Rh+ve na mkewe akawa Rh-ve ingekua nivi.
Mtoto wa kwanza angezaliwa salama ila mimba ambazo zingefuatia zisingeweza kukua, zingeharibika (Misscariage)
hii ni kwakua Huyu mama(Rh -ve) anakua ameshatengeneza kinga za mwili(Antibodies(Ab)) dhidi ya Rh+ve Baada ya ujauzito wa kwanza.
kwakua mtoto anayepatikana kutoka makundi haya ya damu huwa Rh+ve, basi mwili wa mama humtambua kama "Hatari"(Foreign body) kwahiyo basi Rh-ve Ab huvuka uzuio unamtenganisha mama kwa mtoto na kwenda kumshambulia Chembe hai nyekundu za damu za mtoto, hili shambulizi husababisha Upungufu wa damu kwa mtoto (Haemolytic anaemia) ambcho hupelekea kifo chake.
Matatizo kama haya uherekebishika hatua za haraka zitafanyika.

HOSPITALINI.
Mama hupewa Rh immunoglobulin (RhIg) hi kinga dhidi ya Rh-ve Ab anazozizalisha, kinga hii hutolewa katika Hali zifuatazo
masaa 72 baada ya kujifungua
juma la 28 la Ujauzito
baada ya mimba kuharibika, kutoka ama kutungia nje ya mfuko.
Me ni A+ na wife 0- inakuwajee kwenye maswalaa ya uzazi?
 
Me ni A+ na wife 0- inakuwajee kwenye maswalaa ya uzazi?
Kua na magroup mama ya Damu ambayo ni A,B, AB na O. Kuna Kiungo cha ziada kwenye kundi lako la damu ambalo ni Rhesus factor (Rh), Ambapo kama unayo unakua Rh+ kama huna Rh-,
kujibu swali lako makundi yote ya damu yapokua na Rh+ (A+,B+,AB+ na O+) wanakua na wake ambao Rh-ve Shida ipo Rejea Jibu langu hapo juu ulipo ni "quote". Lakina shida haipo kama wanafana Rh factor ama + au -, au mama awe +.
 
Kua na magroup mama ya Damu ambayo ni A,B, AB na O. Kuna Kiungo cha ziada kwenye kundi lako la damu ambalo ni Rhesus factor (Rh), Ambapo kama unayo unakua Rh+ kama huna Rh-,
kujibu swali lako makundi yote ya damu yapokua na Rh+ (A+,B+,AB+ na O+) wanakua na wake ambao Rh-ve Shida ipo Rejea Jibu langu hapo juu ulipo ni "quote". Lakina shida haipo kama wanafana Rh factor ama + au -, au mama awe +.
Sasa suluhisho inakuwa nn mkuu maana wife mjamzito na anajiskia vibayaa kilaa wakatii
 
Sasa suluhisho inakuwa nn mkuu maana wife mjamzito na anajiskia vibayaa kilaa wakatii
Sijajua ni uzao wa ngapi huo, una umri gani huo ujauzito ila mkienda hospitali Daktari atawasaidia na kuwapa njia salama ya kuweka kufika na kujifungua salama.
Usipuuze maumivu yoyote ya tumbo anapokuambia mkeo, Take it serious,Nasisitiza,Nendeni hospitali Mtapata suluhu pale na mama atakua na amani tena.
 
Back
Top Bottom