Nimwache akapange au niondoke mimi?

Kasie umewahi kukaa kwenye mahaba motomoto kwa miaka mingapi na starehe ulizifanya kwa miaka mingapi tunataka tujifunze kutoka kwako

Kwa sasa niko kwenye mahaba motomoto muda mrefu tuu na starehe tunazifanya na Dadii kwa wakati huohuo.

Mkiheshimiana Mahaba kila siku yanakuwa mapya na matamu na hata hamchokani.

K' Matata.
 
Kwa sasa niko kwenye mahaba motomoto muda mrefu tuu na starehe tunazifanya na Dadii kwa wakati huohuo.

Mkiheshimiana Mahaba kila siku yanakuwa mapya na matamu na hata hamchokani.

K' Matata.
Kasie kila unapoandika unaweka K' Matata shauri yako kila siku inataka kuibua swali ila... inaweza ikawa na maana 2 tu basi. ntakwambia maana ya iyo nyingine siku nyingine
 
Kasie kila unapoandika unaweka K' Matata shauri yako kila siku inataka kuibua swali ila... inaweza ikawa na maana 2 tu basi. ntakwambia maana ya iyo nyingine siku nyingine

Usihangaike sana, kuna uzi maalaum wa K' Matata.

Utafute unaitwa mnyambulisho wa K' Matata.
 
Habari wanaJF, naomba mnishauri pia kwa hili.

Nilikutana na binti mmoja mwaka 2012 katika mazingira ya kazini na tukaingia katika mahusiano, binti huyo alikuwa akiishi kwa dada yake mkubwa ambaye wamechangia mama. Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba dada yake huyo alikuwa akimnyanyasa na kitendo kile kiliniuma sana nikaamua kumpangishia chumba akaanza maisha yake hapo, hiyo ilikuwa ni 2013. Tuliendelea na mahusiano mpaka niliamua kujitegemea mwaka 2015 na tangu mwanzo wa mahusiano yetu alikuwa akija mpaka nyumbani kwetu na ndugu zangu wote wanamfahamu. Aliamua kuja kuishi na mimi hivyo nilimkaribisha tukaishi wote, sasa hapa ndo matatizo yakaanza.

Alianza kuzua migogoro ndani na hatukuwa tunaelewana mara nyingi, nilikuwa na biashara nikamweka asimamie biashara ile nilikuwa najua inaingiza kiasi gani lakini tangu aanze kusimamia iliyumba na hakuwa ananishirikisha mauzo ya siku. mostly jibu lake lilikuwa biashara mdogo mdogo, mwaka huo huo akashika mimba na Mungu akajalia akajifungua 2016 March, kipindi hicho nilikumbwa na mtikisiko mkubwa kiuchumi hivyo hali haikuwa nzuri. Katika maisha yetu alikuwa ni mtu wa kufanya maamuzi peke yake na nikijaribu kuhoji inakuwa ugomvi nikaamua kukaa kimya kuepusha shari. Hivyo aliwaleta ndugu zake kuishi kwangu bila idhini yangu maana hali ya uchumi ilikuwa si nzuri. Akaanza kulaumu kuwa ndugu zangu wanamchukia ilhali yeye alikuwa akienda kwetu hafanyi chochote ni kuketi tu muda mwingine hamsemeshi mtu anakuwa busy na simu yake. Tukitoka anaanza kutupa lawama kwangu kwamba ndugu zangu na mama yangu hawampendi. Nilijaribu kumwelewesha na kumwambia kuwa mama hapendezwi na tabia ya yeye kujitenga maana kama anahitaji kuolewa na mimi lazima achangamane na familia yangu lakini haikufua dafu. Hali hiyo iliendelea hata kufikia hatua mama yangu akimpigia simu hapokei kwa makusudi, nikimuuliza anasema hajisikii kuzungumza na simu, mama akipiga kwangu nikimpa pia jibu ni lile lile.

Hali hiyo ilinitesa sana maana nikiangalia maisha yake ya nyuma napata ugumu kumuacha maana namsikitikia mwanangu atateseka sana. Nilifanikiwa kupata kazi nyingine hapa Dar na kuhamia hapa mwaka 2017 July, nilianza kazi vizuri na nikawa natuma pesa za kutumia kama kawaida nilikuwa nikituma laki 2 kila mwezi kwa ajiri ya matumizi, na biashara ile ilikuwa ikiendelea kama kawaida japo sikuwahi kujua mapato yake kabisa. Cha kushangaza ni kwamba kila baada ya wiki mbili niliambiwa hakuna pesa ya kutumia na hakuna chakula mtoto hana chakula pia, ilinibidi nitoe pesa yangu ya kujikimu niitume kwao kitu ambacho kiliendea kuwa hivyo kwa muda wa miezi 5. Wakati mwingine sikuwa na pesa kabisa kwa sababu ya matumizi kwake kuwa mengi na nilijaribu kuhoji pesa inatumika vipi ilizua mgogoro sana. Na alikuwa mtu wa kulalamika na kunitumia sms za matusi[Zipo Zote] kunitukana lakini sikuangalia hayo maana imani yangu ilikuwa ni kujenga familia na huyo dada. Mwaka jana mwezi wa 12 nilimwambia ajiandae ahamie huku hivyo vitu vyote nikampa melekezo avipeleke kwa mama yangu na ndivyo tulivyokubaliana. Nilituma pesa ya nauli Tshs 210,000/= Kwa ajili ya safari (100,000/=) na kumalizia kodi ya nyumba (100,000/=) lakini huwezi amini kabla ya siku moja safari kuanza aliniambia kuwa hana pesa ya nauli nimtumie nauli.

Nilishikwa na hasira sana na tayari nyumba niliwambia wakabidhi kwa mwenyewe, Vitu aliamua kuita ndugu zake wakaja kuchukua bila kunishirikisha. Nilipigiwa simu na mdogo wangu akiniambia mbona mambo yako tofauti na mlivyopanga? kwa hekima niliwaambia wadogo zangu waondoke tu lakini pia haikutosha ndugu zake na huyo dada walianza kuwamwagia wadogo zangu matusi kiasi cha kushangaa kuna nini mpaka iwe hivyo. Nilimpigia huyo dada na kumuuliza kuhusu tukio hilo niliambulia matusi ya ajabu sana na hapo nimetoa tena pesa nyingine ya nauli ili tu mwanangu awe karibu yangu.

Nikajisemea kuwa akifika nitamhoji anieleze vizuri, lakini alipofika alikuwa ni mtu mwenye maneno mengi sana na matusi makali, niliamua kuachana nayo hayo na kufungua ukurasa mwingine wa maisha (Kumsamehe). Tukaishi maisha ambayo kila siku anazua jambo, wakati mwingine namsalimu haitikii, namsemesha hajibu ikafika wakati nikaamua kumtizama tu. Nilipanga niende kwao kutoa mahali mwezi wa 11 mwaka huu lakini kwa tabia hizi sidhani kama naweza. NImeshajaribu kuzungumza naye, kumshirikisha mchungaji wa kanisa analosali, kwa muda fulani nikaona mabadiliko lakini hali ilirudi vile vile. Ilifika kipindi nimetoka kazini nikamkuta ndugu yake kaja kumsalimu, kabla sijaingia ndani nilisikiwa wakinizugumza vibaya sana. Nilichukia sana lakini nikamwambia Mungu kwamba ikiwa mimi ndiye nimemfanya mtu huyu awe hapa sina haja ya kuchukia kwa hiki anachonena kuhusu mimi. Niliingia ndani nikabadili nguo zangu na kutoka kwenda matembezi.

Hivi karibuni kuna ndugu yangu alikuwa anaolewa huko kanda ya ziwa, nikamwambia huyo dada apige hesabu ya mahitaji yake na mtoto kwa ajili ya harusi. Alinipa hesabu yake nikasema sawa ilikuwa around 200K nikatafuta pesa Mungu akajalia nikapata 1M nikamwambia kuna pesa hii imepatikana so wajiandae kwa ajili ya kwenda kwenye harusi. Tulipanga kwenda kufanya shopping the next day. Tulikwenda kariakoo kuanza shopping, cha ajabu yale aliyopanga kununua nikaona anatafuta nguo za mama yake (Kitu ambacho hakuwa amenishirikisha na ilikuwa nje ya budget) nilikaa kimya nikamnunulia mwanangu, yeye alipomaliza kununua alivyokuwa ananunua akanambia anahitaji pesa ya kujinunulia yeye pia.

Seriously nilishikwa na hasira sana maana haikuwa katika budget, na ukizingatia tunakwenda kwa siku chache tu na hatukupanga kufanya yote hayo maana kulikuwa na mambo mengine ya muhumi ya kufanya baada yakurudi dar. Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu maana aliongea maneno makali sana kiasi kwamba nikashikwa hasira nikampa hiyo pesa aliyohitaji, aliema asante but sikumjibu kabisa. Tulikwenda nikijua tunafikia kwenye tukio lakini kumbe kwake ilikuwa ni tofauti tulipo fika alinambia nimpeleke kwa dada yake, nilifanya kama alivyohitaji. Nikategemea asubuhi atakuja ajishughulishe katika shughuli za tukio hakuonekana simu hapokei mara nakuja baada ya nusu saa mpaka ikafika jioni. Kesho yake nikamwambia ajitahidi kuwahi aje kujumuika na kusaidiana na wenzake lakini alikuja saa nne asubuhi na kunifuata moja kwa moja anaomba pesa aende salon. Sikumpa nilimwambia sina maana tayari alishaniudhi. Akaingia ndani kwamba anakwenda kubadili nguo aje kufanya kazi, kumbe haikuwa hivyo akaondoka kwenda zake salon. Sasa tangu hapo hakukanyaga tena kwetu, mpaka siku ya harusi yenyewe ndo akaonekana tena. Tulijumuika na baada ya sherehe kuisha nilianza maandalizi ya kurudi Dar, siku iliyofuata akaniambia anahitaji kuzungumza na mama yangu, mimi na ndugu zangu nikasema sawa. Akatuita tukaketi kumsikiliza akaomba msamaha wa kilichotokea na kuhusu matusi yaliyotukanwa kwenye sakata la vitu na mengine mengi wakamsikiliza na wakamwambia wao hawana tatizo kabisa, akanaambia nimsindikize kwenda kwa dada yake nikamsindikiza.

Huko njiani alinitolea maneno makali sana nikajiuliza kwamba huo msamaha aliokuwa akiomba alimaanisha nini? au alikuwa akiwajaribu ndugu zangu na mama yangu? sikutaka mengi wala sikujibu kitu nikamfikisha nikaondoka. Sasa mwezi huu ilikuwa niende kwao nikatoe mahali lakini moyo wangu sasa haumuhitaji tena maana naona tunakoenda nitafanya kitu cha ajabu juu yake kinachoniumiza ni mwanangu tu.

Nilimweleza kuhusu kuachana mimi na yeye akasema ataenda kupanga chumba hapa hapa Dar kitu ambacho nikifikiria mazingira hayo kwa mwanangu siyo kabisa, naombeni ushauri wenu nifanyeje? maana jambo hili limenichosha sana. binti ni mzuri but tabia zimenishinda
Pole sana kiongozi. Katika haya uliyoyasema nimeona yafutayo
1. Mwanao anatumika kama mtaji kwako. Na inaonekana mkeo ameshajua kuwa kwenye ishu ya mtoto husemi kitu......
Kwenye hili unakosea sana. Kwa kumtumia mtoto UTAPATA TABU SANA... Kumbuka, kuna watoto hawana wazazi na wanishi. Sembuse wewe ambaye upo na una uwezo wa kumhudumia. Kuendelea kuishi na mtu wa hivyo UTAKUJA KUFA KWA PRESHA AU UFANYE KITU CHA AJABU HAPA DUNIANI HADI UJE KUJISHANGAA.... Mwache akapange na utatakiwa kumpunguzia mahitaji. Maana akishahama, atamtumia sana mtoto kupata hela. IKIWEZEKANA TENGENEZA MAZINGIRA AKUPELEKE USTWI WA JAMII, Huko lazima ukang'ang'anie kupeleka hela ustawi na yeye akazichukulie kule

2. Unafanya maamuzi ya kukaa kimya na kutochukua hatua IN THE NAME OF naepusha shari... Hii ni hatari.. Kaa kimya lakini lazima uchukue hatua. Unatukanwa mitusi ya HAJA eti unakaa kimya..!!!! UNADHANI HALI HIYO ITAISHA LINI? CHukua hatua... Mpeleke kwa wazazi wake au ndugu zake wengine mkayazungumze. UKIACHA, UTAKUJA FANYA MABAYA NA MENGINE YA KUUWA AU KUISHIA GEREZANI

3. UTARUHUSUJE NDUGU ZAKE WAKUTUKANE? HOW YAANI..!! Na inawezekana anapanga hayo na ndugu zake. Kama wana uwezo wa kukutukana kiais hicho, IPO SIKU WATAKUPIGA MAKOFI na nhutakuwa na cha kufanya

4. Umeacha hali imekuwa kiasi cha ndugu wa mkeo kuwatukana ndugu zako...!!! WHAT KIND OF FAMILY unaijenga? Huoni kwamba uwepo wake umesababisha magomvi katika familia? TO ME, KWENYE HILI UNAIHITAJI KU-DISPLINE MMOJA KATIKA NDUGU ZAKE ILI WATIE ADABU. Na wakiona wanakuweza, hawataishia hapo. KUNA SIKU MAMA YAKO MZAZI ATAKULA MAKOFI, kama si toka kwa mkeo basi NDUGU ZAKE....

5. HOW dare you...!!!! Umenunua vitu, unamuamisha mkeo, unaacha maamuzi kuwa vyombo viende kwenu, all of the sudden, VITU VYOTE VINAKWENDA KWA NDUGU WA MKEO, and you are there watching vinaenda...!!!! HOW DARE YOU ...!!!!! Yaani mkeo hafuati instructions zako bado UNATAKA UKALIPE MAHALI...!!!! MY FRIEND, KAMA AMEWEZA KUFANYA HAYO KIPINDI CHA KUBEMBELEZA NDOA, EXPECT DISASTER HUKO MBELE YA MAISHA ...>>!!! TRUST ME... nakushauri umuache huyo mwanamke... MATABIA ALYOYAONYESHA MAGUMU SANA...

6. Hiviii..!!! inakuwaje hela nyingi unazompa mkeo, ni baada ya kuwa na hasira tu? Yaani wewe unatoa hela ili kuzuba mdomo wa mwanmke wako asikutukane au asifanya maajabu..!!! HAYA, BAADA Y AKUMPA HELA MARA KADHAA KWA HASIRA, ameacha ujinga wake? Na kwa kumpa kwako mara nyingi kwa sabau ya hasira.. MWENZIO KESHAJENGA KICHWANI KWAKE KUWA, ILI APATE HELA KWAKO, LAZIMA AFANYE UJINGA....Hayatakuwa na mwisho hayo..... HATA NINGEKUWA MIMI, KAMA NIKIKUUDHI NDO UNATOA HELA... naanzaje kuacha kukuudhi?

MWISHO NAKUSHAURI MUACHE KABISA... MATESO UTAKAYOYAPATA KWA KUISHI NAYE MAISHA YAKO YALIYOBAKIA YATAKUWA MAKUBWA SANA..... Matatizo ya kisaiklojia utakayo mpitisha mtoto wakati mkiishi pamoja ni makubwa kuliko mkiachana....

Ngali K
 
Na alikuwa mtu wa kulalamika na kunitumia sms za matusi[Zipo Zote] kunitukana lakini sikuangalia hayo maana imani yangu ilikuwa ni kujenga familia na huyo dada.
DAH AISEE WATU SIJUI MNA UVUMILIVU WA AINA GANI..MI SIWEZI NAMZINGUA MAPEMA KABISA..SMS ZA MATUSI..HAPANA...LABDA MI NINA TATIZO MAANA HAPO MI NAONA KAMA ULIANZA KULEA UJINGA MAPEMA
 
maana jambo hili limenichosha sana. binti ni mzuri but tabia zimenishinda
HATA ULIVOMALIZIA BASI TU HATA KUKUITA ZOBA BBWEGE NIMEPUNGUZA TU MAKALI,...WEWE NI MS....FALA KABISA...WAPO WASHAURI WANAKUSHAURI TU SUIWAZE..BASI KAMA NI MZURI VUMILIA MATUSI NA MSIKILIZE KILA ANACHOTAKA....USIMUACHE MSIKILIZE TU VUMILIA KILA KITU...BWEGE KABISA WE TUOMBE MSAMAHA WANAUME WENZAKO
 
Baba yake ni Mjita na mama yake ni Muhaya, lakini wazazi wake walishatengana hawako pamoja
Hahahahhahhahhahhah yan hapo ndo nimepata sababu ya yote anayoyafanya, ogopa sana kuoa mwanamke wazazi wake wametengana na watoto wakakimbilia kwa maza asiye na akili akawalea kwa kuwalisha sumu kuhusu baba yao, wakifika kwenye ndoa wanaanza kufanya practices, hayo in malezi wala hutambadirisha kwa lolote lile, pigs chini ndo ushauri was mwisho, yaliwah kunikuta hayo
 
Nimesoma story yote Na geji ya hasira ilikua inazidi kupanda hapa nilipo nimebadilika rangi nimekuwa mwekundu Na nilichogundua Umetoka kwenye familia yenye upendo wa AGAPE..!! Aiseeh we jamaa ni mvumilivu sana sana!! huyo ilitakiwa apate mtu kichaa kama mimi..!! Mwanamke kamwe nasema kamwe hawezi kuniletea ujinga anaokufanyia wewe!!
Nasema angekua na mimi angepata tabu sana nasema angepata tabu sana!! hayo yote aliyokufanyia kwangu asingejaribu.
Kisa mtoto? Nop Nop Upuuzi sitaki kabisa.
We jamaa una chembe chembe za ulokole ndani yako.!! wengine tunazo lakini mwanamke anavotaka kupanda kichwani huwa zinaondoka.
Pole sana kiongozi.
 
Nilimvumilia nikijua atabadilika lakini kadiri siku zinavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya zaidi, maana mpaka sasa kajenga uadui na ndugu zangu na mama yangu pia bila sababu yoyote
We huchepuki? Au hajawahi kukufumania?
 
hasira zimenifanya nisimalize kusoma hii hadithi yako.
kiufupi tu...inatia hasira sana. hata shetani anakushangaa
 
Anakutukana? Mwanamke unaishi naye ndani anakutukana? How? My fellow men nisaidieni...

Ni matusi gani hayo? Ya nguoni au yapi????
 
Usioe kichaa huyo chukua mwanao mwache akaishi anakotaka dunia itamfunza tu......mwanamke gani mwendawazimu huyo we nae una moyo sana hongera ingekua me ndiye mwanaume nilishafukuza hiyo mburukengez zamani sana
 
Anakutukana? Mwanamke unaishi naye ndani anakutukana? How? My fellow men nisaidieni...

Ni matusi gani hayo? Ya nguoni au yapi????
Huyu labda karogwa ....hata nichukie vipi siwezi kumtukana mwanaume wangu zaidi nitanuna hata mwezi siongei ila sio matusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom