Nimetembelea shule za Dar es Salaam wanafunzi bado wanakaa chini mchangani, sijui mikoani kukoje!

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,528
8,187
Leo nimepita shule ya msingi Upendo iliyopo Mbezi Luis jijini Dar es Salaam. Kwanza shule ina wanafunzi wengi kuliko uwezo wa madarasa mpaka wanaingia kwa shift.

Pili shift husika inabeba wanafunzi wengi mpaka wengine wanakaa chini tena sio chini kwenye sakafu, ni chini kwenye mchanga. Unaweza kusema labda wamechelewa kumalizia sakafu kipindi hiki cha kufungua shule, madarasa yamechakaa yakionekana ni ya muda mrefu bila kuwekwa sakafu. Mwalimu hawezi kupata morali ya kufundisha kwenye madarasa hayo na ratiba iliyomzidia.

Hivi ule mkopo wa benki ya dunia ndio walisema wamepeleka kwenye madarasa? Na pesa za Tozo wakasema zinaingia humohumo..

Upendo Secondary.jpg

Pichani ni wanafunzi wa darasa la 3C shule ya msingi Upendo iliyopo Mbezi Luis Dar es Saalam wakiendelea na vipindi baada ya shule kufunguliwa​
 
Zile pesa va uviko 19 zilikwenda wapi !. kuuliza ruska maana bado ugonjwa unatafuna watu
 
Hebu tuletewe na wanafunzi wa SMZ je tupo sare sare kwa hali zetu? Tunataka tujue sisi sote kama raia wa Jamuhuri ya muungano wa TZ.
 
Hilo darasa sio kwamba halijawekwa cement. Ukweli Ni kwamba liliwekwa cementi ya mchongo bila zege. Muulizeni mwalimu mkuu kwanini amefanya hivyo. Kwanini aweke floor ya michongo?

Kuhusu watoto kurundikana Ni kwamba mzazi akiambiwa idadi imetosha akilalamika anaambiwa na mwalimu Fulani wa kike mwenye ukaribu Sana na mwalimu mkuu atoe hela ya beer mtoto aandikishwe.

Wao wenyewe wamejipangia kufundisha darasa la Saba ambàko hakuna msongamano. Mziki wanaupata walimu wa darasa la kwanza.
 
Miti ya mbao ipo mingi Tanzania tunafeli wapi? Hapo hatujaja kwenye mkakati wa serikali wa kugawa tablet kwa wanafunza, kama hili la madawati tumeshindwa karne ya 21.
 
Vipaumbele ndugu, wanapenda vieiteee 😁
Vipaumbele Ni magari ya milioni Mia sita.
Gari Kama la Mwigulu lile la serikali la milioni Mia sita lingeuzwa nadhani tunaweza kupata vyumba sita vya madarasa na madawati hamsini. Ungiongeza na service ya gari na mafuta kwa mwezi, tunaweza kuajiri walimu watano wa msingi.

Piga Mara mawaziri wote na manaibu. Tatizo la vyumba na madawati itakua historia. Ukiongeza na ya makatibu wakuu na banaibu wao. Tunaajiri waliku elfu kumi wa sekondary. Lakini who cares after all wanaosoma shule za kayumba hatutegemei watakua viongozi wa kesho, Hawa watakua wapiga kura tu.

Viongozi tayari wameandaliwa, Ni watoto wa kina Mwigulu, dada Joy, Malima, Makamba, Nape ( watoto wa Bashiru na Lukuvi hawamo kwenye list hata wa yule kalamaganga)
 
Kwamba hujui hali ya mikoani ikoje?!; Hali halisi ndio hiyo! Maana hapo umefika Mkoa wa Dar Es Salaam, Wilaya ya Ubungo, Kata ya mbezi.

Hali halisi ya shule katika mikoa yetu ndiyo hiyo
 
Leo nimepita shule ya msingi Upendo iliyopo Mbezi Luis jijini Dar es Salaam. Kwanza shule ina wanafunzi wengi kuliko uwezo wa madarasa mpaka wanaingia kwa shift.

Pili shift husika inabeba wanafunzi wengi mpaka wengine wanakaa chini tena sio chini kwenye sakafu, ni chini kwenye mchanga. Unaweza kusema labda wamechelewa kumalizia sakafu kipindi hiki cha kufungua shule, madarasa yamechakaa yakionekana ni ya muda mrefu bila kuwekwa sakafu. Mwalimu hawezi kupata morali ya kufundisha kwenye madarasa hayo na ratiba iliyomzidia.

Hivi ule mkopo wa benki ya dunia ndio walisema wamepeleka kwenye madarasa? Na pesa za Tozo wakasema zinaingia humohumo..

View attachment 2476017
Pichani ni wanafunzi wa darasa la 3C shule ya msingi Upendo iliyopo Mbezi Luis Dar es Saalam wakiendelea na vipindi baada ya shule kufunguliwa​

Angalia usije ukatekwa, huu ukweli hautakiwi kwenye hizi zama za kuupiga mwingi.
 
Tatizo lingine kubwa la nchi hii ni overpopulation. Kama kasi ya ukuaji idadi ya watu haitadhibitiwa ili iendane na kasi ya ukuaji uchumi madarasa na madawati hayatakaa yatoshe.
Kuna rais aliponda matumizi ya Contraceptives pia akahimiza watu wazaane mpaka mayai tumboni yaishe na akiahidi atatoa huduma zote bure huku Waziri wa Afya naye akikazia kwa kupiga makofi na meno nje nje... imekuwaje leo twashangaa population yetu?
 
Back
Top Bottom