Nimesikitika kukutana na nakala na cheti cha shahada ya Uhandisi kutengenezwa kifungashio

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,331
24,215
Kweli hiki ni kiashirio cha usomi kukosa maana katika jamii!
Nimeenda pharmacy kununua dawa, nilipofika nyumbani kucheki kifungashio nakuta nembo ya usomi, UDSM.
Kila aliyepita pale UDSM anaifahamu.
Kutazama vizuri naona ni nakala ya cheti cha mtu, tena cha uhandisi nilikopitia mimi!
Nikasikitika sana tena sana!

Certificareof academic achievement sasa ni kifungashio, hata kama ni discarded photocopy!
Cheti kinasoma :
This is to certify that "ABRAHAM JACOB MSURA"
........ DEGREE OF BACHELOR OF SCIENCE IN
ENGINEERING

WITH HONOURS Second Class Upper Division.

Nimechoka kabisa, usomi hauna maana.
Naenda kuuza kifusi.

1.png
2.png
3.png
 
Zipo nakala nyingi sana hasa za mitihani, vyeti etc. Nadhani nakala za kuombea kazi mahali hukusanywa na baada ya muda kutolewa kwa wadau wa kuziharibu (kwa kuchomwa, ama kupelekwa viwanda vya kutengeneza mabox, karatasi, tray za mayai, etc )
 
Sio original ni copy shenzi original anayo shida nini Mimi mwenyewe copy nazifanyia summary za hesabu Ila original zipo laminated
Hata kama siyo original, kujidhalilisha na kudhalilisha fani kwa kutengenezea vifungashio copy ya cheti chako, ni kuridhika kudharaulika.
Katika hilo ukilikubali binafsi, basi hatuwezi kukusaidia maana unaweza kutumika kama door mat kupangusia matope kabla ya kuingia ndani ya nyumba, na mwenyewe ukaridhika tu.
 
Hio plain paper tu iliyopakwa ink hakuna cha ziada
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom