Nimenasa sauti ya Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Mbogwe, Ndg. Jacob Rombo akiiba mafuta ya Serikali

Hapo hakuna ushahidi wowote kuwa aliyefanya hivyo huyo aliyetajwa na kama hayo mafuta ni ya serikali.
Lakini kama ni kweli,Mwamba anatuangusha watumishi wenzake.Wenzake leo wameshtakiwa kwa kupiga zaidi ya bilioni 1.2.Yeye anapiga laki mbili tu.
 
Majambazi wa kutumbua hao

Badala ya kushirikiana na Mkuu wa Wilaya kutatua matatizo ya wananchi ye yupo kuzunguka sheli kuiba mafuta.
Ndiyo maana huwa hawatutetei mafuta yakipanda.
 
Wewe umethibitisha hiyo sauti ni ya huyo kiongozi? Kama huyu mdude ana ugomvi nae akaamua kumtengenezea zengwe tutajuaje sisi. Usikurupuke kutoa hukumu kabla hujajiridhisha.
Sauti ni Yake na huyo dada Mweupe wa Hapo sheli ni sauti yake wote nawafahamu hapo..
 
mambo mengine ni mepesi sana kuyasema na kuripoti ila kuthibitisha sasa 🐒

kumbuka Sheria ni msumeno hukata pande zote 🐒
Si ndio mnajifichia kwenye hicho kichaka cha sheria kwa vile mnaona mna hongo za kupindisha ukweli !? Lakin hiyo haibadilishi kwamba ni mwizi na mbadhirifu wa mali za umma
 
DAS alipaswa kumtuma dereva akamaluza hiyo kitu.

100% ya madereva wanapiga za mafuta.

V8 zinaandikiwa 1L Kwa km 5! Wakati za kisasa full umeme zinatumia 1L Hadi km 15!!

Kuna vituo teule vya kujazia mafuta. Hapo kama unachota noti kisiama kitaidai serikali.

100% wanafanya hivi.
 
Si ndio mnajifichia kwenye hicho kichaka cha sheria kwa vile mnaona mna hongo za kupindisha ukweli !? Lakin hiyo haibadilishi kwamba ni mwizi na mbadhirifu wa mali za umma
hayo si maneno tu ambayo hata hivyo bado hujasema yote 🐒

mtu anajifichaje na unaona, na kichaka kiko wap dhidi ya upotoshaji na aina hiyo hiyo ya malalamiko kila wakati 🐒

ni kawaaida kutengeneza script na kuzusha ati jambo fulani liko hivi au vile. Hakuna wa kubabaika na hizo now days 🐒
 
Huyo Mtu anayetajwa ninamfahamu ni Rafiki angu wa Muda mrefu japo Tangu Tukiwa Mzumbe..
Na Mpaka CCM tumekaa Pamoja "Jaju" ninafahamiana naye sana na nakiri kwamba hiyo ni sauti yake..

Sema "Jaju" Naye amezidi Beef na Wapinzani kutokana na kuwabana sana kwa Hoja..
 
Ma DAS vibaka mnateteana
 
Wezi wakati watanzania wote ni wezi.

Utakuta mtu hapa Jf anawasema wezi huko aliko kama ni mfanyakazi anampiga boss.

Kama ni biashara anakwepa kodi
Watu wanapiga hadi pesa za kanisa, misiba shereh.

Kiufupi watanzania sio waaminifu kuanzia wananchi hadi viongozi.
 
Ndugu watanzania wenzangu wavuja jasho wa nchi hii, hiyo sauti mnayoisikia ni ya katibu tawala DAS wilaya ya Mbongwe mkoani Geita akiiba mafuta ya serikali kwenye moja ya vituo vya mafuta vilivyopo wilayani hapo.

Tukio hili limetokea January 2024 katika kituo cha mafuta kiitwacho Minzingo kilichopo Masumbwe wilayani Mbongwe.

Katika sauti hii DAS huyo anasikika akimuambia mhudumu wa kituo cha mafuta ampe pesa kash Tsh. 235,000/- kutoka katika fungu la mafuta ya serikali. Mhudumu anamjibu DAS huyo kuwa yeye kama mhudumu anaruhusiwa kutoa mafuta na sio pesa. Lakini Katibu tawala huyo mr. Jacob Rombo anamlazimisha mhudumu huyo ampe pesa hizo huku mhudumu akihofia kupoteza kazi kwani kitendo hicho ni kinyume na maadili yake ya kazi. Baadaye mhudumu huyo analazimika kumpa pesa hiyo huku akiwa na wasiwasi na katibu tawala huyo akijaribu kumfariji na kumtania kumuita shemeji.

Kitendo hiki kimeuumiza moyo wangu ukizingatia kwamba kabla ya uteuzi wa katibu tawala huyu kulikuwa na (mchujo) vetting. Nasikitika kwamba Samia alijua ameteuwa mtu mchapakazi ambaye anaenda kumsaidia kazi yake kule Mbongwe kumbe kateuwa jambazi linaloenda kuhujumu uchumi wa nchi. Bado najiuliza idara ya Usalama wa taifa ilikuwa wapi kumshauri Samia kuhusu uteuzi wa katibu tawala huyu mwizi na jambazi wa mali za umma? Idara ya Usalama wa taifa pale Mbongwe wanafanya kazi gani kiasi kwamba wizi wa mali za umma namna hii hawajui?

Katika mazingira haya, mimi kama mwanaharakati na mdau wa utawala wa sheria na uwajibikaji nazitaka mamlaka zinazohusika kutengua uteuzi wa katibu tawala huyu. Pili akishatenguliwa haraka sana akamatwe na kufanyiwa ukaguzi ili kujua hayo mafuta ameiba kwa muda gani na afikishwe mahakamani.

Hatuwezi kukaa kimya wakati wananchi wanalia na gharama kubwa za matibabu halafu kuna DAS mmoja anakunja laki 2 kila siku za wizi wa mafuta ya serikali.
View attachment 2941340
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Jamaa ameshakalia kuti kavu walahi....
 
Huyo Mtu anayetajwa ninamfahamu ni Rafiki angu wa Muda mrefu japo Tangu Tukiwa Mzumbe..
Na Mpaka CCM tumekaa Pamoja "Jaju" ninafahamiana naye sana na nakiri kwamba hiyo ni sauti yake..

Sema "Jaju" Naye amezidi Beef na Wapinzani kutokana na kuwabana sana kwa Hoja..
actually naweza kukubaliana nawe kwa kiasi, kwamba ikibainika na kuthibitika ni yeye, nae basi amezidisha na kuendekeza njaa kupita kiasi, na huo ni uzembe wa kiwango cha juu sana kwa mtu anaepaswa kua makini 🐒

hata hivyo mtoa taarifa ni mtu asie na credibility, kutokana na style yake ya utovu wa kimaadili katika jamii na hivyo kufanya mambo muhimu kama haya kutoka kwake kupuuzwa 🐒
 
Back
Top Bottom