Nimekutana na Degree Graduate wa HR kutoka Mzumbe anauza Pub

bwaiseekwetu

Senior Member
May 29, 2022
145
427
Hakika hali ni mbaya. Katika mizunguko yangu ya kumalizia weekend, nikasema niingie kwenye ki-pub kimoja cha mtaani nipate hata ka-bia kamoja kupoza Koo.

Mhudumu mdada aliyenihudumia ni graduate wa Bachelor degree ya Human Resources Management kutoka Mzumbe University na alimaliza 2019. Anasema tangu a-graduate hajawahi kupata Ajira kokote zaidi ya kusaga soli kutafuta Ajira Nchi nzima kuanzia Januari mpaka December bila mafanikio.

Tufanye nini kama Taifa wana JF? Na kama kuna mwana JF ana msaada wa Ajira tafadhali naomba amsaidie huyu Dada, yupo tayari kufanya kazi mahali popote.

Kwa niaba yake TUTASHUKURU sana kwa atakayesaidia. Kabila lake ni Mmasai, umri miaka 27.
 
Hakika hali ni mbaya. Katika mizunguko yangu ya kumalizia weekend,nikasema niingie kwenye ki-pub kimoja cha mtaani nipate hata ka-bia kamoja kupoza Koo. Mhudumu mdada aliyenihudumia ni graduate wa Bachelor degree ya Human Resources Management kutoka Mzumbe University na alimaliza 2019. Anasema tangu a-graduate hajawahi kupata Ajira kokote zaidi ya kusaga soli kutafuta Ajira Nchi nzima kuanzia Januari mpaka December bila mafanikio.
Tufanye nini kama Taifa wana JF?na kama kuna mwana JF ana msaada wa Ajira tafadhali naomba amsaidie huyu Dada,yupo tayari kufanya kazi mahali popote. Kwa niaba yake TUTASHUKURU sana kwa atakayesaidia. Kabila lake ni Mmasai,umri miaka 27
Hata mzumbe yenyewe wanaoishi eneo lile asilimia 50% graduate ni machinga, mama ntilie na bodaboda inaonekana wewe bado limbukeni.
 
Kilichonihuzunisha ni alipokuja Boss wake mwenye hiko ki-pub ambaye kwa kumuangalia tu ni darasa la Saba na kuanza kumfokea eti kwa nini leo amefungua Pub saa 4 asubuhi badala ya saa 2 asubuhi muda aliompangia.

Muhimu Dada akajitetea kwamba alikuwa anafua. Cha kushangaza Boss anazidi kumfokea kwa nini hukufua jana usiku ulivyofunga Pub?

Dada akamjibu jana nimefunga saa 8 usiku, ningeweza kweli kuanza kufua saa 8 usiku? Kwa kweli nimesikitika sana, ilibaki kidogo ninunue ugomvi ule nimtete Dada yule.
 
Ndo hali ilivyo mkuu. Mwaka 2018 nilikuwa na biashara ya mgahawa ambapo dada mpika vitafunwa alikuwa na Bcom ya UDSM.

Tena hakusema ila nilikuja kujua baadae nikashtuka sana. Kama hujaoa muoe huyo Masai utakuwa umemsaidia 100%. Atakuwa HR wa moyo wako.
 
Hao wapo wengi sana.

Nowdays ukienda saloon wanaosuka nywele wana degree ila hawasemi

Kwa wanaume wasomi wengi wamekimbilia U MC wa harusi
Wachoma Mahindi
Wauza Matunda
Wauza Maziwa
Wachoma Chips
Wauza Vitafunwa
Dada zangu wa Free Delivery Food hapa unaletewa vyakula vya aina mbili utachagua unakula kipi na kipi hauli au unakula vyote kimoja baada ya kingine
Dada zangu wa kusell yourself for your body is your body sexy walker sexy talk hookup hawa ndio wengi inapigwa tu simu moja unaitisha mnakubariana malipo anakuja
Wauza Samaki
Wauza Ice Cream hadi kwa Bakhresa
Viwandani wanagombea malipo 3000 kwa siku
Saidia fundi
Wauza duka la Chakula
Wauza nguo za Mitumba
Wauza Magari
Winga
Matapeli k/koo hapa ni mixture wanawake wanaume au wote wanafanya kua accomplice au accessory after the fact
Wauza mayai
Mobile Money ndio lukuki
Boda boda
Bajaj
Madereva wa Huba na Bolt
Waendesha Malori
Waendesha magari ya Mafuta
Bila kuwasahau Walinzi kwenye makampuni ya ulinzi

Yaan nikiandika list ni ndefu Ila kuna ambao kundi lao ni kubwa sana sana sana na wanatumika sana kwa ujira wa kawaida tu
 
Hakika hali ni mbaya. Katika mizunguko yangu ya kumalizia weekend,nikasema niingie kwenye ki-pub kimoja cha mtaani nipate hata ka-bia kamoja kupoza Koo.

Mhudumu mdada aliyenihudumia ni graduate wa Bachelor degree ya Human Resources Management kutoka Mzumbe University na alimaliza 2019. Anasema tangu a-graduate hajawahi kupata Ajira kokote zaidi ya kusaga soli kutafuta Ajira Nchi nzima kuanzia Januari mpaka December bila mafanikio.

Tufanye nini kama Taifa wana JF? Na kama kuna mwana JF ana msaada wa Ajira tafadhali naomba amsaidie huyu Dada, yupo tayari kufanya kazi mahali popote.

Kwa niaba yake TUTASHUKURU sana kwa atakayesaidia. Kabila lake ni Mmasai,umri miaka 27
Mkuu alisoma Mzumbe campus ipi Kama hutojali
 
Kilichoniuzunisha ni alipokuja Boss wake mwenye hiko ki-pub ambaye kwa kumuangalia tu ni darasa la Saba na kuanza kumfokea eti kwa nini leo amefungua Pub saa 4 asubuhi badala ya saa 2 asubuhi muda aliompangia. Dada akajitetea kwamba alikuwa anafua. Cha kushangaza Boss anazidi kumfokea kwa nini hukufua jana usiku ulivyofunga Pub?Dada akamjibu jana nimefunga saa 8 usiku,ningeweza kweli kuanza kufua saa 8 usiku?kwa kweli nimesikitika sana,ilibaki kidogo ninunue ugomvi ule nimtete Dada yule
Sasa kwa nini hujamtetea?
 
Hii nchi Graduate bado wana nafasi ya kutoboa maisha, lakini hii ni kwa wale graduate ambao ni aggressive, discplined, and with visions.

Ila kwa wale graduate ambao ni form ten na form nine, ambao mda wote wapo cynical. Maisha yatakuwa ni magumu sana kwao. Na ukiongea nao utajua tu
 
Hii nchi Graduate bado wana nafasi ya kutoboa maisha, lakini hii ni kwa wale graduate ambao ni aggressive, discplined, and with visions.

Ila kwa wale graduate ambao ni form ten na form nine. Maisha yatakuwa ni magumu sana kwao. Na ukiongea nao utajua tu
Form 10 form 9 ya wapi UDSM? Acha utani basi Naantombe' Mushi mbon umebadirisha jina?
 
Kilichoniuzunisha ni alipokuja Boss wake mwenye hiko ki-pub ambaye kwa kumuangalia tu ni darasa la Saba na kuanza kumfokea eti kwa nini leo amefungua Pub saa 4 asubuhi badala ya saa 2 asubuhi muda aliompangia. Dada akajitetea kwamba alikuwa anafua. Cha kushangaza Boss anazidi kumfokea kwa nini hukufua jana usiku ulivyofunga Pub?Dada akamjibu jana nimefunga saa 8 usiku,ningeweza kweli kuanza kufua saa 8 usiku?kwa kweli nimesikitika sana,ilibaki kidogo ninunue ugomvi ule nimtete Dada yule
Duh ni maumivu kweli ila aendelee kupambana..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom