Nimekata tamaa ya kuolewa

neema pita

Member
Apr 26, 2012
30
6
Aisee huyu mtu anaitaji ushauri

Nimekata tamaa ya kuolewa kabisa kwani niliedhan kuwa ndo mume wangu kanigeuka vibaya sana.

Umri wangu miaka 28 nimejitunza siku zote nikiamini na kumuomba mungu anipe mme mwema nimekua katika maadili ya kidini nimepoteza wachumba wengi baada ya kutofautiana yote ni baada ya kukataa kufanya mapenz kabla ya ndoa.

Mwaka jana nikapata mchumba tukatambulishana kwa wazazi alinionesha mapenz kiukwel mpaka nikashawishika kufanya mapenz kabla ya ndoa ( najutia sana) ikapelekea kupata ujauzito gafla mwenzangu ananiambia anamchumba doct mwenzie.
Kweli nimekata tamaa ya kuolewa kabisa
1. Umri unaenda tayar ninakikwazo mtoto wanaume wengi kuoa mwanamke mwenye mtoto ni kubahitisha. ukizingatia na umri mbaya... cjui inawezekana mungu hakunipangia kuolewa.

Ni baada ya kupotezana kwa muda mrefu na rafiki yangu leo tumekutana ndo ananipa story jinsi alivyo katamaa ya kuoelewa.
 
Natasha kaolewa na miaka 50+ alikuwa na mtoto na wajukuu 2 asikate tamaa mapema na asione huyo mtoto kama kikwazo as long as alikubali kuibeba mimba yake na kuzaa kwa uchungu hiyo ni baraka
 
Wengine wakiolewa wanaota mapembe kazi zote unaachia HG...hata kumpa mume chakula hutaki...msipoolewa mnaanza mayowe....
 
Nahitaji kuoa mwanamke kama wewe ila tu ikiwa utaingia mzima mzima kwenye ndoa isiwe unaendelea na mahusiano mengine hasa na aliyekuzalisha maana haya mambo ya kijinga yapo. Mtoto nitamlea na kumsomesha sio shida. Ila tu ikiwa utaingia mzima mzima.

NB: niliwahi kuwa na mke tukate gana na sina mtoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom