Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Elnino,

Habari za shughuli.

Ningependa kujua hali ya mahindi yako. Yanaendeleaje? Unategemea kuvuna lini?
 
Kaka elnino nashukuru kwa thread yako lakini tahadhari. Mimi nimelima mwaka huu mvua zimekataa nilikuwa na malengo kama yako lakini kilimo kwanza kimeniponza.nimepeleka mshahara wangu wa miezi minne shambani imekula kwangu.lakini kwa moro nafikiri hali ya hewa ni tofauti na kwetu,wape tahadhari wanaotaka kulima wawe makini wasije kichwakichwa

1. Watafute eneozuri la kulima
2. Wawe na mtaji wa kutosha
3. Wawe tayari kuingia shambani kusimamia [kilimo si mchezo]
4. Wawe tayari kwa matokeo yoyote kukosa au kupata, wakishakubali tuwakaribishe
 
Kaka elnino nashukuru kwa thread yako lakini tahadhari. Mimi nimelima mwaka huu mvua zimekataa nilikuwa na malengo kama yako lakini kilimo kwanza kimeniponza.nimepeleka mshahara wangu wa miezi minne shambani imekula kwangu.lakini kwa moro nafikiri hali ya hewa ni tofauti na kwetu,wape tahadhari wanaotaka kulima wawe makini wasije kichwakichwa

1. Watafute eneozuri la kulima
2. Wawe na mtaji wa kutosha
3. Wawe tayari kuingia shambani kusimamia [kilimo si mchezo]
4. Wawe tayari kwa matokeo yoyote[kukosa au kupata] wakishakubali tuwakaribishe

Pole nafikiri utakuwa maendeo ya bara, yes kwa bara mzee huwa ni bahati nasibu, jaribu maeneo ya ukanda huu wetu ukizingatia huku kuna misimu miwili kwa mwaka basi huwezi kosa kabisa.

Ni kweli yote haya umenena, na ndiyo maana watu hawapendi kuingiza pesa zao kwa kitu ambacho ni bahati nasibu, unajua kuwekeza kwenye kilimo kunahitaji moyo wa ajabu (ujasiri) let say unaingiza 20m then unatengemea mvua za mungu hiyo ni risk kubwa sana lakini sasa ufanyaje na huna mtaji wa kilimo cha umwagiliaji?

Mi nashauri watu wasiogope wa-play card zao waingize pesa lakini wakumbuke kucheki hizo points 4 alizozitoa mdau hapo juu. Mimi naamini hata hao wakulima wakubwa duniani kuna siku walianza kwa kutumia mvua za mungu na vimtaji vidogo vidogo kama vyetu. So let us move on, mzee usikate tamaa jipange tena mwakani.

Kwa sisi Moro mvua ni safi so far, tunategemea kama itanyesha tena end of May or mwanzoni mwa June basi its done.
 
JF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF- hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
Thank you ELININO, but remember life doesn't keep other things constant. If GOD wish you will leave in your dreamz may GOD help you in this plan.
 
Thank you ELININO, but remember life doesn't keep other things constant. If GOD wish you will leave in your dreamz may GOD help you in this plan.


Firstcollina, thanks for your comment & wishes, I'm still on this project really. My first season outputs will be accessed by end of August.

I have also started to set strategic plan for a new season 2011 – thinking to expand this project three to four times of the current capacity.
 
hi elnino,
ukivuna tupe picha on line,
ukivuna mengi let me know ninandugu ana saga na kupack unga,unatarajia kuvuna tani ngapi?
 
jamani infact na mimi naguswa sana na hili wazo zima la kilimo kwanza......ndugu yangu wa moro naomba unisaidie shamba la kukodi na mimi ekari za kutosha na mimi nijisogeze.....maana ndugu hali mbaya........can be reached through 0717107505
 
Heshima kwako El,

Mkuu vipi mahindi yanaendeleaje ?.Mimi nilikuwa Kabuku wiki iliyopita mahindi yameshaanza kukauka naanza kujiandaa na ununuzi wa magunia na dawa za kuzuia wadudu.

Hali ya soko la mahindi ni mbaya sana gunia moja la mahindi [debe sita] ni Tshs. 21,000/=,hali itazidi kuwa mbaya kipindi wakulima watakapoanza kuvuna kuanzia mwezi wa tisa na kuendela. Ujanja hapa ni kuhifadhi mpaka hali ya soko itakapokuwa nzuri.

Sijui soko la EAC kama litaweza kutusaidia kupata bei nzuri.
 
Acha maneno ya kukatisha tamaa, siamini kama EL NINO anaweza kukimbia kwa sababu naamini ni mtu makini,. atakuwa busy Tuliani kushughulikia shamba.

Kuhusu kushuka bei kwa Mahindi, naweza kukubaliana na Ngongo kwamba ni vema kuyahifadhi hadi soko litakapokuwa zuri. ila katika ili inabidi uwe na ghala zuri na upambane vema na wadudu wahalibifu.

Thanks Guys!!!
 
The poor are too risk aversive to be rich. To emancipate the poor you need to make them take more risk. Hongera brother
 
Heshima kwako El,

Mkuu vipi mahindi yanaendeleaje ?.Mimi nilikuwa Kabuku wiki iliyopita mahindi yameshaanza kukauka naanza kujiandaa na ununuzi wa magunia na dawa za kuzuia wadudu.Hali ya soko la mahindi ni mbaya sana gunia moja la mahindi [debe sita] ni Tshs. 21,000/=,hali itazidi kuwa mbaya kipindi wakulima watakapoanza kuvuna kuanzia mwezi wa tisa na kuendela.Ujanja hapa ni kuhifadhi mpaka hali ya soko itakapokuwa nzuri.

Sijui soko la EAC kama litaweza kutusaidia kupata bei nzuri.

Mkuu biashara ya kulima haitaki haraka, mara nyingi ni biashara ya mara moja kwa mwaka, unawekeza december unakuja kuuzza december au feb ndyo utapata faida.
 
Back
Top Bottom