Nimeacha mazoezi baada ya kukutana na mwanamke wa ajabu

Wakuu,

Nimekuwa na tabia ya kufanya mazoezi Alfajir ya saa 10 mpaka 12.

Majuma matatu yaliyopita kama siku nne mfululizo kuna binti huwa nakutana nae lile
eneo ambalo namalizia kunyoosha viungo.

Huwa anakaa kwenye kigogo kimoja ambacho kipo kando ya mti mkubwa ambao
uko eneo hilo.

Siku ya kwanza nilichukulia kawaida tu kuwa ni mtu ambaye labda ana kijishamba eneo hilo maana ni nje kidogo ya mji. Sikumsalimia nae hakunisalimia.

Siku ya pili nilifika hapo majira ya saa 11 na dakika zake, wasiwasi wa kwanza ni namna
alivyovaa vizuri gauni jeupe lenye mng'aro fulani hivi huku akinukia vizuri.

Nikamsalimia akaitikia huku akitabasamu, nikamuuliza kuwa amekuja shambani? Akanijibu kuwa hapo ni nyumbani kwake. Nikacheka kwa kujua ni utani.

Siku ya tatu ni yeye ndio kawahi kunisalimia akanisifia jinsi nilivyo na bidii ya mazoezi
akasema anapenda sana wanaume wenye bidii kama mimi. Hapo kidogo hofu ikazidi.

Siku ya nne niliamua kwenda mapema zaidi ili nisimkute, niliamua kuwahi pale saa kumi
Alfajiri, nikamkuta palepale nikashtuka sana nikamuuliza amefika saa ngapi?

Akanambia, kwani si nilishakueleza hapa ndio nyumbani? Mimi naishi kwenye huu mti siku zote unazokuja hapa huwa nakuona toka mwaka jana(sasa ni mwaka juzi) we si uliwahi kuteleza na kuanguka hapo, akanionesha sehemu ambayo kweli niliwahi kuanguka.

Wakuu nimekosa amani ingawa huyu binti ameonesha urafiki lakini nimeshindwa kurudi tena mazoezini.

Hata nikikaa ndani bado nakuwa na wasiwasi.

Naombeni ushauri wenu niendelee
tu au kuna vimaombi vinatakiwa kufanyika?
Mwanangu fursa hiyo!
 
Huyo ni jini mkuu,ila sidhani kama kuna shida as long as hujaingia kwenye collaboration yeyote naye.Ila kama wewe ni a "true Christian," yaani a "truly born again" Christian,omba ulinzi wa Bwana Yesu just in case,nothing will happen to you.Bwana Yesu ndiye kiboko cha hayo madudu mkuu.
 
ATM hiyo nenda kachote hela za jini, sharti lake ni dogo tu usimsaliti kimapenzi
 
Back
Top Bottom