Niliyoyashuhudia Leo usiku chuo cha CBE ni HATARI

py thon

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
2,471
4,424
Leo mida ya saa mbili usiku nilikuwa natembea hii njia ya CBE lakini niliyoyaona nilistaajabu,ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.

Nimekuta masista du wa chuo cha CBE wakipanga foleni huku wakigombania mihogo saa mbili usiku.

Kwa jinsi walivyo utaona ni matawi ase kweli mwaka huu tunabana matumizi ase

Hadi masista du tunagombania nao mihogo siku hizi ,

Wakati tuliwazoea wakinywa juice wanaacha nusu kwenye glass wakila zege wanabakisha vichips robo kwenye sahani..

Lkn nawashauri mwanafunzi hapaswi kula vyakula vya wanga migumu kama mihogo mida ya usiku ,mwanafunzi yuwapaswa kula vyakula vyepesi usiku ili akiamka asubuhi akili iwe sharp ,kuwe na kiwango cha kuingiza wanga mwilini .
 
Acha dharau, mihogo mitamu sana usifananishe na vyakula vingine asee!. Hata nikivaa suti nyeupe nikiona mihogo lazima nichangamkie fursa ya tumbo langu hiyo.....wengi twaipenda si kwamba ni dalili za hali duni la ha shaa!!!!. Mihogo shikamoooo!!!
 
Wanafunzi cha muhimu kwao ni mkono kwenda kinywani basi,ili hali hawana kipato hiyo jeuri ya kuchagua chakula waitoe wapi!?ni kusweka tu ndugu.
 
Kuna wakati utafika elimu yako, wadhifa wako au umaridadi wako utakuwa hauna msaada kwako,. Na wakati wenyewe ndio huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom