Niliuzika sana basi tuu!!

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,726
19,870
Habari wapendwa wanajf: Juzi nilikuwa msibani fulan wa ndugu yangu si mnajua msibani na kuna kulala nje sasa mnamo mida ya saa 8 usiku si akaja mtu akatumwagia maji pale jamvini aisee nilikasirishwa hadi nikataka nizichape nae watu wakanishika wakaniambie eti ni MTANI wangu.
Badae wakazuia jeneza lisitoke wanataka hela.JAMANI NAOMBENI KUULIZA JE ili utani uwepo kati ya kabila moja na wengine wanaangalia nini maana utasikia mnyamwezi mtan wake mzalamo na hii kitu ina umuhimu gani? NIJUZENI MAANA MI NIMELOWEA HUKU BONGO HATA SIELEWI HIZI MAMBO.
 
ilikuwa njia ya kupunguza ukabila na uadui hasa kwa makabila yalopigana tanzania
nadhani idea ya mwalimu
japo siku hizi hauna mantiki tena
imebaki kusumbuana misibani na harusini
 
hahahaaaaa
pole Billie
hawakujua wewe ni sharobaro men! umezaliwa enzi za dot.com men!!!
haya ni mambo ya zamani na muda si mrefu yatapotea na kusahaulika
 
ni mwingine too much
mtu anaugua hana hela.kafa eti mnazuia jeneza mlipwe
 
Hahahah! pole sana,hapo inabidi kuwa mpole na kusubiri nawewe siku ya siku unamfuma basi hadi wakujue. Lakini ni mambo ambayo tunahitaji kuwa nayo kama tamaduni zetu!! Yanatuweka karibu, kutuunganisha na mambo kadha wa kadha! cha msingi ni kuyafanyia marekebisho ili yaendane na wakati ila siyo kuyapotezea kabisa.
 
Kwanza umenidhi. Angalia umandika nini. NILIUZIKA SANA. Hicho sio kiswahili fasaha. Naomba urekebishe lugha kwanza nami nitapata nafasi ya kuchangia
 
ilikuwa njia ya kupunguza ukabila na uadui hasa kwa makabila yalopigana tanzania
nadhani idea ya mwalimu
japo siku hizi hauna mantiki tena
imebaki kusumbuana misibani na harusini
Ni kweli kua ni njia ya kupunguza uadui na ukabila ila sio idea ya Mwalimu. Ni culture ya Kibantu zaidi na ipo kwenye nchi nyingi, hasa zenye kabila zaidi ya 2 za kibantu.
 
Yani mambo ya kulala misibani nayo ndo matatizo wengine wanalia na wengine wanafanya joke...sijui kulia sana na kufanya joke ndo maendeleo.
 
Kuna kipindi utani unakera sana lakini huna budi kuuzoea maana tafsiri sahihi ya utani ni kuambiana ukweli pasipo chuki, una faida na hasara zake.
Hasara yake kuu. usipotimika vizuri huondoka au kuweza kuondoa mahusiano yaliyokuwepo awali.
 
Kwanza umenidhi. Angalia umandika nini. NILIUZIKA SANA. Hicho sio kiswahili fasaha. Naomba urekebishe lugha kwanza nami nitapata nafasi ya kuchangia

Unapomrekebisha mwenzako angalia na wewe usifanye makosa yaleyale sasa hapo penye "RED" unamaanisha nini?

Mukiukataa utani kila siku watu tutabaki tumenuniana hata misibani. Utani mwingine kwa kweli hua ni mzuri:
Kwa mfano watu wanazuia mwili wa marehemu usitolewe mahali ulipo mpaka watani walipwe fedha na wakishalipwa say sh. 100 wao wanawajibika katika shughuli nyingi za pale msibani kama kupika, kununua vyakula n.k kwa namna hiyo utani unaweza kuleta faraja kwa wafiwa kwa kiasi fulani.
Ni wazo tu.
 
Bora umemkamata wewe.Mi ningeonekana kama natafuta ligi.
Tehe tehe tehe
 
Habari wapendwa wanajf: Juzi nilikuwa msibani fulan wa ndugu yangu si mnajua msibani na kuna kulala nje sasa mnamo mida ya saa 8 usiku si akaja mtu akatumwagia maji pale jamvini aisee nilikasirishwa hadi nikataka nizichape nae watu wakanishika wakaniambie eti ni MTANI wangu.
Badae wakazuia jeneza lisitoke wanataka hela.JAMANI NAOMBENI KUULIZA JE ili utani uwepo kati ya kabila moja na wengine wanaangalia nini maana utasikia mnyamwezi mtan wake mzalamo na hii kitu ina umuhimu gani? NIJUZENI MAANA MI NIMELOWEA HUKU BONGO HATA SIELEWI HIZI MAMBO.
Mnyamwezi mtani wake ni msambaa,,, mm kipindi cha msiba wa mama yangu watani walizuia masufuria ya chakula ikabidi nitoe fedha kiasi flani ili wayaachie..hebu imagine uko kwenye machungu ya kufiwa na mzazi wako bado mtu analeta utani!!! shit!
 
rushanju ni kawaida hayo mambo sipo darasani just typing error Namekubali kosa langu.
Kwanza umenidhi. Angalia umandika nini. NILIUZIKA SANA. Hicho sio kiswahili fasaha. Naomba urekebishe lugha kwanza nami nitapata nafasi ya kuchangia
 
Mchaka mchaka kwani huwa ni pair tu inawezekana kabila moja kuwa na watani zaidi ya mmoja.
Mnyamwezi mtani wake ni msambaa,,, mm kipindi cha msiba wa mama yangu watani walizuia masufuria ya chakula ikabidi nitoe fedha kiasi flani ili wayaachie..hebu imagine uko kwenye machungu ya kufiwa na mzazi wako bado mtu analeta utani!!! shit!
 
mama D naona umefurahi mim kumwagiwa maji ngoja na wewe yakukute hawa watani wangeweka form maalum ya kusaign mtu anayetaka utani ndo awajibike nao maskini iliniuma vibaya kwa kuwa sikuwa na nguo ya kubadilisha.
hahahaaaaa
pole Billie
hawakujua wewe ni sharobaro men! umezaliwa enzi za dot.com men!!!
haya ni mambo ya zamani na muda si mrefu yatapotea na kusahaulika
 
mama D naona umefurahi mim kumwagiwa maji ngoja na wewe yakukute hawa watani wangeweka form maalum ya kusaign mtu anayetaka utani ndo awajibike nao maskini iliniuma vibaya kwa kuwa sikuwa na nguo ya kubadilisha.

Maskinii.....polee!
 
Back
Top Bottom