Nilishindwa kuendelea kuwa nae sababu ya vitu alivyonavyo kichwani

Wakuchanja

Member
Oct 12, 2017
82
54
Habarini wanajamvi,

Miaka minne iliopita nilipata mpenzi ambaye tulipendana sana nakuaminiana pia, mapenzi yaliendelea vizuri na yalinoga kadri siku zinavyo jongea, yule mdada alikuwa anakaa kwao na mimi nimepanga naishi mwenyewe kiukweli nilishindwa gundua baadhi ya mambo kwakua hatukuishi pamoja,

Ikafika kipindi yule mdada akawa anashindwa ishi mbali na mimi hatimae alihama kwao na kuhamia kwangu. Mwanzoni tuliishi vizuri tu lakin kuna vitu nikawa sivielewi nakuvichukulia kawaida tu,kama akiwa nimetoka na mm huku nyuma nikitoka bila kumpa taarifa anajua na anapiga simu kuniambia kuwa nimetoka,hata nikichepuka pia huwa anajua tu bila hata kuambiwa,hyo hali ilifika kipindi ikanishinda sababu ilikuwa inampa kiburi na kunitaka nifate mambo anayoyataka yeye.

Nilichukua maamuzi yakuachana mwaka sasa hatupo pamoja lakin yeye hachoki kunitafuta naombeni ushauri hapo
 
Hebu uwe unafuta text zote za siri tuone kama atajua tena.... ni kawaida mwanamke akikupenda atajitahd awe anakupekua kila mahali sasa mda unapofanya yako yeye alishajua
 
Huyo ana majini,atakusumbua sana usiposimama katika imani,
Achana naye kabisa mbeleni utalia huwa wana kiburi na roho za hasira kiufupi ni pasua kichwa
 
Hii kama nilishasomaga kwenye moja ya magazeti ya shigongo kama nakumbuka ilikuwa hadithi hii
 
Hapana kuna watu wanaoneshwa vitu ndotoni, mfano mm Mara nyingi nikiota kitu kinachonihusu nakiona, hata mpz wangu akicheat sometimes kama vile nagundua, yaan kuna vitu navifatilia nahisi vina ukweli, sijui ni kwa kuwa nasali sana?

Nawazaaaa kuna siku kabisa moyo unaniambia nimecheatiwa, naomba weee kama wiki nisipoota kitu ninachohisi basi napotezea.

Na nikiota kitu naandika kwenye note book nitakiuliza muda mwafaka.

Kwa wale wanaosali wananielewa . orodhesha vitu unavyotaka majibu yake, sali hata mwezi, ukiota ndoto inayofanana, andika sehemu, kuna siku utapata majibu.
 
Back
Top Bottom