Anfaal
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 1,154
- 113
Nchi yetu, vituko haviishi. Kila sehem kuna mambo yake. Na watu wake huamini kuwa ni mambo ya kawaida na ndio nchi inatakiwa iende hivyo. Licha ya kwamba mengi katika yanayotokea tuhuma huelekezwa kwa serikali lakini sisi wananchi tunanafasi kubwa ya ukombozi wa nchi yetu.
Pale uwanjani wakati wa kucheck in, wakaniambia mzigo wangu umezidi kama kilo 8. Nilishtuka kwa sababu huwa ninakawaida ya kucheck uzito wa mzigo kabla ya kusafari. Mara hii nikapatwa na hofu maana ni jambo ambalo huwa sipendi kamwe linitokee. Wale wahudumu wa pale, (hasa dada mmoja mjamzito), akawa wa kwanza kunirukia kila kilo dollar 30 kwahiyo inabidi ulipe dollar 240. Akaitwa mtu kwa haraka wewe toa beki lake weka pale. Aliyetoa begi akaniambia wewe ongea nao uwape chochote. Bahati mbaya hili la chochote huwa si katika mfumo wangu wa maisha niliojiwekea. Nikaanza kutoa baadhi ya vitu lengo hasa likiwa vibaki. Wale wahudumu pale wakaendelea kuninasihi niongee na wale watu pale watakubali. Wakati ninafanya hayo, akapita mzungu mwingine naye nikaangalia mzani wake ukawa umezidi wakamuacha aende. Sikujali lile kwa kuwa sikuwa muhusika wa ule mzigo, mara ghafla dada yule akarudi alivyoona kuwa kweli natoa mizigo akasema nakupa allowance ya 5kg, nikabaki ninaduwaa, kumbe anauwezo huu. Nikapack tena vitu vyangu, kupima mzigo haujazidi. Sikuelewa hasa tatizo lipo wapi. Lakini pia kauli za pale zilikuwa ni zenye kukera mno na zimejaa dharau ya hali ya juu. Kuna haja ya sisi Watanzania kujifunza kufanya kazi. Ubabaishaji hautatufaa kamwe. Naamini hii inaweza kuwasaidia watoa huduma wengine lakini pia nitawaandikia na wenye ndege maana wanahangaika na competition lakini kuna watu wanawaangusha.