Nilikuwa na wake wengi kabla sijaokoka, sasa nimeokoka. Je, niwaache?

Akidu

Member
Sep 19, 2022
47
76
Nilikuwa na Wake Wengi Kabla Sijaokoka . Sasa Nimeokoka , Je! Niwaache?

Je Mkristo Kuwa na Wake Wengi Ni Dhambi
?

Mwl. Akidu
0628366559

Suala la binadamu kuishi mfumo wa maisha ya kuwa na wake wengi limekuwepo tangu nyakati za mwanzoni mwa ulimwengu.

Miongoni mwa wanadamu wa kwanza kuoa wake wengi alikuwa ni Lameki anayetokea ktk uzao wa Kaini mwana wa Adamu.

Ukiangalia vizuri hapo juu, sijasema Lameki ndiyo alikuwa wa kwanza bali nimesema alikuwa miongoni mwa wanadamu wa kwanza.

Hii ni kwa sababu Biblia imekuwa na utaratibu wa kuelezea historia ya baadhi tu ya watu ktk kizazi chao . Na siyo watu wote.

Mfumo huu wa maisha uliendelea kuwepo enzi na enzi , nyakati na nyakati kabla ya kuzaliwa kwa Yesu , wakati Yesu akiwepo duniani , baada ya Yesu kuondoka duniani na hata leo hii mfumo huu bado upo.

Manabii wa Mungu wakubwa wa imani, makuhani wa dini, Watakatifu wacha Mungu, wafalme na watu wa kawaida wote walitambua kuwa mfumo wa wake wengi ulikuwa mfumo wa maisha wa kawaida tu ambao ni hiari ya mtu mwenyewe. Hulazimishwi kufanya Wala huzuiwi.

Kabla sijaendelea mbele, huwa najiuliza swali moja:
Ikiwa mfalme Suleiman alikuwa na wake 1000, na bado wanaume wengine wakawa na wake zao tena zaidi ya mmoja (yaani Hakuna aliyekosa mwanamke), je Kama Suleiman angeoa mke mmoja , wale 999 wangeolewa na nani hapa duniani?

Hii ni hesabu ya kawaida tu ya kibinaadamu

Ukweli ni kuwa ktk dunia Kuna mambo Mungu aliyafanya yawe yanajiendesha yenyewe tu kwa kutumia nature (asili) yake ikiwemo suala la wake wengi ili iwepo balance ya mzani kulingana na idadi ya watu. Ili asiwepo mtu atakayelalamika kuwa amekosa kuolewa kwa sababu wanaume ni wachache kuliko wanawake.

Japo ilikuwa ni mpango wa Mungu kwa asili kbs kila mwanaume awe na mwanamke na kila mwanamke awe na mwanamume lkn hiyo hiyo nature /asili pia inatambua kuwa si kila mwanamke anaweza kuwa mke na si kila mwanaume anaweza kuwa mume . Ndiyo maana wapo wengine hubaki kuwa makahaba tu . Hata ufanye nini huwezi kumuweka ndani akatulia.

Ikiwa ilikuwa ni mpango wa Mungu kila mwanamke awe na mwanamume, vipi ikitokea wanawake wakawa wengi zaidi ya wanaume?

Hicho ndicho kilichotokea mpk mfumo wa wake wengi ukaanza.

Sababu nyingine iliyosababisha mfumo wa wake wengi uwepo duniani ni asili ya mwanaume. Mwanaume kwa asili ameumbwa na tamaa ya kufurahishwa kwa tendo la ndoa. Na kwa asili hiyo ya tamaa. Hali hiyo ikimzidia yeye akashindwa kuizidi , ndipo hupenda kuwa na wanawake wengi.

Sasa ili isiwe dhambi ndipo ukawepo utaratibu wa kihalali wa kuoa wake wengi. Mwanaume anapenda kwa kuona (kutamani kwa macho). Mwanamke anapenda kwa kusikia (amesikia mara ngapi sauti ile ile ikijirudia ktk hisia zake).

Sababu ya tatu iliyo wazi ya mfumo wa wake wengi ilikuwa ni kuijaza dunia. Mungu aliwaagiza wanadamu wazaane waijaze dunia. Kwa mantiki hiyo ilikuwa ni lazima wazalishaji viumbe (wanawake) wawe wengi zaidi kuumbwa kiidadi ili dunia iwahi kujaa.

Ndiyo maana hutaona mahali ktk Biblia Mungu amewalalamikia wanadamu kwanini wameoa wake wengi. Au kwann wamezaa watoto wengi Sana.

Twende Sasa ktk tafakari ya uchambuzi wa kutumia akili zaidi

Ukisoma vitabu vya Injili vinavyozungumzia maisha na mambo yote aliyofanya Yesu , Hakuna mahali palipoandikwa Yesu alizungumzia lolote juu ya ndoa za wake wengi.

Yesu alijibu hoja moja ya mwanamke aliyewahi kuolewa na wanaume wengi lkn siyo hoja ya mwanaume aliyewahi kuwa na wake wengi.

Dhana ya mfumo wa mke mmoja tunakuja kuipata ktk Vitabu vya mtume Paulo akiwasisitizia viongozi wa dini. Kama nitakavyofafanua mwishoni.

Ikumbukwe yapo pia mambo mengi mtume Paulo alikuwa anayatoa Kama mawazo yake ya ushauri wa busara na hekima ya maisha ya wakristo. Ili kuepusha magomvi, migogoro , migongano ,taharuki , sintofahamu n.k ktk kanisa.

Na alikuwa anasema wazi kbs kuwa hapa siyo Mungu bali Nasema Mimi Kama mtume wa Mungu (Yaani nashauri kwa hekima zangu nilizopewa na Mungu).

Hili Jambo la ndoa za wake wengi ni miongoni mwa mambo yenye contradiction Sana . Ndiyo maana hadi leo lipo dhehebu la kikristo lililo na msimamo wa kuoa wake wengi (The last church). Huku Bariadi tunawaita " watola mali".

Kuna mwanatheolojia mmoja aliwahi kuniambia, Ukiona Jambo linaleta contradiction Sana Basi rudi kwny lugha ya asili ya mwanzo kbs iliyotumika kuandika biblia. Ukweli ni kuwa Kuna baadhi ya mambo tafsiri yake haiendi moja kwa moja km ilivyo kule kwny lugha ya mwanzo (kiebrania, kiyunani) na baadae kilatini ,kingereza, kiswahili.

Chukulia mfano andiko linalosema " mtu asimwache mke wake isipokuwa kwa sbb ya uasherati/ uzinzi"..
Hii ilikuwa ni kauli ya Yesu.

Ktk tafsiri ya kawaida tu ya lugha unapata uelewa kuwa, kumbe mke akifanya uzinzi unaruhusiwa kumuacha ..

Lkn pamoja na andiko hili, Ukristo haukubaliani na talaka.

Nilipofatilia kwa kina kwanini iwe hivyo, nikaambiwa kuwa ktk lugha ya mwanzo iliyotumika kuandika biblia ,mstari huo haukutafsirika hivyo. Bali walimaanisha " Ikiwa ulioa mtu ambaye ni Ndugu yako basi unaweza kumuacha " .

Mpk hapo ni contradiction . Tufuate lugha ya asili ya mwanzo au tufuate lugha iliyotumika kututafsiria?

Ukitaka kusimamia tafsiri ya lugha Basi hutaona sehemu ktk Biblia imeandika direct kbs inayomtaka muumini wa kawaida wa kikristo kuwa na mke mmoja.

Biblia imeandika direct kuwataka viongozi wa dini (askofu,mzee wa kanisa n.k) kuwa mme wa mke mmoja... Na msimamo huu ulikuwa ni wa mtume Paulo.

Sasa je, waumini Wote Ni maaskofu au ni wazee wa kanisa?

Si wapo Wengine ni waumini wa kawaida tu wala hawana mpango wa kuja kuwa maaskofu,wachungaji wala wainjilisti!

Suala la wake wengi ktk Biblia halina tofauti na suala la mvinyo. Ukisema mvinyo hauruhusiwi Biblia itakupinga . Na ukisema ulevi unaruhusiwa Biblia hiyo hiyo itakupinga.

Ndiyo maana mm nampenda mtume Paulo, kwa sbb Kuna mambo alikuwa anatuandikia anasema kbs " hapa siyo Mungu ila huu ni ushauri wangu mm km mtume wa Mungu . Kwahiyo Ni mambo ya hekima na busara tu kwaajili ya kutusaidia kuishi vizuri . Lkn pia siyo lazima ni option.

Ndiyo maana leo wanawake wanasimama mbele ya kanisa . Lkn ukimsoma mtume Paulo anasema hawapaswi kuwa viongozi, hawapaswi kusimama mbele ya kanisa Wala kusema neno lolote. Wawe watulivu na wasipoelewa waende wakawaulize waume zao nyumbani baada ya ibada.

Je, hili linawezekana kwa Sasa? Kama haliwezekani na lipo kwny agano la kale na agano jipya tunaanzaje kuwahukumu wenye wake wengi ambao walikuwepo tangu agano la kale ..

Kuna mambo kwny Biblia ni hekima na busara za kuishi vizuri tu Kama wakristo. Hulazimishwi kufanya Wala huzuiwi. Na kwa mtazamo huo, wazee wetu watangulizi ktk Imani waliamua kufuata hekima na busara ya mke mmoja kama mfumo mzuri wa maisha wa mkristo.

Mtume Paulo anasema ingekuwa vyema tusioe Wala kuolewa tukae km yy (kapera) maana waliooana hawana muda wa kutosha kumpendeza Mungu, wanapendezana wenyewe . Lkn akasema ambaye hawezi kujizuia tamaa aoe.

Inawezekana wakatoliki waliona ni busara kufuata mtazamo wa Paulo wa kutokuoa/ kuolewa kwa masister na mapadre.

Lkn Wapentekoste na Waprotestanti na waadventisti wakaona ni vyema kufuata mtazamo wa Paulo wa kuoa mke mmoja kwa wachungaji na viongozi wote wa dini.

Ni option tu. Paulo aliyesema wanaomtumikia Mungu wasioe ndiye aliyesema waoe Kama hawawezi kujizuia.

Na ndiye aliyesema viongozi wa dini (askofu , wazee wa kanisa n.k) wawe mme wa mke mmoja km hawawezi kujizuia.

Je, wewe hapo ulipo ni kiongozi wa dini?

Unadhani Kulikuwa na maana gani mtume Paulo kuwaambia viongozi wa dini wawe ni waume wa mke mmoja Ikiwa wakristo wanaume wote tunatakiwa kuwa na ndoa ya mke mmoja? Kwani wao wanatokea kwenye kundi ambalo siyo la wakristo?

Option.

Ni makubaliano tu yasiyomchukiza Mungu. Na kwa mtazamo huo, watangulizi wetu ktk imani mwanzo wa kanisa (baada ya wakina mtume Paulo kuondoka duniani) wakaupanua mtazamo huo wa mke mmoja mpk kwa waumini wa kawaida.

Ni makubaliano tu ya namna ya kuishi vizuri km jumuiya ya kikristo ilimradi msimchukize Mungu.

Leo hii padre akioa au akiwa na watoto/mwanamke kwa Siri anaonekana katenda dhambi. Lkn ni wapi ktk Biblia panamlazimisha mtumishi wa Mungu asioe ? Zaidi ya huo ushauri wa Paulo ambao nao ulikuwa ni option!

Ni makubaliano tu

Hata Yesu mwenyewe alitoa option kwa watumishi wa Mungu "anayetaka kuoa aoe anayetaka kuwa towashi awe towashi (Mathayo 19: 11-12).

Chukulia tu hata mfano wa mvinyo; Wakatoliki wanakunywa pombe, maana Biblia inaruhusu kunywa mvinyo lkn inakataza ulevi. Tafakari kwa kina hapo.

Katika point hiyo hiyo madhehebu mengine yanazuia kbs kunywa pombe kwa sbb Biblia imekataza ulevi licha ya kuwa imeruhusu kunywa mvinyo.

Tunarudi pale pale. Option.

Au fikiria kwa mfano Wasabato wamezuiwa kula nguruwe kwa sababu Biblia agano la kale imekataza ulaji wa nguruwe.

Lkn madhehebu mengine yanakula nguruwe kwa sbb Biblia ktk agano jipya imeruhusu watu wale kitu chochote kilichowekwa mezani ikiwa dhamiri yako haikusuti / haikuhukumu kwa kufanya hivyo (Wakorintho 10: 23-31=> kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila kuuliza uliza kwaajili ya dhamiri; maana dunia ni Mali ya Bwana na vyote viijazavyo)

Mtume Paulo anasema kama umeokoka na wokovu umekukuta ukiwa unaishi na mwenza ambaye hajaokoka / asiyeamini Basi endelea naye huruhusiwi kumuacha labda mpk akuache yeye mwenyewe.

Tena andiko hilo Paulo anasema "haya nayasema mm siyo Mungu"

Sasa fikiria umeokoka na wakati unaokoka ukajikuta tayari upo kwny ndoa ya wake wengi na Paulo amesema huruhusiwi kumuacha mwenza wako asiyeamini / ambaye hajaokoka Bali atatakaswa kupitia wewe...
Kwahiyo unakuwa umeokoka lkn upo Kwenye ndoa ya wake wengi.

Tafakari Sana hayo maneno ya andiko la Paulo na ujiulize.

Je, huyu aliyeokoka akiwa na ndoa ya wake wengi na hatakiwi kumuacha/ kuwaacha wenza wake anafanya dhambi?

Ikiwa Paulo ametoa mtazamo huo ,

Je, kuwa na wake wengi ni dhambi?

Mambo mengine ktk Biblia ni Busara na hekima tu za kuishi vizuri kama mkristo.. Makubaliano tu mliyojiwekea

Pendelea kusoma Biblia mwenyewe utaelewa mambo mengi ambayo mengine haufundishwi kanisani .

Yule ana imani ya wake wengi km nabii Ibrahimu, anaabudu mara 5 kwa siku km nabii Daniel , anatoa sadaka kwa maskini na wahitaji km Kornelio .

Wewe una imani ya mke mmoja ya mtume Paulo kwa viongozi wa dini, au una imani ya mtume Paulo ya kutokuoa kbs, unaabudu mara 1 kwa wiki, hutoi sadaka kwa maskini.

Japo wanadamu wote tuna Mapungufu, unadhani kati ya huyo wa kwanza na huyo wa pili ni nani atakayeugusa moyo wa Mungu?

Mwl akidu
 
Weka mstari unaodai paulo alisema wachungaji tu ndjo mke mmoja. Nijuavyo mimi alieleza tusioe isipokuwa kama umezidiwa basi uoe mke mmoja ila haku specify yupi aoe mmona au yupi afate nyayo za mfalme suleimani
 
Acha baki na mmoja ila usiwafukuze wala kulala nao.wape talaka watunze hadi wapate wa kuwaoa au wape mtaji wakajitegemee
 
False teacher
Acha kuliremba remba neno la Mungu liendane na tamaa zako

Marko 10:4-9
4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
 
Ongeza wengine wengi utapata matokeo bora😄
 
Mke wa kwanza ndio mke halali....
Wengine endelea kuwatunza watoto wao...wenyewe wape uhuru wakafanye yao ht km kuolewa upya
 
Back
Top Bottom