Nilikuta Bunduki na Bastola ya Osama haina risasi hata moja

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
"Nlikuta bunduki na bastola yake haina risasi hata moja na alikua hajajiandaa kwa mapambano yoyote licha ya kusikia kishindo cha helikopta nje"

Kauli hiyo anasema Mwanajeshi wa Seal 6 team Mark Owen sio jina lake halisi baada ya kuvamia na kuingia chumba alichokua anaishi Osama Bin Laden. Mark Owen ndio alikua mwanajeshi wa kwanza kumshoot Osama baada ya Kuingia chumba alichokua anaishi.

Ila cha kushangaza baada ya kukagua chumba alichokua anaishi Osama na familia yake na kukutana na Bunduki aina ya AK47 na Bastola moja vyote havikua na risasi hata moja which means that Osama hakujianda na makabiliano yoyote wala hawakukuta zile tisheti zenye Mabomu ya kujitoa Muanga.

Mark Owen mzoefu wa opereshi hatari za makundi ya kigaidi anazidi kusimulia katika operation zake nyingi alizofanya hawa viongozi wa makundi ya kigaidi wengi wanakua hawana hata Bunduki au wanakua nazo kama geresha tu ila ukweli unaweza kuta zina risasi tano au hazina.

Akihojiwa na kipindi cha 60 minutes na pia katika kitabu chake cha No easy day licha ya Osama kusikia kishindo cha helikopta ya Black hawk iliyodondoka na makabiliano na wafuasi zake floor za chini akina Kuwait ali walimkuta hajajiandaa kabisa.

Tunapata Somo kubwa hapa hawa viongozi wa makundi ya kigaidi wanawatoa chambo wenzao hasa vijana huku wao wakiwa hawapo tiyari kufa, same same na makundi ya waasi wao utakuta wanakula bata Ulaya huku RAIA mkizidi kuchinjana kama kuku.
 
Kabla ya kuandika chochote kuhusu osama ni vizuri ukaingia google ili umsome vizuri na umfahamu kwa uhakika.......
 
Wapumbavu kama wewe ndo huwa wanaamini kuwa Osama alikuwa gaidi. Wajinga nao watakuambia Wamarekani ni watu wazuri na wema.
#I'llComeBackShortly
 
Kuna wamarekani wengi wanaamini Osama yuko Bahamas anakula bata na akina Nyalandu
 
Wapumbavu kama wewe ndo huwa wanaamini kuwa Osama alikuwa gaidi. Wajinga nao watakuambia Wamarekani ni watu wazuri na wema.
#I'llComeBackShortly
Aise wapumbavu tena Rafiki yangu mbona neno Kali hilo, vipi yale majengo pale USA WTC nani alichora michongo mbaya zaid hata sisi tuna Historia ya kushambuliwa na magaidi.
Na mbona alikua akijirekodi kila watu akisisitiza watu wajitoe muhanga
 
Back
Top Bottom