Niliibiwa simu yangu Kigali Rwanda ndani ya Lisaa nikaipata

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,837
Hili tukio nilitaka nisiliweke mapema hivi kwakuwa bado nipo ndani ya himaya ya Paul kagame maana wataona nawachafulia nchi yao endapo wataona hili bandiko mtandaoni. Asubuhi ya Leo nilienda sehemu moja ipo hapa Kigali niyauswahilini kiasi wanaishi watu wenye hali ya chini. Nilikaa sehemu moja hivi kula matunda lakini baada ya hapo mda kidogo kucheki simu yangu sikuiona nilichanganyikiwa kwa kweli, ila kwakuwa kila hatua tano polisi wapo nikamwita askari mmoja nikamwambia nimepoteza simu yangu either kwakudondosha au kuibiwa Sina uhakika ilitoweka ktk mazingira yapi

Haloo baada ya kumwambia tu akaita askari zaidi ya kumi na macall yao yale, walipojaa wakasema nionyeshe valid documents zakuwepo rwanda, nikatoa passport yangu wakasema nitaje namba ya simu nilivyotaja tu Kuna askari mmoja ivi shombeshombe mrefu kiasi akasearch ndani ya dk 10 ivi akawaambia wenzake kuwa simu ipo mji jirani ikabidi tupande kwenye gari zao tulipofika tu ilikuwa ni zero point ya mtu aliye na simu yangu. Aliwekwa pingu nikakagua simu nikapewa

Tuliporudi Kigali mm nikawaambia nataka niende kwenye makaburi ya Rwanda genocide hivyo naomba ni waache, wakasema haina shida hivyo wao wakabaki na yule mtuhumiwa. Can you imagine simu ya Android kwa hapa bongo ingechukua mda gani kupatikana? Mimi niliipata ndani ya Lisaa tu tena bila kutozwa pesa yoyote Ile. Hii ni Rwanda
images%20-%202022-09-02T185901.739.jpg
 
Nchi yeyote inyopitia matatizo ya wao kwa wao ndani ya nchi huwa baadae inakuja kuwa nchi ya kistaarabu na inayopiga hatua kubwa za maendeleo.
Hakuna asiyefahamu Rwanda hali waliyopitia mwaka 94,hatimaye leo hatuwafikii kwa ustaarabu na tukizubaa itatuacha kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja.Acha Rwanda,njoo Kenya hapo,angalia waliyopitia kwenye uchaguzi wa mwaka 2007,hiyo hali imeifanya Kenya kupiga hatua sana na watu wanaheshimiana na serikali inaheshimu watu!.
Uenda na sisi tutafika huko siku moja.
 
Can you imagine simu ya Android kwa hapa bongo ingechukua mda gani kupatikana? Mimi niliipata ndani ya LiCan you imagine simu ya Android kwa hapa bongosaa tu tena bila kutozwa pesa yoyote Ile. Hii ni Rwanda View attachment 2343391

Mpwayungu nakuambiaga siku zote Acha uongo
Na juzi Tu hapa nilikuambia wewe upo zako Kwa mtogole unakula mihogo na pilipili ya mbilimbi..

Mtu ambaye yupo sehemu tofauti na alipokuwa awali hawezi kufanya kosa dogo la kiuandishi km hili,upo Rwanda unasema Kwa hapa bongo ...wewe haupo Rwanda,upo hapa bongo

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Hili tukio nilitaka nisiliweke mapema hivi kwakuwa bado nipo ndani ya himaya ya Paul kagame maana wataona nawachafulia nchi yao endapo wataona hili bandiko mtandaoni. Asubuhi ya Leo nilienda sehemu moja ipo hapa Kigali niyauswahilini kiasi wanaishi watu wenye hali ya chini. Nilikaa sehemu moja hivi kula matunda lakini baada ya hapo mda kidogo kucheki simu yangu sikuiona nilichanganyikiwa kwa kweli, ila kwakuwa kila hatua tano polisi wapo nikamwita askari mmoja nikamwambia nimepoteza simu yangu either kwakudondosha au kuibiwa Sina uhakika ilitoweka ktk mazingira yapi

Haloo baada ya kumwambia tu akaita askari zaidi ya kumi na macall yao yale, walipojaa wakasema nionyeshe valid documents zakuwepo rwanda, nikatoa passport yangu wakasema nitaje namba ya simu nilivyotaja tu Kuna askari mmoja ivi shombeshombe mrefu kiasi akasearch ndani ya dk 10 ivi akawaambia wenzake kuwa simu ipo mji jirani ikabidi tupande kwenye gari zao tulipofika tu ilikuwa ni zero point ya mtu aliye na simu yangu. Aliwekwa pingu nikakagua simu nikapewa

Tuliporudi Kigali mm nikawaambia nataka niende kwenye makaburi ya Rwanda genocide hivyo naomba ni waache, wakasema haina shida hivyo wao wakabaki na yule mtuhumiwa. Can you imagine simu ya Android kwa hapa bongo ingechukua mda gani kupatikana? Mimi niliipata ndani ya Lisaa tu tena bila kutozwa pesa yoyote Ile. Hii ni Rwanda View attachment 2343391
Tuwekee picha ya Mhuri uliogongwa kwenye Passport yako wakati unavuka Boarder kuingia Kigali
 
Mpwayungu nakuambiaga siku zote Acha uongo
Na juzi Tu hapa nilikuambia wewe upo zako Kwa mtogole unakula mihogo na pilipili ya mbilimbi..

Mtu ambaye yupo sehemu tofauti na alipokuwa swali hawezi kufanya kosa dogo la kiuandishi km hili,upo Rwanda unasema Kwa hapa bongo ...wewe haupo Rwanda,upo hapa bongo

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Umemdaka pabaya 😂😂😂
 
Back
Top Bottom