Nilichogundua, waimbaji wengi wa injili wa sasa hawana Yesu, ni biashara zaidi

Unacho sema ni sahihi lakini nani anapaswa kuwaonya hao 🌝 maana mvuta bangi hawezi kumwambia mwenzake aache bangi😁 hata akimwambia hawezi kumfokea vikali

Asanteni ☺️
Kama hujui tu, mvuta bangi ndio ana uhalali mkubwa zaidi wa kumuumbua muongo na mnafiki kuliko asiyevuta bangi.
Haihitaji kuwa mwema au mbaya ili kumuonya anayekosea ili kuwalinda wengine. Tusiogope kuwanyoshea kidole wale wote wanaoharibu taswira ya imani zetu kisa sisi pia sio wasafi. Uovu upingwe na watu wote.
 
Kwahiyo ndio mnatusimanga..? Tutaacha kuimba muanze kuhangaika kwa kukosa vibe za nyimbo za kidini nyie tusengenyeni Tu!
...Zamani tulipokuwa na Munishi TU kwani nyimbo za INJILI hazikuwepo ? msitutishie kuacha Kuimba, acheni Ufuska !!
 
Do as I Say.., not as I Do..., Mantra kama hio ndio ninayoitumia hapa Jukwaani na kwenye Maisha yangu naangalia Nguvu ya Hoja na sio Mtoa Hoja...

Kutangaza Injili ni lazima ufanye kwa matendo ? - Kama wanatangaza kwa ujumbe na Ujumbe kwenye ule wimbo unakwenda mainstream huoni kwamba wanakidhi the objective kuliko hata yule anayekesha na kusali lakini hana medium ya kufikisha ujumbe ?(hata kama wanafanya wapate pesa - the end justifies the means)
Injili sio usanii bali ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa watu wote. Utahubirije kile usichokiamini au usichokitaka kukiishi.
Kama maisha yako hayana muunganiko wa moja kwa moja na injili unayoihubiri au kuimba, maana yake hiyo ni dhihaka kubwa kwa Mungu na malengo yako yatakuwa kuitumia injili vibaya (kibiashara!) na mwisho utaishia kupotosha watu.

Kwa kifupi sana Mhubiri (muimbaji) wa injili anapaswa kuwa na maisha masafi ili kulinda ushuhuda
 
Mimi nimeamua kufunguka hapa JF ili kuwafungua na wengine. Kuhusu viongozi wa dini, hilo pia ninalifahamu, ipo siku yao nitawapiga nyundo nzito pia.

Yapo mengi makubwa kuliko hata hilo la ndoa ☺️ tena hayo mazito yanafanywa na wachungaji, maaskofu, mapadri, masheikh, manabii, na mitume ni makubwa kuliko hilo ndoa lakini hakuna anaye wakemea hao ila ni vile tu wanajitahidi kuyaficha sana,, ni makanisa mengi sana yana behind the scenes ila waumini hawajui na mimi nayajua kwa sababu ni mdadisi sana,, hatuyasemi sababu yatazua mambo mengine mazito na kuwavunja moyo watu

Hata hizo ndoa mnazo sema wasanii wamevunja pia kuna siri ambazo sisi hatuzijui kwahiyo mnataka hadi mtu afie kwenye ndoa kisa ni msanii hatakiwi kukimbia mateso 🥺 Tisiwe wepesi wa kulaumu ila tuwe wadadisi wa mambo, tukiwa wadadisi wa mambo tutaweza kusaidia watu wengi sana ila kwa kuwalaumu watu bila kujua vyema chanzo cha tatizo tutapoteza watu wengi sana,, mtu akifanyiwa jambo baya ambalo halisemeki hadharani akifanya maamuzi hadharani anaonekana ni mkosaji ndg zangu kwa hali hii tunakosea sana
Wasanii wenu kuna mengi sana wanayapitia...
Kama mtu amekaa kwenye ndoa kwa miaka zaidi ya 15 then anakuja kuondoka hapa lazima kuwe na sababu ikiwemo kuchoka kuvumilia mateso

Kuachana kwa namna hii sababu kubwa ni kuchoshwa na jambo fulani alilovumilia kwa kipindi chote lkn hakuna hata uhafadhari na miaka inazidi kusonga kumbuka kila mtu yupo hapa duniani ili afurahie maisha sio kuteswa na mtu

Kwanini mtu ateseke kwa sababu akichukua hatua ataonekana yeye ndio mkosaji.. huu ni ukatili unaofanywa na wanajamii kushirikiana na mtesaji mwenyewe🥺 hili ndio jambo la kukemea sio kumkea mtu aliye amua kujipunguzia mateso
 
Kama hujui tu, mvuta bangi ndio ana uhalali mkubwa zaidi wa kumuumbua muongo na mnafiki kuliko asiyevuta bangi.
Haihitaji kuwa mwema au mbaya ili kumuonya anayekosea ili kuwalinda wengine. Tusiogope kuwanyoshea kidole wale wote wanaoharibu taswira ya imani zetu kisa sisi pia sio wasafi. Uovu upingwe na watu wote.

Ukiwa mvuta bangi ni vema kumshauri mtu ambaye havuti bangi sababu mvuta bangi anafahamu athari zake vyema,, lakini mvuta bangi hawezi kumshauri kitu mvuta bangi mwenzie,, hapa hataweza kumwambia mwenzake acha bangi atasema "tuache" bangi,, kama hadi hapa hujanielewa basi bhn 😂😂
 
Injili sio usanii bali ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa watu wote. Utahubirije kile usichokiamini au usichokitaka kukiishi.
Kama maisha yako hayana muunganiko wa moja kwa moja na injili unayoihubiri au kuimba, maana yake hiyo ni dhihaka kubwa kwa Mungu na malengo yako yatakuwa kuitumia injili vibaya (kibiashara!) na mwisho utaishia kupotosha watu.

Kwa kifupi sana Mhubiri (muimbaji) wa injili anapaswa kuwa na maisha masafi ili kulinda ushuhuda
Hizo ni Imani na Maisha ya mtu huwezi kumpangia jinsi ya kuishi..., ninavyosikiliza mfano Nibebe ya yule sijui nani sisikilizi sababu anaishi maisha kama aliyoishi mama Theresa hata kama akiwa Teja ila kazi aliyofanya ni nzuri na inaburudisha..., tukiseme watakatifu ndio waimbe playlist ya wengi itatoka kwenye nyimbo za kutosha na kushuka mpaka sifuri....

Usifuate matendo ya mtu bali sikiliza neno kama lina mantiki na kama halina achana nalo....., After all hata kwenye vitabu kina Daudi, Suleiman n.k. maisha yao huenda yalikuwa ya hovyo kuliko hata hawa wa sasa
 
Hata nyimbo zao ni za kumsifu huyo mungu wao anayewatanganisha watu.

Mungu wa upendo anaunganisha watu.
 
Hizo ni Imani na Maisha ya mtu huwezi kumpangia jinsi ya kuishi..., ninavyosikiliza mfano Nibebe ya yule sijui nani sisikilizi sababu anaishi maisha kama aliyoishi mama Theresa hata kama akiwa Teja ila kazi aliyofanya ni nzuri na inaburudisha..., tukiseme watakatifu ndio waimbe playlist ya wengi itatoka kwenye nyimbo za kutosha na kushuka mpaka sifuri....

Usifuate matendo ya mtu bali sikiliza neno kama lina mantiki na kama halina achana nalo....., After all hata kwenye vitabu kina Daudi, Suleiman n.k. maisha yao huenda yalikuwa ya hovyo kuliko hata hawa wa sasa

Safi sana mkuu 🤗 hawa wanataka kuleta itikadi za umbea kwenye dini 😂 wanataka wote tuwe kama mange kimambi
 
Tusipende Sana kuhukumu

Kuna watu wanadai wameokoka hawa ndo wahuni Sana .

Mimi napenda MTU akiyezaliwa katika usafi na akaishi katika usafi na sio yule anayedai alikuwa katika uchafu na ameuacha na kuhamia katika usafi.
 
Sasa kule studio wanarecord bure? Haikuandikwa kuwa mtumishi wa Mungu atakula madhabahuni?
Mpigie simu Boni Mwaitege, Rose Muhando, Christina shusho nk dau watakalokutajia ndipo utajua kuwa wanatoza ili kufidia gharama za kurekodi au wana agenda nyingine
 
Ndio
Hata Diamond, Harmonise au Zuchu (tena akiwa na mtindo wa maisha ulio kinyume na Yesu) anaweza kuimba nyimbo za Injili na watu wakabarikiwa. Hivyo kuimba gospel na watu wakapata vibe ya gospel sio issue. Issue inakuja pale tunataka kuhusianisha injili unayoihubiri (kuimba) na maisha unayoishi, kama haviko sambamba tunapaswa kukuonya wazi wazi, maana huo ni usanii wa kidunia kwa mgongo wa injili. Hatuutaki, maana unaua thamani ya Injili kwa watu wanaomtafuta Yesu maishani mwao. Ni dhihaka.
maana nikasisitiza hakuna alie mkamilifu ( sisi ni binadamu) hivyo tuwaombee maana shetani yupo kazini na anawalenga zaidi watendakazi ambao wanawakumbusha watu kuhusu uwepo wa Mungu
 
Back
Top Bottom