Nikiwaona Vijana wanaograduate, Nawahurumia sana

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
7,583
10,819
Wakuu leo katika pita pita zangu nimepita njia ambazo zina vyuo,
Mabibo(NIT) na Uhasibu (TIA).

Na leo kwenye vyuo hivi kuna Mahafali.

Watu ni wengi sana kwenye hayo maeneo.

Nimejikuta nawaonea sana huruma vijana hawa waliovyaa majoho yao na wamejipamba vizuri sana sura zao hasa wadada.

Nimereflect tu hali ya kitaa ilivyo. Nikawahurumia tena.

Hivi kuna ulazima sana?

Natamani wafanye kimya kimya.

Anyway Mungu awasaidie.

Tuwaombee Vijana.
 
Taasisi za fedha zipo nyingi sana zinawahitaji ila wawe na uvumilivu katika kipindi chote cha kupata ajira. Kuhitimu taaluma hiiyo si lazima waajiriwe wote, wengine watalazimika kufanya shughuli ambazo hawakuzisomea, wajiandae kisaikolojia kuwa na altenative way kufanikiwa maishani mwao
 
Maisha lazima yaendelee na kila mtu ana mipango yake,

Ajali za Ndege zinatokea ila watu hawaachi kusafiri,Ndoa zina matatizo ila watu hawajaacha kuoa au kuolewa Ajali za Magari kila siku ila kila siku watu wananunua Magari,

Maisha lazima yaendelee,kila mtu angekua na mawazo kama yako basi hakuna kitu kingekua kinafanyika hapa Duniani coz kila kitu kina faida na hasara zake.
 
Back
Top Bottom