G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Naam, imefikia pahala watanzania tunajitumbukiza kwenye vijistori vya hovyo hovyo na kuvinadi pasipo kufanya utafiti wa kina. Hili mimi naliona kama tatizo kubwa sana kwetu kama watanzania.
Hivi karibuni ameibuka kijana mmoja ambaye alidai kuwa alifungua mlango wa ndege iliyopata ajali huko Kagera ya PW na kufanya abiria 23 watoke nje. Anadai kuwa mlango huo aliufungua kwa kuugonga na kasia la mti kutokea nje ndipo ukafunguka na mbali zaidi akadai kuwa alienda hadi upande wa Rubani na kufanya naye mawasiliano.
Sasa mimi nasema hivi, huu ni utapeli na ujinga wa hali ya juu kuuamini. Kwanza kijana yule hakuufungua mlango kwa njia anayodai! Kwangu mimi hilo hapana! Mlango ulifunguliwa kutokea ndani kwa mujibu wa fizikia ya ndege! Hilo kwenye mjadala nalifunga.
La pili ni kuwa upo uwezekanano mkubwa wa wale abiria pamoja na rubani waliokwama eneo la mbele ambapo ndege ilijikunja kutokana na kujibamiza kwa nguvu kwenye ardhi waliaga dunia muda mfupi sana baada ya dhoruba hiyo. Kishindo kilichoifanya ndege ikunjike hakikuwa kishindo cha kawaida hata kidogo. Yani kwa muonekano ule ndege ilipata dhoruba kali eneo lile na kwa sisi tunaopanda ndege kila uchwao tunajua muitikio wake ulikuwaje.
Kingine ni yule kijana aliyedai kuwa alipata kishoka cha kuvunja kioo ila akazuiwa kufanya hivyo. Emb acheni masihara nyie ya kuamini kila hadithi. Mnajua unene wa kile kioo??? Kama ndege iliweza kujibamiza vile hadi body ikakunjika kuelelekea chini na kioo kikabakia vile vile, je angeweza kukivunja kwa kishoka??
Munaoamini hii story na kutembea nayo kichwani "Wapumbavu wakubwa" Na siku nikikutana na yule kijana kweli atakula viboko kwa kuwadanganya watanzania wajinga!