Nijitibu vipi addiction ya soda?

Canabian Rasta

JF-Expert Member
Aug 18, 2022
773
1,708
Wakuu, wakubwa kwa wadogo naomba kujua madhara nitakayopata kwa unywaji wa soda, nimekua kama teja, kuna wakati nanunua majiyakuywa na soda pembeni yan kwanza nakuywa soda nikiridhika ndo nakuywa maji kidogo.

Nilianza kwa kuywa soda chupa moja wakati wa mchana tuu saivi naweza kuywa mara3 kwa siku, nimefikia hatua nanunua cret la soda kwajili ya usiku kabla ya kulala niwe napiga moja then naenda on bed, nina khofu nikitu gani kitafata baadae ila kwa sasa sina tatizo lolote.

Ugojwa wangu ni Mirinda nyeusi, Sprite, Stone tangawizi au pineapple pia energy drinks hua nagonga maramoja moja kama nikiywa soda then nikawa sijaridhika.
 
Asee hii ni hatari, unakaribisha ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine mengi.

=
Soda ni kinywaji kilicho na kalori nyingi, sukari nyingi, na kafeini.

Matumizi ya mara kwa mara ya soda yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya yako, ikiwa ni pamoja na:
  • Uzito kupita kiasi na unene wa kupindukia: Soda ina kalori nyingi, na ulaji wa kalori nyingi unaweza kusababisha uzito kupita kiasi na unene wa kupindukia. Uzito kupita kiasi na unene wa kupindukia unaweza kuongeza hatari yako ya kupata magonjwa mengi, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kiharusi, kisukari cha aina ya 2, na saratani.

  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu: Soda inaweza kuongeza hatari yako ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kama vile ugonjwa wa moyo na kiharusi. Hii ni kwa sababu soda ina sukari nyingi, ambayo inaweza kuongeza viwango vya cholesterol na triglycerides katika damu yako. Viwango vya juu vya cholesterol na triglycerides vinaweza kuongeza hatari yako ya kupata plaques kwenye kuta za mishipa yako ya damu. Plaques zinaweza kusababisha kupungua kwa mtiririko wa damu na kuziba kwa mishipa, ambayo inaweza kusababisha mashambulizi ya moyo na viharusi.

  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata kisukari cha aina ya 2: Soda inaweza kuongeza hatari yako ya kupata kisukari cha aina ya 2. Hii ni kwa sababu soda ina sukari nyingi, ambayo inaweza kuongeza viwango vya insulini katika damu yako. Viwango vya juu vya insulini vinaweza kuongeza hatari yako ya kupata kisukari cha aina ya 2.

  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata saratani: Soda inaweza kuongeza hatari yako ya kupata saratani fulani, kama vile saratani ya kibofu cha mkojo, saratani ya matiti, na saratani ya mapafu.

  • Kupungua kwa ulaji wa virutubisho: Soda haina virutubisho muhimu, na ulaji wa mara kwa mara wa soda unaweza kusababisha kupungua kwa ulaji wa virutubisho. Hii inaweza kusababisha shida za kiafya, kama vile upungufu wa damu na matatizo ya ukuaji.
Unapotumia soda, ni muhimu kuzingatia kiasi. Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza kwamba watu wazima wasitumie zaidi ya gramu 600 za sukari kwa siku. Hizi ni takriban vijiko 16 vya sukari. Soda moja ya kawaida ina takriban gramu 39 za sukari. Hii ina maana kwamba mtu anayetumia soda tatu kwa siku anaweza kuzidi kiwango cha sukari kilichopendekezwa na WHO.

Ikiwa unatumia soda mara kwa mara, ni muhimu kupunguza kiasi unachotumia. Unaweza kufanya hivi kwa kubadilisha tabia zako za kunywa. Kwa mfano, badala ya kunywa soda wakati wa mchana, unaweza kujaribu kunywa maji au chai. Unaweza pia kujaribu kupunguza kiwango cha sukari unachotumia katika soda kwa kuchagua soda zisizo na sukari au soda zilizo na sukari kidogo.

Ikiwa una wasiwasi kuhusu afya yako, unapaswa kuzungumza na daktari wako. Daktari wako anaweza kukusaidia kukuza mpango wa afya unaofaa kwako.

Endelea kusoma hapa | Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu
 
Ugojwa wangu ni Mirinda nyeusi, Sprite, Stone tangawizi au pineapple pia energy drinks hua nagonga maramoja moja kama nikiywa soda then nikawa sijaridhika.
Nijitibu vipi addiction ya soda.
  • Anza polepole. Usijaribu kuacha soda mara moja. Badala yake, jaribu kupunguza kiasi unachotumia hatua kwa hatua. Kwa mfano, unaweza kuanza kwa kunywa soda moja kwa siku, kisha kupunguza kwa soda moja kila siku nyingine, na kadhalika.

  • Pata mbadala. Badala ya kunywa soda, jaribu kunywa maji, chai, au kahawa.
 
Hii kahawa si ina caffeine?
 
Unaacha soda unakunywa chai na kahawa.! Are you serious.?
 
Hii kahawa si ina caffeine?
Swali: Hii kahawa si ina caffeine?

Jibu: Sahihi, kahawa ina kafeini.

"Hata hivyo, kafeini inaweza kuwa na athari chanya kwa afya, ikiwa inatumiwa kwa kiasi. Kahawa inaweza kusaidia kuboresha utendaji wa ubongo, kuongeza nguvu, na kusaidia kupunguza hatari ya baadhi ya magonjwa.

Pia ina virutubisho muhimu, kama vile vitamini B, vitamini C, na potasiamu. Kwa kuongeza, kahawa inaweza kuwa na ladha nzuri na ya kuburudisha, ambayo inaweza kufanya iwe rahisi kuchukua nafasi ya soda."
 
Wakuu, wakubwa kwa wadogo naomba kujua madhara nitakayopata kwa unywaji wa soda, nimekua kama teja, kuna wakati nanunua majiyakuywa na soda pembeni yan kwanza nakuywa soda nikiridhika ndo nakuywa maji kidogo...
Tembelea wodi ya watu wenye kusuka kama ipo.. kingine ukiwa na kisukari ukiumia kidonda kinapona kwa mbinde Au hauponi kabisa wengine wanaoza miguu kama ukifikiria hivi utaacha soda
 
Fanya hivi angalau kwa siku utembee kilometa Tano ili kuichoma hio sukari.

Pia juice ya ndimu au matumizi ya ndimu yanauwa madhara yote unayohofia.

Kazi ya ndimu ni kuflax sumu zote mwilini hata ukiwa addicted na vinywaji hivyo upati madhara.

Mbaya kama we ni mtu wa gari yaan nyumbani AC,AC kwenye gari, ofisin Ac ufiki 60
 
Unaacha soda unakunywa chai na kahawa.! Are you serious.?

Hoja: Unaacha soda unakunywa chai na kahawa.! Are you serious.?

Jibu : Hatumaanishi Chai (majani ya Chai) iliyowekwa Sukari, Mfano mimi binafsi natumia kahawa iliyowekwa Tangawizi bila sukari.

=
Soda ni kalori nyingi na ina sukari nyingi, ambayo inaweza kusababisha uzito kupita kiasi na unene wa kupindukia. Pia inaweza kuongeza hatari ya magonjwa ya moyo, kiharusi, na aina fulani za saratani.

Ikiwa unatafuta njia mbadala ya soda, chai na kahawa ni chaguo nzuri. Unaweza kutengeneza chai au kahawa bila sukari kwa kutumia asali, stevia, au matunda.

Kwa mfano, unaweza kutengeneza chai nyeusi na asali, chai ya kijani na tangawizi, au kahawa na maziwa ya soya. Unaweza pia kuongeza viungo kama vile tangawizi, karafuu, au mdalasini kwenye chai au kahawa yako ili kuongeza ladha.
 
Asee hii ni hatari, unakaribisha ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine mengi.

=
Soda ni kinywaji kilicho na kalori nyingi, sukari nyingi, na kafeini...

Ahsante sana [mention]Mwl.RCT [/mention] kiukweli umenisadia sana kwa ufafanuzi, saivi soda zangu ndani itabidi nizibandike jina kisukari/kiharusi juu ya chupa ili nikiwa na hamu nikumbuke huu ujumbe wako hamu ikatike.

Pia itabidi nihamie kwenye izo soda zisizo na sukari then nifanye utaratibu wa kuacha kabisa, kama nikifanikisha nitakua balozi wa kuhamasisha watu kuacha kutumia soda.
 
Wakuu, wakubwa kwa wadogo naomba kujua madhara nitakayopata kwa unywaji wa soda, nimekua kama teja, kuna wakati nanunua majiyakuywa na soda pembeni yan kwanza nakuywa soda nikiridhika ndo nakuywa maji kidogo...
Ushauri wangu ni kwamba, usiache kunywa soda ila, wakati wowote ule kabla ya kunywa soda hakikisha umekunywa maji kama litre moja hivi ndipo unywe soda.

Ukipata matokeo sitaki unishukuru, nenda kamshukuru Mungu wako, then uje kuishukuru JF.
 
Wakuu, wakubwa kwa wadogo naomba kujua madhara nitakayopata kwa unywaji wa soda, nimekua kama teja, kuna wakati nanunua majiyakuywa na soda pembeni yan kwanza nakuywa soda nikiridhika ndo nakuywa maji kidogo...
Pole sana ila ni simpo tuu.. Mara nyingi soda huwa haikati kiu kabisa.. Ndio maana umesema huwa unaanza na soda halafu baadaye unakunywa maji, that means maji yanayokukata kiu.

Wengi tuliweza kwa kugeuza unaweza kununua soda kama unavyotaka, lakini hakikisha umenunua na maji tena makubwa.

Kisha hata kama unaitamani soda kiasi gani.. Anza na maji.. Kunywa maji ya kutosha, gugumia chupa yako halafu ukiiangalia soda utaona huna hamu nayo kwa wakati huo utaamua kuiweka pembeni kwanza.

Hata ukiinywa utakunywa kidogo sana na la muhimu ni kuwa maj yashatangulia ya kutosha.

Hata uwe na hamu ya soda kiasi gani ukianza tu kunywa maji ile kiu na hamu ya soda huwa inakata kabisa, lakini ukianza na soda unaweza ukanywa hata chupa mbili na bado kiu ipo na lazima utalazimika kunywa maji ndio utakuwa okay.. So just do vice versa utakuwa umetibu tatizo kirahisi sana.

Nyongeza ni vema uwe unanunua vile vichupa vidogo vya soda usisithubutu kununua chupa kubwa.. Kuna kaushamba fulani tunako waswahili eti mtu anadhani zile size ndogo ni kwaajili ya watoto no no no.. Au eti utaonekana huna hela hiiiii learn to mind your business.

Kile ni kipimo kizuri kwa mtu mzima mls 250 hadi 300 usizidishe hapo utakufa na utagundua hao uliokuwa unawaogopa au kuwaonea aibu ulikuwa tuu ni ujinga wako tuu maana hakuna aliyekuwa na time na wewe.. Ni kunishtukia tuu.

Mimi ukiona ninavyokula hotelin au mgahawani utanishangaa nipo very very selective.. Ni afadhali nishinde njaa kuliko kula kitu ambacho najua kitaniletea shida.. Huwa sili kabisa.

Mimi nakula mchemsho tuu usitiwa tiwa sijui nini au macuta mafuta, asubuhi, jimbi, mihogo, viazi mtori plain, vitafunwa vya mafuta nadra na nakula kwa hamu tu au kama hakuna alternative basi nitakula kidogo sana.

Juice za viwandani ndio mauaji ya halaiki yaani baada ya miaka michache hili taifa sijui litabaki na kina nani????

Unakuta eti mtu hanywi pombe jambo jema kabisa halafu anakunywa kopo zima la Azam juice peke yake kwenye masherehe na mwingine anapewa makopo 2 na anajisifu eti alichangia fedha kubwa halafu asinywe wee.. Yaani mchango wako mwenyewe unakuuaa?

Ana unafuu mlevi kuliko mnywa juice 🧃 ilijazwa masukari ya viwandani na masweetener hatari kabisa.

Vifo vya kujiua Tanzania ni vingi mno mno sijui huko kwa Mungu Tutajibu nini??
 
Tembelea wodi ya watu wenye kusuka kama ipo.. kingine ukiwa na kisukari ukiumia kidonda kinapona kwa mbinde Au hauponi kabisa wengine wanaoza miguu kama ukifikiria hivi utaacha soda

Ahsante mkuu, ninampango wa kwenda kuona wagojwa ila nitaplan nisitoke bila kuona wagojwa wa kisukari.
 
Pole sana ila ni simpo tuu.. Mara nyingi soda huwa haikati kiu kabisa.. Ndio maana umesema huwa unaanza na soda halafu baadaye unakunywa maji, that means maji yanayokukata kiu...

Inshot vitu vya viwandani sio salama, nivizuri tupeane tips za juice za asili ambazo sio nzito nzito maana mi kuanza kupenda soda ni sababu ni kiywaji soft yani kikiwa baridi nikuweka mdomoni na kupiga funda nnazoweza nikishusha nasikia ubongo upo safi.

Nawaza kujaribu juice ya miwa sijui na yenyewe inamadhara!? maana nimeona sehemu af nikaona inaendana na vinywaji navypenda iko simple sio nzito.
 
Back
Top Bottom