Nigombee ubunge jimbo gani 2015?

Magu

Senior Member
Jun 13, 2011
156
56
Ndg zangu wana jf nawaombeni ushauri wenu, nimezingatia yafuatayo kabla ya yote, Jf injumuisha intellectuals na ndo mana tuna slogan yetu kuwa jf's ni great thinkers, pili pia palipo na wengi haliharibiki jambo, na mawazo ya wengi ni mawazo ya Mungu. Mimi ni mzaliwa wa Wilaya ya ukerewe, lakini bahati mbaya sikuwahi kukaa baada ya wazazi wangu kuwa katika utumishi wa umma, na wakati walipostaafu wakaamua kuishi wilaya ya Magu, wamejenga na kumiliki mashamba na kutambulika kama wakazi wa Magu. Mimi binafsi nimejenga Dar na naishi na kufanyakazi Dar. ↲Mimi ninakusudia kuingia ktk mchakato wa kugombea ubunge 2015, tatizo langu sijui ni wapi naweza gombea, magu, ukerewe? Nawaombeni ushauri wenu ndg zangu
 
Jiulize Je Ktk nyumba yenu unakubarika, kama haukubariki hiyo ela ni bora ufanyie biashara maana utafirisika eeh!
 
Kama umejenga Dar es Salaam na unaishi huko kwa nini uende kuwatapeli watu wa Magu au Ukerewe? Ndiyo ninyi mnaopata ubunge msionekane tena jimboni. Kama una hamu sana na ubunge gombea jimbo la Dar. Huko unakotaka kwenda unayo political base au unataka kutumia rushwa kununua ubunge?
 
Kwa hiyo huna ajenda unayotaka kuhangaika nayo! Ajenda yako ni kwenda Mjengoni tu!! Basi usigombee popote.
 
Kwa hiyo huna ajenda unayotaka kuhangaika nayo! Ajenda yako ni kwenda Mjengoni tu!! Basi usigombee popote.

There is always a political agenda kwa kila mtu anaye fikiria kuingia katika game hii, kwa sababu wote tunalenga katika kuwatumikia watanzania disregard of thier location, b'se if i contest from magu, Ukerewe or Dar, at the end of it, will be to represent Tanzanian's. Japo kila mahari pana political challenge zake. But I believe wherever i go, it will be to work for the Tanzanian's.
 
Kwanza unafahamu maana ya kuwa Mbunge?
Uwezi ukasema una mpango wa kugombea ubunge eneo ambalo ulifahamu,na hata ukisema unaifahamu Tz nzima bado utaonekana mwongo.
Kwanza unapaswa kufahamu kuwa ubunge ni dhana pana sana.
Mbunge ni lazima awe anafahamu matatizo ya wananchi anaowakilisha. Na mengine mengi hapo.
 
Back
Top Bottom