Nigerian solves 150 yrs Math Problem!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Profesa kutoka Nigeria Opeyemi Enoch anadaiwa ameweza kusolve Math problem ambalo wanahisabati wa Dunia wamelishindwa kwa miaka 150, linaitwa Riemann Hypothesis.

Kwa wale wanaofahamu Hisabati kidogo, Riemann Bernhard ni Mwanahisabati wa Kijerumani aliyetoa mchango mkubwa sana kwenye Hisabati. Kama unafahamu Integration ziligunduliwa na Bw. Riemann na kihisabati huwa zinaitwa Riemann Integrals, na ndiye aliyetunga ile alama iliyokaaa kama herusi ya S
8a120ff933ad9e18e3862da78b0baee3.png
!

Atapokea Euro milioni moja kwa kazi hii kubwa!
 
Ahaaa!!! Wapi ma prof wa UDSM, na wao walishindwaaaaa???


Siyo Wa UDSM peke yake ni wa Dunia nzima wameshindwa kuanzia Tokyo mpaka Stanford kuja Shanghai mpaka Munich au Paris na hili tatizo limekuwepo kwa miaka 150 yaani wanahisabati wa Dunia nzima wameshindwa kulitatua kwa miaka 150!
 
Hebu iweke hapa hiyo Math problem. Kuna magenius humu

Wameshachelewa lilikuwepo kwa miaka 150 iliyopijta lkn sasa hivi limeshatatuliwa, ila bado yapo mengine sita yamebakia yanaitwa ,,seven millenium problems" sasa yamebakia sita!

 
Siyo Wa UDSM peke yake ni wa Dunia nzima wameshindwa kuanzia Tokyo mpaka Stanford kuja Shanghai mpaka Munich au Paris na hili tatizo limekuwepo kwa miaka 150 yaani wanahisabati wa Dunia nzima wameshindwa kulitatua kwa miaka 150!

Kwani mulimpa profesa J akashindwa?
 
USAHIHI:

Hii habari sio ya kweli. Bado haijathibitishwa rasmi na wenye kuthibitisha. Stori hii imekuwepo kwenye mitandao mikubwa sana kama yahoo tangu mwanzoni mwa wiki hii. Media kubwa kubwa za UK zimeongelea sana hii kitu lakini hadi sasa hakujathibitika kama huyu profesa amesolve hii hesabu. Habari zilizopo kwa sasa ni kuwa hii stori haina uhakika wowote imekaa ''kichanga la macho zaidi''. Kukaa kichanga la macho pia ni kwa mujibu wa mitandao mikubwa kama yahoo.

wrong answer The Nigerian mathematics "genius" who fooled the British media


http://qz.com/552327/the-nigerian-mathematics-genius-who-fooled-the-british-media/?utm_source=YPL



 

Attachments

  • mathematics.jpg
    mathematics.jpg
    105.3 KB · Views: 697
NI UONGO Soma maelezo haya "Unfortunately, it looks like in this case it?s not a real proof of the Riemann Hypothesis, and this post on a Nigerian discussion forum says emphatically he has not solved it. As mentioned in that post, there?s a paper on academia.edu under his name, which is actually a copy of a paper by someone called Werner Raab (retired). Raab?s website ? index is empty, and has a single broken link to ?the truth of the Riemann hypothesis?. Some digging reveals that that URL has never worked. Confusingly, Enoch seems to be gathering papers about the Riemann Hypothesis on academia.edu under his own name."
Huyu jamaa amesema yeye mwenyewe kuwa amesolve je ni nani ameprove au hata kukubaliana naye? interview na BBC alifanya yeye na akapost Twitter mwenyewe kwenye account yake.
Gonga hapa uelewe vizuri Riemann Hypothesis not proved | The Aperiodical

HUWEZI KUJITANGAZA MSHINDI MWENYEWE na kusema eti umepigiwa simu umeshinda kiasi hicho cha pesa.
 
Wameshachelewa lilikuwepo kwa miaka 150 iliyopijta lkn sasa hivi limeshatatuliwa, ila bado yapo mengine sita yamebakia yanaitwa ,,seven millenium problems" sasa yamebakia sita!


Mkuu millenium prize problems yapo saba mawili yameshakuwa solved moja ni hili la Riemann hypothesis ambalo litakuwa limeshasoviwa na huyu mnigeria(kama solving yake imethibitishwa) na lingine ni Poincare conjecture lililosoviwa na mrusi Grigory Yukovlevich Perelman mnamo mwaka 2003 kwa mapenzi yake huyu jamaa alikataa zawadi yake ya kusovu hilo swali hivyo yamebaki matano(5) na si sita(6) yaliyobaki ni (1)P versus NP problem.(2)Hodge conjecture.(3)Yang Mills existance and mass gap.(4)Navier-Stokes exsitance and smoothness.(5)Birch and Swinnerton Dyer conjecture.Kazi kwenu watabe wa hesabu google uyapate uweze kuyasovu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom