Nifanyaje nipate leseni ya biashara?

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,880
Heshima kwenu wakuu,

Aisee hii hali mbaya ya kiuchumi imenifanya nifungue kaduka kangu mtaani, sasa TIN nimeshapata nilikuwa na leseni nikaenda TRA wakanibadilishia ikawa ya BUSINESS.

Sasa wakuu mwenye ufahamu je leseni ya biashara naipata wapi na je ni requirements gani natakiwa niwe nazo ili niipate leseni na inapatikana wapi wakuu mimi naishi Tabata Segerea.

HAPA KAZI TU
 
nenda kwenye halmashauri husika. Mfano kama unaishi mbagala DSM ungeenda pale Halmashauri ya Manispaa ya Temeke karibu na national stadium. Nenda kawaone ni jambo la siku moja tu ukiwa na documents wanazohitaji. maximum ndani ya siku tatu unapata leseni..
 
Heshima kwenu wakuu,

Aisee hii hali mbaya ya kiuchumi imenifanya nifungue kaduka kangu mtaani, sasa TIN nimeshapata nilikuwa na leseni nikaenda TRA wakanibadilishia ikawa ya BUSINESS.

Sasa wakuu mwenye ufahamu je leseni ya biashara naipata wapi na je ni requirements gani natakiwa niwe nazo ili niipate leseni na inapatikana wapi wakuu mimi naishi Tabata Segerea.

HAPA KAZI TU

Mkuu maelezo yako hayajakaa vizuri kiasi fulani.
Ukishakua na TIN you just go with it straight Halmashauri. Halmashauri wataangalia nature ya biashara yako then watakupatia leseni. Haichukui hata Massa mawili maana sikuhizi wanafanya kwenye system.

Hope TRA walikukadiria how much to pay annually. Lipa kodi kwa maendeleo ya taifa.!!!
 
ambacho sijaelewa ni kwamba TRA wamenipa TIN tu mkuu ila hakuna makadirio yoyote tuliyofanya
 
Nenda ofisi ya wilaya yako ukiwa na kopi ya tin, mkataba wa pango, kopi ya kitambulisho chako, tax clearance certificate (cheti kinachoonyesha hudaiiwi kodi, unapewa tra ulipobadili tin). Ukiwa navyo hivi unajaza fomu unapata leseni.
 
Back
Top Bottom