Nicki Minaj Kutumbuiza Saudi Arabia Azua Gumzo !

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
9,560
12,685
Tamasha la Nicki Minaj lazua gumzo Saudia
Nicki Minaj
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Nicki Minaj anajulikana kwa kuvalia mavazi ya kuonesha mwili na mtindo wa densi ambao baadhi ya watu wanasema ''unakiuka'' maadili ya kijamii

Tangazo la kuwa Nicki Minaj atakuwa mmoja ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la muziki nchini Saudi Arabia, limezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii nchini humo.

Mtindo wake wa mavazi na maudhui ya ngono katika nyimbo zake ni baadhi ya masuala watu wanahoji huku wakitafakari tamasha hilo litapokelewaje katika jamii ya kihafidhina ya Waarabu.

Rappa huyo anatarajiwa kutumbuiza watu katika tamasha la Jeddah World Fest Julai 18.

Tamasha hilo ni mfano wa hivi karibuni wa jinsi Saudi Arabia inavyoendelea kulegeza misimamo yake mikali hasa katika masuala ya burudani ili kuimarisha ukuaji wa sekta ya sanaa.

"Nicki Minaj" alitrend katika mtandao wa Twitter baada tamasha lake la Jeddah kutangazwa.

"Hebu tafakari kupata fahamu baada ya kupoteza fahamu kwa miaka mitatu na ukizinduka kitu cha kwanza unasikia ni kuwa Nicki Minaj atafungua tamasha la muziki Saudi Arabia, kusema kweli nitafikiria niko katika taifa lingine ," mmoja aliandika.

Mwingine alihoji ikiwa waandalizi wa tamasha hilo walifanya ukaguzi wa maonesho yake yaliopita japo angalau katika mtandao wa Google kabla ya kumpa kazi hiyo. "Hivi hakuna mtu Saudi Arabia aliyemtafuta Nicki Minaj kwenye google?" aliandika Kabir Taneja.
Haki miliki ya picha @KabirTaneja

Sio maoni yote yalikuwa ya kufanya mzaha. Mtu mmoja aliandika katika Twitter yake kuwa tamasha hilo la Minaj halitakuwa sawa hasa ikizingatiwa kuwa litafanyika karibu na mji Mecca- amabo ni mtakatifu kwa waumini wa Kiislam .

Katika video iliyowekwa kwenye Twitter mwanamke aliyevalia mavazi ya kidini alihoji kwa nini mamlaka ya nchini humo inamrusu rapa huyo kutumbuiza katika tamasha hilo huku ukiwazuia wanawake kuvaa mavazi yanayowabana hadharani.

"Atakuja kutingiza makalio yake na akiimba nyimbo zake zilizo na maudhui ya ngono huku akijitingisha zaidi," alisema "Halafu unaniambia mimi nivae abaya. Hilo linaingia akini kweli ?"

Wengine walisema hatua ya mwanamuziki huyo kufanya tamasha nchini humo ni unafiki, ikizingatiwa kuwa anatumbuiza piakatika matamasha ya wapenzi wa jinsia moja ili hali anajua msimamo wa Saudia kuhusu uhusiano wa aina hiyo. Hukumu ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Saudia Arabia ni kifo.

Minaj sio msanii wa kwanza kuzua hali ya utata kwa kukubali kufanya tamasha nchini Saudi Arabia.

Mariah Carey alipuuza wito wa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kumuomba afutilie mabali tamasha lake nchini Saudia huku rapa Nelly nae akilaumiwa vikali kwa kuandaa tamasha la wnaume pekee.

Hatua ya hivi karibuni ya kulegeza misimamo kuhusu masuala tofauti ya kijamii ikiwemo burudani ni sehemu ya mkakati wa mwanamfalme Mohammed bin Salman wa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Turki Al al-Sheikh, mkuu wa kitengo cha burudani alitangaza kuhusu mpango wa siku zijazo wa kufanyia mageuzi sekta ya muziki katika ujumbe wa Twitter mwezi Januari.

"Mungu akijaalia, hatua itakayofuatia katika masuala ya burudani siku zijazo ni maonesho kutoka kwa watumbuizaji tofauti, michezo ya watoto katika maeneo yalio na bustani pamoja na michezo mingine mingi itakyowasaidia vijana, wanawake na wanaume kusaidia kampuni za kitaifa za burudani," aliandika.
 
atatumbuiza kavaa hijjab duh tusubir tuone...wakijipindua TU kamwaga razi sijui watamkata kichwa....
Hata akivaa hijab haizuii kitu maana baada ya hapo atapata wafuasi wengi...akianza kufanya ufuska wake akiwa US dk 0 habari zipi Riyadh!!!
 
Hivi kwanini hayo mambo machafu huonekana ni kawaida huko yakifanyika sehemu nyengine ila kwa waarabu inakuwa ajabu?
 
Tamasha la Nicki Minaj lazua gumzo Saudia
Nicki Minaj
Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Nicki Minaj anajulikana kwa kuvalia mavazi ya kuonesha mwili na mtindo wa densi ambao baadhi ya watu wanasema ''unakiuka'' maadili ya kijamii

Tangazo la kuwa Nicki Minaj atakuwa mmoja ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la muziki nchini Saudi Arabia, limezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii nchini humo.

Mtindo wake wa mavazi na maudhui ya ngono katika nyimbo zake ni baadhi ya masuala watu wanahoji huku wakitafakari tamasha hilo litapokelewaje katika jamii ya kihafidhina ya Waarabu.

Rappa huyo anatarajiwa kutumbuiza watu katika tamasha la Jeddah World Fest Julai 18.

Tamasha hilo ni mfano wa hivi karibuni wa jinsi Saudi Arabia inavyoendelea kulegeza misimamo yake mikali hasa katika masuala ya burudani ili kuimarisha ukuaji wa sekta ya sanaa.

"Nicki Minaj" alitrend katika mtandao wa Twitter baada tamasha lake la Jeddah kutangazwa.

"Hebu tafakari kupata fahamu baada ya kupoteza fahamu kwa miaka mitatu na ukizinduka kitu cha kwanza unasikia ni kuwa Nicki Minaj atafungua tamasha la muziki Saudi Arabia, kusema kweli nitafikiria niko katika taifa lingine ," mmoja aliandika.

Mwingine alihoji ikiwa waandalizi wa tamasha hilo walifanya ukaguzi wa maonesho yake yaliopita japo angalau katika mtandao wa Google kabla ya kumpa kazi hiyo. "Hivi hakuna mtu Saudi Arabia aliyemtafuta Nicki Minaj kwenye google?" aliandika Kabir Taneja.
Haki miliki ya picha @KabirTaneja

Sio maoni yote yalikuwa ya kufanya mzaha. Mtu mmoja aliandika katika Twitter yake kuwa tamasha hilo la Minaj halitakuwa sawa hasa ikizingatiwa kuwa litafanyika karibu na mji Mecca- amabo ni mtakatifu kwa waumini wa Kiislam .

Katika video iliyowekwa kwenye Twitter mwanamke aliyevalia mavazi ya kidini alihoji kwa nini mamlaka ya nchini humo inamrusu rapa huyo kutumbuiza katika tamasha hilo huku ukiwazuia wanawake kuvaa mavazi yanayowabana hadharani.

"Atakuja kutingiza makalio yake na akiimba nyimbo zake zilizo na maudhui ya ngono huku akijitingisha zaidi," alisema "Halafu unaniambia mimi nivae abaya. Hilo linaingia akini kweli ?"

Wengine walisema hatua ya mwanamuziki huyo kufanya tamasha nchini humo ni unafiki, ikizingatiwa kuwa anatumbuiza piakatika matamasha ya wapenzi wa jinsia moja ili hali anajua msimamo wa Saudia kuhusu uhusiano wa aina hiyo. Hukumu ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Saudia Arabia ni kifo.

Minaj sio msanii wa kwanza kuzua hali ya utata kwa kukubali kufanya tamasha nchini Saudi Arabia.

Mariah Carey alipuuza wito wa wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kumuomba afutilie mabali tamasha lake nchini Saudia huku rapa Nelly nae akilaumiwa vikali kwa kuandaa tamasha la wnaume pekee.

Hatua ya hivi karibuni ya kulegeza misimamo kuhusu masuala tofauti ya kijamii ikiwemo burudani ni sehemu ya mkakati wa mwanamfalme Mohammed bin Salman wa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Turki Al al-Sheikh, mkuu wa kitengo cha burudani alitangaza kuhusu mpango wa siku zijazo wa kufanyia mageuzi sekta ya muziki katika ujumbe wa Twitter mwezi Januari.

"Mungu akijaalia, hatua itakayofuatia katika masuala ya burudani siku zijazo ni maonesho kutoka kwa watumbuizaji tofauti, michezo ya watoto katika maeneo yalio na bustani pamoja na michezo mingine mingi itakyowasaidia vijana, wanawake na wanaume kusaidia kampuni za kitaifa za burudani," aliandika.
Mshirika kapata mshirika mwenzake katika kumshirikisha ILAH....
 
Hiyo mijamaa pamoja na itikadi kali inapenda sana hayo mambo sema basi tu !
yanaongoza kwa kuwasumbua dada zetu facebook, nilishika simu ya girl wangu nikazama fb messenger uchafu niliokuta hawa waarab wanamtumia niliwa-undermine sana. Majinga makubwa
 
Yale yamewaachia dini kina kimsboy wao hawana time kabisa 😂😂😂
 
Saudia ya siku hizi ipo tofauti sana
Hongera mwanamfalme kwa kufanya amerika kuwa mshirika wako
 
yanaongoza kwa kuwasumbua dada zetu facebook, nilishika simu ya girl wangu nikazama fb messenger uchafu niliokuta hawa waarab wanamtumia niliwa-undermine sana. Majinga makubwa
Uchafu gani tena!?
 
Back
Top Bottom