Ni wakati gani wa kumuambia mchumba wako kuwa una mtoto!

bpouz

Member
May 26, 2008
38
9
hbar wadau bana naleta hii mada ni wakati gan muafaka wa kumuambia mpnz wako kuwa katika mahusiano yako ya nyuma yalipelekea kuwa na mtoto je ni wakat wa mwanzo wa mapenz au katikati au baada ya ndoa koz yamewah kumkuta rafik yangu alikuwa na mchumba wakafika ktk stage ya introduction kwa wazaz wakatoa nusu mali, ikawa inasubiliwa kumalizia from known where dem kapata habar mchumba wake ana mtt na ajamuambia mshikaj akazuga demu akavunja uchumba akadai heri angemuambia mwenyewe kuliko kusikia
 
hadi mnafikia uchumba hamjaambiana mna watoto? Unawezaje kuficha au kutoongelea wanao kwa marafiki zako?
labda sio rafiki.

Dunia haiishi vituko.
 
Kabla hata hujamuambia jina lako. Na kama mnajuana majina, wakati wa "tongozi" hiyo issue iwe ndio sentensi ya kuanzia.
 
Ukimwambia mwanzo kabisa atakutosa.
Anzeni mahusiano baada ya muda mwambie kabla hamjaanza uchumba rasmi ili ajue mtu anaejifunga nae alivyo
OTIS
 
Wakati muafaka ni pale mnapoanza kufahamiana na kuanzisha mahusiano ili ujue hiyo ''package'' ikoje. Habari za kufichana hazina maana kabisa!!

...Sawa kabisa BJ...mimi huwa nawashangaa sana wale wanaodai kwamba mnapoamua kuwa Wapenzi basi hakuna sababu ya kuulizana yaliyopita mnaenda mbele kwa mbele....Unaweza kudhani umepata kumbe umepatikana ukipita mtaani watu wanakuchora tu.
 
Day zero hujanena kwa lugha ukikutanae tuu, unaanza da "mwanangu nimeikia anaumwa kidogo" unamalizia anyway forget that!
Then mkazie macho kusoma signal kama vipi take note ya ushauri wake.
Wenye akili wanaanza hapohapo maswali
1. Yuko wapi " answer kijijini
2. Why that " kwanini usikae nae answer sina mlezi
3. Mama yake???? Answer "is long story

Postpone hayo mazungumzo ya mtoto then endeleza mengine:
Note: you can use any format or trend ila umeelewa what is expected.
 
Back
Top Bottom