Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 289
Pale Lumumba kulikuwa na kitengo cha propaganda, kwa watanzania wengi propaganda ni uongo. Moja ya kazi ya kitengo kile ilikuwa kuwaeleza watanzania uongo dhidi ya vyama vya upinzani kuhusu ukabila, udini na ukanda ambao kwa kipindi hicho uliwaingia barabara na ndio matokeo ya CUF chama cha waislamu na CDM cha wakristo.
Katika pitapita yangu kwenye thread moja hapa ndani ya JF niwekutana na majina ya watu ambao wanataka kurudisha CDM kwenye uongo ule ule bila wao kujitambua. Ni upuuzi mkubwa kugawa nchi kikanda, kidini na kikabila hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania tunashauku kubwa ya mabadiliko. Taifa hili halikupigania uhuru kwa kuwabagua watu wa kusini, kanda ya kati au pwani eti kwa sababu wapo wachache na waislamu. Kumbuka katika uchaguzi hatutazami tu idadi ya watu katika maeneo husika ila tunatazama idadi ya watu walijiandikisha kupiga kura na ushiriki wao kwenye kupiga kura.
Kuwa na mtazamo kwamba kanda ya ziwa na kaskazini pekee ndiyo wanaoweza kuiangusha CCM ni upuuzi. Tunachopaswa kutambua ni kwamba lazima uamsho huu ufanywe kwa Watanzania wote bila kujali dini,ukanda na ukabila. Nguvu ya umma (without discrimination za ukanda,udini na ukabila) ndio itakayotupa uhuru ya pili wa taifa letu (i.e. uhuru wa kifikra kuondokana na ukoloni mweusi ndani ya Taifa letu)
Mabadiliko hayawezi kuwa na tija kwa mantiki ya kugawanya nchi yetu ya Tanzania katika makundi.Tunajenga mitazamo ileile ambayo CDM wanaikimbia kutokana na propaganda za kipindi cha miaka ya nyuma. CDM hakijadominate kanda ya pwani si kwa sababu ya waislamu wengi bali nia kwa sababu hakijawekeza nguvu ya kutosha kutoa elimu ya uraia.Suala la msingi hapa ni kwa jinsi gani CDM wanatakiwa kujipanga.Kwa mitazamo ya kibaguzi tutajenga imani kwamba maeneo ambayo CHADEMA inaungwa mkono ni maeneo yenye wakristo wengi na hivyo kuwatenga waislamu, na hii ni hatari,lazima tuwekeze kwenye fikra tulivu kutatua changamoto katika maeneo ambayo bado siasa ya CDM haijakubalika na majority.
Lakini villevile tutambue kwamba hatuwezi kuwa na raisi toka CDM na kufanya kazi kwa ufanisi bila kuwa na wabunge wa kutosha hivyo kuna majukumu makuu mawili: Kuhakikisha hatupotezi wabunge tulio nao sasa na kuongeza idadi ya wabunge.
Nawakilisha