Ni Taasisi gani zinakopesha vikundi vya Wakulima

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
604
340
Tofauti na TADB inayohitaji vikundi vya muda mrefu kuanzia miaka mitatu kuvikopesha. Ni taasisi gani nyingine za kifedha zinazokopesha vikundi vya wakulima Tanzania? Mwenye kujua atufahamishe.
 
EFTA....agricultural mashines and equipments loans. They are located at IT plaza adjacent to PPF Tower building.
 
kikundi chako kina wanachama wangapi?
zao gani kinalima?
kimesajiliwa wapi?
je kina kaguliwa hesabu zake.....?
 
Tofauti na TADB inayohitaji vikundi vya muda mrefu kuanzia miaka mitatu kuvikopesha. Ni taasisi gani nyingine za kifedha zinazokopesha vikundi vya wakulima Tanzania? Mwenye kujua atufahamishe.
Zipo taasisi za aina mbili, kuna taasisi zinazotoa mikopo moja kwa moja mfano( TADB ,CRDB, NMB, EFTA, FINCA na baadhi ya bank ambazo zinatoa kipaumbele kwenye kilimo, lakini pia kuna taasisi ambazo zinakupa dhamana ili uweze kupewa mkopo na bank taasisi hizo ni Kama PASS, Vision fund, Yetu microfinance na nyingine nyingi
 
Kikundi kina wanachama 15 kimesajiliwa brela na wilayani. Ni kipya hakijawa na rekodi ya kukaguliwa mahesabu.
 
Zipo taasisi za aina mbili, kuna taasisi zinazotoa mikopo moja kwa moja mfano( TADB ,CRDB, NMB, EFTA, FINCA na baadhi ya bank ambazo zinatoa kipaumbele kwenye kilimo, lakini pia kuna taasisi ambazo zinakupa dhamana ili uweze kupewa mkopo na bank taasisi hizo ni Kama PASS, Vision fund, Yetu microfinance na nyingine nyingi
TADB maombi yetu yamefeli kwa kuwa kikundi bado kipya. NMB wanatoa mikopo kwa baadhi ya mazao kama vile korosho miwa na kahawa ambayo kikundi chetu hakilimi kwa sasa. CRDB hawatoi mikopo ya kilimo kwa sasa. EFTA wanadili zaidi na mashine. FINCA afisa wao aliyeko huku anadai hawatoi mikopo ya kilimo. PASS na VFT hatujaongea nao.
 
Ongea na pass na ukifeli nicheki nitakusaidia
 
Back
Top Bottom