Ni sheria ipi inazuia chama tawala kuiba sera za vyama vingine?

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
CCM imewahi kuiba sera ya CUF ya kufuta kodi ya kichwa, pia imeiba sera za chadema kuhusu katiba, kilimo na udhibiti wa matumizi ya serikali.

Binafsi naamini sera huundwa baada ya kufanya utafiti. Kama CCM wamepewa utawala baada ya kunadi sera A, kisha wanatumia sera B Za chama Q Je, huo sio wizi wa hatimiliki na ukiukwaji wa mkataba kati ya wananchi na chama tawala? Wanasheria mliomo humu janvini mnasemaje kuhusu uwezekano wa kukishtaki chama cha aina hii? au angalau kukishinikiza kuingia makubaliano maalum na chama chenye sera husika kabla ya kuanza kuitumia?
TUTAFAKARI!!!
 
Binafsi nimechukizwa sana na hatua ya Rais kuanzisha mchakato wa Katiba kwani ni jambo ambalo halimo kwenye sera za chama chake kwa hiyo hawana taarifa zozote za kiutafiti za kufanya jambo hilo!! matokeo yake kutapatikana katibu ya kufikirika au kubuni isiyoakisi nadharia za kitafiti!!!

TAFADHALI WANASHERIA ANGALIENI NAMNA YA KUOKOA HILI MAANA NI HATARI SANA INGAWA KILA MTU ANASHABIKIA KUUNDWA KWA KATIBA MPYA!!
we are dealing with a right thing at right time but with wrong people!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom