Ni sawa kukemea uzee kwa njia hii???

madingi wa siku ni mafaki..
kina mama sijui tuwaiteje, labda mabomu


Nadhani hapo Bujibuji ulimaanisha "siku hizi' ni 'mafataki'.
 
Iliwahi tokea long back in 2007 , mitaa fulani ya Sinza nilikuwa nasubiri Mnyama huku nikipata ulabu taratibu , ghafla nikaona Binti mmoja Mrembo kweli akaingia akawa anakunywa wine nina hakika ni under 20 yule , akawa busy na simu basi nikajua du si rizki jamaa yake (kijana mwenzake anakuja) toba baada ya muda aliingia Mzee ,yaani mtu mzima kweli cha ajabu alipofika tu akaanza kujisifu , " Eti wife alikuwa ananibanabana nisitoke sasa nimetime nikatoroka na simu nimeacha nyumbani kitandani akipiga atasikia inaita ndani kwahiyo leo hatatusumbua mpaka nirudi mwenywe " kweli nilichoka that day na kabinti hakakuwa na aibu hata kidogo "FEDHA" acha kabisa!
 
Kuna watu wana majibu ya mkato kiasi kwamba hutakaa umuulize tena! The bottom line is Tanzania is a dying nation! Kuanzia kwenye uongozi wa nchi mpaka kwenye mmomonyoko wa maadili kwenye jamii tunazoishi! Yaani imefika mahali ambapo kuna vitu vinaonekana vya kawaida wakati viko kinyume na maadili.

Mashoga siku hizi eti wameanza kuonekana ni watu wa kawaida katika jamii, hawajifichi tena. Vibinti vya sekondari siku hizi wala havina ''boyfriends'' wanaosoma nao, wana wakaka na wababa wanaofanya kazi na wenye kipato. Wanafunzi wenzao wanawaita ''daddy I am goin''.....!!!

Niishie hapo kwa sasa!
Masaki hii hapa nimeshindwa vumilia yaani kwangu hii ni welcome 2010! duh eti daddy am goin'
 
Usiwalaumu sana wazee, vibinti vya siku hizi vina tabia za ajabu sana! Na hizi simu za mkononi ndio kabisaaa!

Kuna siku simu yangu iliishiwa chaji na umeme ulikuwa umekatika, nikaomba ''handset'' ya mtoto wa kike wa anko wangu aliyekuwa kaja kunitembelea pale kwangu. Akanipa, nikaweka laini yangu lakini meseji na namba nyingi za simu zilibaki kwenye ile ''handset''. Niliyoyaona humo nilitetemeka !! Mtoto ana umri mdogo lakini mambo yake ni makubwa kuliko hata mimi mwenyewe!!!
Tamaa ndio zinawaponza mabinti kutaka hiki na kile ambavyo sio vya muhimu ktk maisha lkn napo kama hawa mababa wasipo wafuata sio rahisi wao kujiingiza mi naona watu wazima ndio wenye matatizo au waaribifu
 
Back
Top Bottom