Ni nini mtazamo wako wewe mwanandoa katika scenario hii

Habari wana jamii.... Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.
Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni

Kwa kweli kuolewa na mtu ambaye amefiwa na mwenza wake ni mtihani mkubwa sana. Sijapitia comments nyingine huenda umeshaambiwa bali si vibaya na mimi nika share my own experience. Mama yangu alifariki na mshua akaoa tena, lakini mpaka mshua na yeye anafariki hakuna siku inapita hajamtaja 'mamsap' wake (my mother), for 20 good years not a single day! Akikerwa ndio kabisaaa mpaka utamuonea huruma. Hapo unaweza ona kwamba hawa wanapata shida mno kupata chaguo kama lile. Pia kumbuka kwamba kwao wao inatokea wametengana na wake zao si kwa mapenzi yao bali ya Mungu, hawajaachana kwa ugomvi wala kwa hiari. Mapenzi yao bado yapo, ni vile tu yamekatizwa. So wewe ni kama substitute ambae ukiweza ziba nafasi vizuri basi utaweza win his love. Tatizo litakalo pelekea mpaka aanze kutundika picha za marehemu mke wake mpendwa ni pale atakapoona unafanya vitu ambavyo mke wake alikua hafanyanyi and vice versa(sisiemi uwe kama yule mama marehemu, la) bali kwake mume itakua ni kero inayompelekea kum-miss la aziz wake ambae ndio alikua chaguo lake la awali. So wewe unatakiwa uwe faraja kwake (komaa).

Sijajua ulikaa nae muda gani kabla hujaingia ndoani, usikate tamaa endelea kumsoma, upate kumuelewa. Hapa sijataka kugusia watoto. Tutakesha. If interested njoo PM we can talk over a cup of tea.

Otherwise I wish you luck.

PS. Halafu shoga wanawake hatununagi, hata mwanaume avimbe vipi, tena huyo wa aina hiyo ndio wale “fragile” ” this side up” “handle with care”
 
Habari wana jamii, Ni takribani miaka miwili imepita tangu nimeolewa na tuna mtoto mmoja. Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.

Basi mimi sio mzuri sana na mtembeleaji wa social network sababu ya ubusy wa kazi, lakini leo nikaona ngoja nipite pite walau niperuzi account yangu ya facebook. Mh nikapita pia kwenye account ya hubby nikakuta ameupload picha ya marehemu mke wake waliyopiga wakiwa pamoja katika hug bila kuwa na maelezo yoyote katika hiyo picha. Nimepita kama vile sijaiona na sijamuuliza chochote.

In fact hatuko kwenye condition nzuri make kuna some misunderstanding baina yetu. Ni nini mtazamo wako wewe mwanajamvi? Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni
Uzuri ni kwamba..
1. Unajuwa kuwa aliowa...
2. Unajuwa kuwa alifiwa na mkewe
3. Unajuwa kuwa hata alie, aweke picha popote, achane picha, bado haviwezi kumrudisha duniani marehemu mkewe
4. We unahangaikaje na mtu alikufa?
5. Unadhani kukuowa wewe maana yake anamchukia marehemu mkewe?
6. Hivi unadhani hamkumbuki? Au ikitokea (GOD FORBID) wewe umetangulia, akusahau milele?

Kuna vitu wanawake nashindwaga kuwaelewa... HIVI UNGEKUTA KAWEKA PICHA YA MWANAMKE UNAYEJUWA YUPO HAI, SI UNGEJIUWA..???
 
Bora umekuta ya marehemu ungekuata ya ya mtu yuko hai si ungejichinja
 
Kamkumbuka wa zamani, yaaani marehemu amemisi anajuta kwa kuondokewa na mkewe huyo wa zamani.

Analiona pengo lake hata kama upo nae,anatamani angerudi au angekuwepo. Moyo wake bado uko kwa marehemu.
 
Ni sahihi kabisa yeye kumkumbuka mwenza wake wa awali kwasababu hakuna binadamu asiyekuwa na zuri lakumfanya asikumbukwe, and guess what sio lazima huyo dada (RIP) awe na mazuri kushinda yako but ninachokiona hapa ni mume wako kuwa over emotional, hadi kutaka kukuumiza na wewe kwa kumbukumbu za mkewe wa zamani.
Mi nafikiri ukae na mumeo muongee na msameheane kwa mlichokoseana, lakini pia umwambie mnapokosana sio lazima akuoneshe kuwa anammiss mkewe wa zamani, kwasababu huko ni kutokukujali wewe, muulize hivi yeye anapokukosea wewe anataka wewe ummiss nani? Namaanisha hivi tujifunze kuishi kulingana na "what circumstance have given us" ni kweli kuna muda tunaumia lakini haimaanishi kupona kwetu pale tunapoumia ni mpaka tuwaumize waliotuumiza.
 
kazi yako wewe ni kuweka hizo misunderstanding kuwa understanding
mambo sijui ya kumpost nani sijui nani hiyo ni juu yake ili mradi sheria ifatwe kila mtu na AC yake hakuna kuchaguliana cha kupost
we endelea kuangalia meli ya titanic inavyozama halafu utajua kufuatacho ITV ni Isidingo the need ova
 
Uzuri ni kwamba..
1. Unajuwa kuwa aliowa...
2. Unajuwa kuwa alifiwa na mkewe
3. Unajuwa kuwa hata alie, aweke picha popote, achane picha, bado haviwezi kumrudisha duniani marehemu mkewe
4. We unahangaikaje na mtu alikufa?
5. Unadhani kukuowa wewe maana yake anamchukia marehemu mkewe?
6. Hivi unadhani hamkumbuki? Au ikitokea (GOD FORBID) wewe umetangulia, akusahau milele?

Kuna vitu wanawake nashindwaga kuwaelewa... HIVI UNGEKUTA KAWEKA PICHA YA MWANAMKE UNAYEJUWA YUPO HAI, SI UNGEJIUWA..???

Sasa hapa umeongea nini?

Huyo mwanaume mpaka anaoa tena alilazimishwa?
 
Unamuonea wivu hata marehemu?Badala ya kumuombea Allah amuweke mahali pema peponi marehemu ww unamuonea wivu?
Wanawake watu wa ajabu sana aisee!
 
Habari wana jamii, Ni takribani miaka miwili imepita tangu nimeolewa na tuna mtoto mmoja. Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.

Basi mimi sio mzuri sana na mtembeleaji wa social network sababu ya ubusy wa kazi, lakini leo nikaona ngoja nipite pite walau niperuzi account yangu ya facebook. Mh nikapita pia kwenye account ya hubby nikakuta ameupload picha ya marehemu mke wake waliyopiga wakiwa pamoja katika hug bila kuwa na maelezo yoyote katika hiyo picha. Nimepita kama vile sijaiona na sijamuuliza chochote.

In fact hatuko kwenye condition nzuri make kuna some misunderstanding baina yetu. Ni nini mtazamo wako wewe mwanajamvi? Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni
Nadhani jamaa anamkumbuka huyu mke wake labda kulingana na vituko unavyo mfanyia
 
Wanawake wana wivu hata k wa mtu aliekufa. Umesema we si mtu wa media. Mbona unaomba udhauri jf?
Ukweli ni kwamba mtu akifa huwa tunaumia, na pengo la mtu halizibiki, kulia au kumkumbuka huyo mwanamke ni ubinadam na haimaanishi alikuwa Mzuri kuliko wewe. Next mambo ya ndoa tafuta mtu mzima Mwenye busara muongee. Sio kuleta kwenye mitandao
 
Hivi ni mimi pekee ninaye amini wivu kiasi ni sehemu ya upendo? Kwa wakristo tunajua hata biblia inasema "Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu.."

Pole sana dada, wanaume tuna matatizo yetu ya kihisia vivyohivyo nyie pia mathalani ni tofaut kidogo.

Kuolewa na Mwanaume aliyefiwa ni changamoto sana, wengi wao huwa hawako tayari kuoa na huwa wanashinikizwa kuoa mara nyingi sana kwasababu ya kulea watoto.

Ushauri wangu; Jaribu kuelekeza upendo wako maradufu kwa watoto wake, usiwe mtu wa kuonyesha upendeleo wowote. Wanaume tunapenda wanawake wanaofahamu nafasi zao na kutimiza wajibu. Naamini kuwapenda watoto wake ni njia mbadala wa kuuteka moyo wake.

Asante, Mungu akutangulie.
 
Back
Top Bottom