Ni Nani hasa Mwenyeji wa Zanzibar? Je, ni Muafrika, Muarabu, Mshirazi au wote?

Hahah yeye atakuwa mzanzibaria huyo
Kwa hiyo unasema kuwa wabara hawakuwepo zanzibar ila wazenji walikuwepo huko wakiendelea na maisha miaka hiyo ?

Mkuu kwa kuanzia tu kitu ambacho ni muhimu kufahamu, Zanzibar ilikuepo Kabla ya Tanganyika, Na wazanzibari wenye asili ya bara wameanza kuhamia Zanzibar wakati Zanzibar tayari imeshakuepo na watu wapo. Kipindi cha Biashara ya Utumwa ndio wengi walipoanza kuhamia kwa wingi. Simaanishi huko nyuma hakukua na watu weusi walikuepo ili wengi wao walianza ku imagrate kipindi hicho.

Hayo yote sio muhimu, La muhimu ni kuwa Tanganyika inaitawala Zanzibar kimabavu na wamekua wakitumia lugha kuwa eti wanawatetea waafrica wanaoishi Zanzibar kitu ambacho sio sahihi, mana hao wanaowaita ndugu zao waafrica wameshaikataa CCM kitambo sana na ndio maana kila chaguzi CCM wanapigwa karibu kwa asilimia 80% wanaishia kutumia nguvu kuchukua serekali.
 
Kuna msemo kuwa "Hadi pale simba atakapojua kuandika, historia lazima itamtukuza mwindaji "

Kuhusu Historia ya nani walikuwa watu wa kwanza kuingia; Si rahisi kupata makubaliano ya pamoja, itoshe kusema kuwa Zanzibar ni jamii mchanganyiko. Wote; Wabantu, Waajemi, Waarabu na wengineo wameishi na kuijenga Zanzibar kwa namna moja au nyingine. Wote ni Wazanzibari.
 
Labda kweli ikiwa utaanza kutizama kijuu juu utaona maneno hayo ni ya upendeleo kwa upande fulani. Lakini Zanzibar ni visiwa, wewe unajuwa wazi kwamba hata leo hii ukitaka kuja znz ni lazima upande boti au ndege. sasa miaka ya maelfu iliyopita unadhani mwafrika gani wa afrika mashariki alokuwa hakuhitajia usafiri wa baharini kufika znz. Jiulize Mtanganyika alikuwa ana shida gani znz? Znz haikuwa pori la wanyama ukasema wamekuja kuwinda, wala watanganyika hawakuwa na uhaba wa matunda yao na vyakula vayo nini kilikuwa kiwapeleke znz?
Eeenh Heee,
Unashikilia hili la kuunda vyombo vya majini.

Hujui kwamba watu walikuwa wakivua samaki na kutumia mitumbwi, na hata magogo yaliyoelea na kusafiri?
Hivyo visiwa kijiolojia vilikuwa sehemu ya nchi kavu iliyoungana na Tanganyika.
Itakuwaje visiwe na watu na wanyama waliokuwa bara baada ya kumeguka kwa miaka mingi toka bara?

Unachoonyesha hapa ni elimu ya kuungaunga na upeo mdogo wa uelewa wa mambo.
 
Mkuu Kalamu

Yapo mengi yaliondakiwa na watu tuliowaona siku wanafika znz na baba zao kwa ajili ya kuchuma karafuu. Ukitaka kusoma historia ya znz waloziandika hao, uwe unasoma kabla ya kupata chakula kwasababu uanweza kutapika. Wamedanganya sanaaa.
Haya sasa, unaona ulivyopiga gigrii 360?
Maandiko ya hao waliokuja "kuchuma karafuu, yanaweza kumtapisha mtu" lakini haya ya kwako unayoleta hapa, huo ndio ukweli mtupu!

Hata kama unamsimlia mjinga maandiko yako hayo, mjinga huyo naye kuna siku ataazima "akili za bandia" na kuona upuuzi wa maandiko unayoyategemea wewe.
 
Mkuu Kalamu

Najuwa hili ni shida kukubaliana lakini wewe umesoma sana. Hebu tafuta sababu moja tu ya msingi kwanini mtanganyika au muafrika mwengine yoyote alikuwa na shida ya kusafiri hadi visiwani zanzibar katika miaka ya 500s AD.

Tukizingatia kwamba Waafrika walikuwa wamejiweka kikabila, shida zao zilikuwa kuwinda, kulima na jioni kudance. Mtazamo wa Maisha yao hayakuwa wa malengo ya maendeleo yoyote, yaani walikuwa wakiishi kwa mila na desturi zao tu. Kitu gani unadhani kingewafanya kusafiri hadi znz?
Hili ni jibu la kipuuzi unalolirudia rudia hapa.

Kama Tanganyika walikuwepo watu, kwa nini visiwa vya Zanzibar wasiwepo watu?

Unajua hivyo visiwa vilipotoka?

Wewe unadhani vilisombwa toka arabuni au Iran na kuja kuwekwa hapo vikiwa havina kitu chochote, si wanyama wala binaadam?

Au unadhani viliibuka tu toka baharini na kuwa nchi kavu?

Vipi aisee, mbona hata hujiongezi angalau hata kidogo?

Wewe unadhani watu wa mwambao wa pwani ya Afrika mashariki walikuwa hawavuwi samaki kama sehemu ya maisha yao ya kila siku?

Wao walikuwa wakiona maji ya bahari na kuyakimbia kama ni moto utakaowaunguza?

Mbona wewe una dharau sana na uwezo wa watu wetu. Maandiko yako hapa yanaonyesha dharau wazi, tena ya kibaguzi na kuwabeza binaadam weusi, wewe ni mbaguzi?
 
Mkuu Kalamu

Kuhusu muungano, labda litakushangazi hili, mimi binafsi naupenda na ninauhitajia. Muungano unalinda usalama wa zanzibari wa aina fulani fulani, ni bora kwetu kuwepo milele. Mie halinikeri kwamba rasi wetu wanachaguliwa dodoma, wacha achaguliwe popote pale lakini muungano uwepo na udumu.

Ikiwa kutakuwa na issue yoyote kuhusu kuwepo kwa Tanznaia, lizingatie hili, shida hiyo itafanywa na Watanganyika, na katika uchaguzi uliopita tumeanza kuona cheche zikianza. soon watanganyika watalazimisha kuwepo kwa nchi na serikali yao ya tanganyika.

Mwarabu hakuchukuwa ardhi ya mtu kwa sababu hapakuwa na mwenyewe zanzibar. Hilo halitaki darubini.

Kuhusu utumwa, ndio ulokuwa mtindo wa siku zile kabla ya industrila revolution, kwahivyo waarabu wazaungu, hata waafrika wenyewe kwa wenyewe walifanyana watumwa.
Ninakuelewa vizuri kwenye hili.

Yaani baada ya "wenye nchi nyie" kunyang'anywa nchi yenu kupitia Mapinduzi, salama yenu na kinga kwenu ni 'Muungano'.

Muungano kama ulivyo sasa ni ngao kwenu kutoka kwa 'Wazanzibara', ambao wao walikuwa ni wachuma karafuu tu walionyang'anya nchi yenu.
Muungano unawafaidisha nyinyi, '"Wazanzibari" mnaolindiwa nchi yenu na waTanganyika, huku mkifanya shughuli zenu za kuwanyang'anya mali; kwa vile "waTanganyika hawajui kulinda mali zao."

Hapana.
Usitegemee sana hiyo habari ya Tanganyika kuiachia Zanzibar tena kwa kuwa na serikali ya Tanganyika.

Kitakachotokea sasa ni kwa Tanzania kuhakikisha kwamba Zanzibar ni sehemu isiyoweza kujitenga tena na Tanganyika, kama ilivyo kwa Hong Kong na China.

Kwa hiyo ondoa kabisa hayo matumainio yako ya kuiona Tanganyika ikiiachia Zanzibar. Na hata kama ingeamua kuiachia, Mwarabu (Mzanzibari), hana chake tena; Wazanzibara hawataruhusu tena upuuzi.
 
Na wazanzibari wenye asili ya bara wameanza kuhamia Zanzibar wakati Zanzibar tayari imeshakuepo na watu wapo
Hao watu ambao walikuwepo hapo zanzibar kabla wabara kuja hapo walikuwa waafrika au waarabu ?

Kama ni wa africa weusi kama sisi why waarabu waje kuchukua watumwa huku bara wakati huko huko zanzibar wapo watu mfano wa watumwa wanaowataka ?
Kipindi cha Biashara ya Utumwa ndio wengi walipoanza kuhamia kwa wingi.
Kabla ya biashara ya utumwa hao wazanzibari walikuwa waafrica au watu weupe ?
 
Hao watu ambao walikuwepo hapo zanzibar kabla wabara kuja hapo walikuwa waafrika au waarabu ?

Kama ni wa africa weusi kama sisi why waarabu waje kuchukua watumwa huku bara wakati huko huko zanzibar wapo watu mfano wa watumwa wanaowataka ?

Kabla ya biashara ya utumwa hao wazanzibari walikuwa waafrica au watu weupe ?
The Arabs are fighting back. W aluanza Hizbu wakaja CUF sasa wako ACT propose tu wanapiweza kujishikiza. Tayari kasema wametoka Iran, ebo, sasa mbona hawakubaki Iran? Columbus na Marco Polo na Vasco da Gama wakaenda Jamaica na Australia, je na huko ni Iran? Wengine wakaja wakagundua Ziwa Victoria na Mlina Kilimanjaro, je, nao ni Iran? I am missing Marehemu Asha Bakari angewapa vidonge vyao.
 
Recommended post






ITV Tanzania









#PHOTO: The President of the United Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan placing a bouquet of flowers in the grave of the first president of Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume immediately after the prayer that took place at the head offices of the Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar today on 07 April 2021 in the memorial day of (Karume Day).
Translated from Swahili


May be an image of flower and outdoors

May be an image of one or more people, people standing and outdoors

May be an image of 1 person, flower and outdoors

May be an image of outdoors and tree




7 April at 13:21 ·
Public

2,944 · Like · React · 82 Comments · Share · Like Page · Full Story · Save · More
 
Kabla ya kufikiwa na Hassan Bin Alli na watoto wake saba, Zanzibar ilikuwa tupu hakuna mtu hata mmoja. Kumbuka kwamba Zanzibar ni visiwa na nilazima uvuke bahari kuvifika. Waafrika wa Afrika Mashariki kazi zao ilikuwa kuwinda na kulima sio kuunda majahazi. Siamini pia kwamba waliweza kuogelea baharini wakafika Zanzibar.

Pia kusafiri kwa miaka ile ilitokana na utashi wa kutaka kukusanya mali zaidi, watanganyika leo hii hawaijali mali yao unadhani walikuwa na utashi wa kutafuta mali zaidi katika maelefu ya miaka iliyopita? Besides, Zanzibar haikuwa na mali yoyote isipokuwa majahazi yalikuwa yakuchukuwa maji tu hapo miaka hiyo. Mtanganyika alikuwa hana shida na maji ya Zanzibar kipindi hicho.

Muafrika wa kwanza kufika znz aliletwa kwa ajili ya kazi tu.
........MJINGA ANAWEZA KUWA HATA NA Phd, IKIWA ANATUMIA AKILI BANDIA

Watanganyika leo hawaijali mali yao ....WATANGANYIKA WA LEO WALIKUWEPO ENZI HIZO? Kwa hiyo hawa wavuvi wa pwani ya TANGANYIKA ya sasa hawakuwa wanajua kabisa kuvua zaidi ya kilimo tu na kuwinda? Jamii za enzi hizo kila jamii ilikuwa inaishi kulingana na mazingira yao ..kwa vyovyote lazima wali master mazingira yao ya pwani ...ikiwemo uvuvi pamoja na kuunda nyezo(mitumbwi/majahazi etc) ili kuwawezesha kufanikisha hilo .... hivi Watanganyika wa enzi hizo wa MAZIWANI huko na wale kwenye mito mikubwa nao walikuwa hawavui ?Lazima walikuwa wanavua na kwa kufanya HIVYO lazima walikuwa na vyombo vya kuwasaidia kufanya hivyo kama mitumbwi n.k ....
 
Hao watu ambao walikuwepo hapo zanzibar kabla wabara kuja hapo walikuwa waafrika au waarabu ?

Kama ni wa africa weusi kama sisi why waarabu waje kuchukua watumwa huku bara wakati huko huko zanzibar wapo watu mfano wa watumwa wanaowataka ?

Kabla ya biashara ya utumwa hao wazanzibari walikuwa waafrica au watu weupe ?

Kabla ya utumwa watu waliokuepo Zanzibar walikua ni Watu wenye asili ya Asia (Wahindi, Waarabu, Washirazi),

Ila wadanganyika baada ya kushibishwa propaganda za Lumumba wanalipinga hilo bila ya fact ya ina yoyote.
 
Kwa hyo zanzibar ilikuwa sio ya waafrica ?

Unapozungumza waafrica nashindwa kukuelewa hasa unakusudiaje, Ila kama unakusudia wa bara hilo nishakupa maelezo yake.

Kwa kifupi tu hao wanaojiita waafrica wengi wao walihamia Zanzibar in 1900's na wengi wao hawakua hata raia wa Zanzibar wakati wa vugu vugu la uhuru. Na ndio maana baada ya mapinduzi Mzee karume alitangaza kuwa kila aliekuemo Zanzibar baada ya mapinduzi rasmi ni raia wa Zanzibar. Mana wengi wao hawakua wazanzibari including yeye mwenyewe. Alikua raia rasmi wa Zanzibar 1960-61 baada ya kuukana uraia wa Malawi mahakamani.
 
Unapozungumza waafrica nashindwa kukuelewa hasa unakusudiaje, Ila kama unakusudia wa bara hilo nishakupa maelezo yake.

Kwa kifupi tu hao wanaojiita waafrica wengi wao walihamia Zanzibar in 1900's na wengi wao hawakua hata raia wa Zanzibar wakati wa vugu vugu la uhuru. Na ndio maana baada ya mapinduzi Mzee karume alitangaza kuwa kila aliekuemo Zanzibar baada ya mapinduzi rasmi ni raia wa Zanzibar. Mana wengi wao hawakua wazanzibari including yeye mwenyewe. Alikua raia rasmi wa Zanzibar 1960-61 baada ya kuukana uraia wa Malawi mahakamani.
Sawa mkuu.

Kumbe tunakubiana kwamba hawa wazenji wa sasa wasiwatemge na kuwasema watanganyika wakati wengi wao wametoka huku huku tanganyika
 
Sawa mkuu.

Kumbe tunakubiana kwamba hawa wazenji wa sasa wasiwatemge na kuwasema watanganyika wakati wengi wao wametoka huku huku tanganyika

Point si kuwa na wao wametokea Tanganyika, point ni kuwa wanapigania haki yao. Kuwalazimisha wakubali kuendelea kudhulumiwa na Tanganyika kwa sababu na wao wengi wana asili ya Tanganyika hilo sio sawa mkuu.
Ni sawa na kumlazimisha mtu aridhike kudhulumiwa na mtu mwengine kwa kua wanatoka ukoo mmoja au kabila moja, Hio waiwezi kuwa haki.
 
Kiwa
Ndugu Wana Jukwaa

Kuna maneno mengi yasioningia katika mizani ya akili yanayozungumzwa na watu hasa wenye asili ya Tanganyika kuhusu Zanzibar na Uzanzibari. Watu wamekuwa wakiunda historia ya zanzibar kutoka katika hisia na wivu wao binafsi. Historia ya kuunga unga vipande, historia isio na kichwa wala miguu.

Ikiwa unahaitaji kuijuwa Zanzibr na Wazanzibari, soma hadi mwisho

Mtu wa mwanzo kabisa kuweka mguu wake katika ardhi ya Visiwa vya Zanzibar ni wa Iran and waarabu. Ukitaka kujuwa hilo tizama katika picha na vifaa vya kale. Kwahivo Zanzibar imejengwa na kuimarishwa na waarabu na wairani. Ni haki kabisa kusema kwamba Zanzibar ni sehemu ya Urabuni. Hilo si ajabu kwasababu ndani ya Afrika zipo nchi za Kiarabu. Kwahivyo wachilia mbali kwamba Zanzibar iko pembeni kwa Afrika. Muafrika wa kwanza kufika Zanzibar katika wanaume aliletwa kwa ajili ya kuimarisha kilimo kwasababu waafrika walionekana ni wakulima mahiri sana na katika wanawake waliletwa kwa ajili ya kuolewa. Hakuna Mtanganyika au Muafrika yoyote Zanzibar alokuja kwa hiyari yake katika miaka ya mwanzoni ya karne za 13, 14, 15, 16 na 17 hata mwanzoni mwa karne ya 18

Kwanini Waarabu na Wa Irani ndio walikuja mwanzo Zanzibar?

Kwasababu watu wa Tanganyika walikuwa hawana sababu yoyote ya kuvuuka bahari na kuja Zanzibar. Watanganyika walikuwa na maisha yao yanayowatosha wenyewe, matunda, kilimo na wanyama. Na hakuna ushahidi wowote kwamba watanganyika walikuwa wakiunda majahazi au kama walikuwa ni mabaharia kama vile walivyokuwa Waarbu na Wa Irani.

Nani Kaitwala Zanzibar katika historia

Waarabu walifanya utawala wa kwanza na bora sana Zanzibar. Na nakuombeni musibabaishwe na majina ya watawala wa zamani wenye majina kama vile Mkama ndume an Mwinyi Mkuu, wote hao walikuwa waarabu. Katika utawala bora wa Zanzibar maendeleo yakawa makubwa watawala wakaona haja ya kuitanua dola ya zanzibar, ndio Tanganyika na nchi zote za afrika mashariki ikiwemo na DRC na Mozambique zikawa katika Zenj empire. Neema kubwa zilipatika kwa kufikiwa na utawala bora, watu wengi kwa mara ya kwanza wakafundishwa kuvaa nguo na usafi na mengineo.

Kwanini kuna Wazanzibari weusi?

Baada ya maisha kuanza, watu wa Zanzibar (waarabu na wairani) wakawa wanahitajia kuowa ndio hapo walipoanza kulekea mrima kutafuta wachumba. Bagamoyo, Kilwa kivinje na kwengineko. Hilo lililetea kupatika wazanzibari wenye rangi nyeusi. Marco Polo alipofika zanzibar alikuta wenyeji wa hapo ni weusi wenye nywele za singa.

Maisha bora yalikuwa zanzibar

zanzibar chini ya uongozi shupavu wa waarabu ilifika mbali kimaisha. Zanzibar ilikuwa na simu majumbani manano mwaka 1886, undersea cable zilitoka znz kupita Aden hadi London. Zanzibar ilikuwa nchi ya Mwanzo Afrika kutumia elevator, pale Beit el Jaibu. Zanzibar ilikuwa nchi ya tatu kutumi aumeme duniani.

Elimu ilikuwa kubwa sana zanzibar hata NASA waliweka tracking station Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi tajiri sana katika Africa, wafanyakazi wa zanzibari walikuwa wakisafiri kama watalii wakati wakipata likizo zao makazini. Gari la kwanza kutembea Kuwait lilinunuliwa Zanzibar, nchi za Uarabubi zilikuwa zinakuja znz kununua vyakula na nguo kama leo tunavyokwenda Dubai sasa.

Zanzibar ilikuwa nchi huru ndio maana waafrika waliokuja kufanyakazi na kutafuta maisha yao tu waliachiliwa kuingia katika siasa, kosa kubwa sana hilo. Wakafanya mapunduzi na kuuwa wazanzibari 17,000 usiku mmoja. Baada ya hapo Zanzibar inaakza kufa kidogo kidogo. Leo hii watuna tena chetu,
Kiwanda cha magari kilikuwa wapi?
 
Baada ya yote hayo ya ajabu niliyoyasoma leo kutoka kwa mleta mada hii, maajabu hayakuishia hapo.

Nilitaka kujua angalao kidogo mwandishi huyu yupo vipi?

Kabla sijaenda mbali nikakutana na haya maneno:

"MJINGA ANAWEZA KUWA HATA NA Phd (PhD) IKIWA ANATUMIA AKILI BANDIA"

Nikiri, imenichukua muda kidogo kuyatafakari kwa kina maana ya maneno hayo kumi; na kama yana maana, hata kama imefichika.

Baada ya tafakuri hiyo, nimetambua kwamba mwandishi hana lolote kichwani.

Hii si kumshambulia yeye binafsi kwa mawazo yake, bali ni katika kutafuta ukweli wa mambo anayoyawasilisha hapa.

Kuna haya mengine niliyoyaokota humo yanayomfunua mwandishi:

"Mwafrika wa kwanza kufika Zanzibar aliletwa kwa ajili ya kazi tu" - Yaani utumwa. Yaani hivyo visiwa hata wanyama pori hawakuwemo humo, na wao waliletwa baada ya waarabu kuishi humo?

"Pia kusafiri kwa miaka ile ilitokana na utashi wa kutaka kukusanya mali zaidi. Watanganyika leo hii hawajali mali yao unadhani walikuwa na utashi wa kutafuta mali zaidi katika maelfu ya miaka iliyopita?" -Kama huelewi maana ya maneno haya ni kwamba huu ndio uamini alio nao juu ya watanganyika mwandishi huyu.

"Zanzibar ilikuwa nchi huru (yaani raia wake wakiwa waarabu, na siyo waafrka weusi)
"Ndio maana waafrika walikuja kufanya kazi na kutafuta maisha yao tu (yaani hawa waafrika hawakuwa raia wa Zanzibar).
"Hawa wafanya kazi wasiokuwa raia wa Zanzibar (wafanyakazi wa kuja) wakaingia kwenye siasa na kufanya mapinduzi.

"Wakawaua wazanzibari (waarabu) 17,000 usiku mmoja"
Hivi hakuna mwafrika hata mmoja aliyeuawa katika mapinduzi yale? Maana hawa hawakuwa raia wa Zanzibar!

"Baada ya hapo Zanzibar inaanza kufa kidogokidogo.
"Leo hii hatuna tena chetu -
Yaani Waarabu wa Zanzibar, ambao walikuwa ndio raia halali wa Zanzibar (Wazanzibari)

Swali ninalojiuliza hapa, hivi hawa ndugu zetu waliopo Zanzibar ambao sio waarabu, wanayaelewa haya?

Binafsi nilikuwa silielewi hili. Leo nimefunguka macho kwa mara ya kwanza kabisa.
Huyu jamaa ni Hizbu. Hawa ndio wanaotaka Muungano uvunjike ili warudi kutawala Znz.
 
Point si kuwa na wao wametokea Tanganyika, point ni kuwa wanapigania haki yao. Kuwalazimisha wakubali kuendelea kudhulumiwa na Tanganyika kwa sababu na wao wengi wana asili ya Tanganyika hilo sio sawa mkuu.
Ni sawa na kumlazimisha mtu aridhike kudhulumiwa na mtu mwengine kwa kua wanatoka ukoo mmoja au kabila moja, Hio waiwezi kuwa haki.
Binafsi ninachokipinga mimi ni suala la wao kuona kuwa watanganyika wote wabaya na kuwaletea aina fulani za ubaguzi

Mimi sioni shida wao kudai haki yao kwa kuwa wao ni watanganyika wenye muda mrefu pale zanzibar,lakini likija suala la huyu mzenji huu mbara isiwe kigezo cha kubaguana na kuona kwamba ati kila mtangantika basi anatawala zenji wakati hayo yanafanywa na watawala pekee.

Mfano wa kauli hizo utaskia "mitanganyika inatutawala kimabavy" kana kwamba watanganyika wote kule ni viongozi wakati kuna watangantika ambao nao kimsingi hawana mamlaka yoyote na zanzibar.
 
Binafsi ninachokipinga mimi ni suala la wao kuona kuwa watanganyika wote wabaya na kuwaletea aina fulani za ubaguzi

Mimi sioni shida wao kudai haki yao kwa kuwa wao ni watanganyika wenye muda mrefu pale zanzibar,lakini likija suala la huyu mzenji huu mbara isiwe kigezo cha kubaguana na kuona kwamba ati kila mtangantika basi anatawala zenji wakati hayo yanafanywa na watawala pekee.

Mfano wa kauli hizo utaskia "mitanganyika inatutawala kimabavy" kana kwamba watanganyika wote kule ni viongozi wakati kuna watangantika ambao nao kimsingi hawana mamlaka yoyote na zanzibar.

Ni kweli mkuu hayo megine ni makosa, lakini yanachangiwa na situation ya mazingira ilivo.
Hebu tizama chuki dhidi ya wasukuma ilivyokua katika miaka mitano hii hapa bara, kwani hivi ni wasukuma wote waliokuemo kwenye system ya Serkali? Lakini chuki zinazotokana na uonevu huvuka mipaka, nakama Marehemu angeendelea kutawala Miaka 10 tu mengine hivi unahisi watu wangekua wanachuki kiasi gani na wasukuma? Hii inatokana na uonevu ambao mwisho wa siku binaadamu anakosa cha kufanya Zaidi kuzalisha chuki kwa anaefanyia
 
Back
Top Bottom