Ni Naibu Waziri yupi aliyemchafua Mengi?

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Jana usiku kwenye taarufa ya habari ya saa mbili kampuni ya NICOL ilimsafisha R. Mengi kuwa hahusiki wala hakushinikiza ununuzi ununuzi wa kiwanda cha dawa cha mdogo wake. Baada ya kusafishwa, Mengi alisema sasa anafikiria hatua ya kuchukua juu ya naibu waziri aliyemchafua ingawa alisita kutaja jina. Naomba kuuliza kama kuna mwana JF anayemfahamu huyu mh. Mengi alidai kuwa huyu waziri anavuta umatemate toka kwa tajiri mmoja kwa lengo moja tu la kumchafua.
 
kumbe ile kumsaliti Felix Mosha ilikua ili asafishwe!!anasema eti kiwanda kilinunuliwa bila ya yeye kushirikishwa!huo ni uongo wa mchana kiwanda chako,kampuni ya nicol yenu na wewe upo ktk management iamue kununua kiwanda chako bila ya wewe kujua huo ni utapeli wa mchana
 
Do not go around the bush, huyu atakuwa Adam Kighoma Alli Malima mbunge wa Mkuranga ; mvaa mapete ya fedha ya ulinzi wa giza na anayetembea na bunduki ya vita!!
 
ok nashukuru kwa kupata mwanga maana jana mheshiwa huyu aliposema maneno haya nilifikiri lakini sikujua ni nani,nawashukuru walio mtaja Napata picha halisi sasa
 
Jamani hivi huyu Jaji Bomani yeye apumziki maana kila siku na vyeo kibao, mara bodi ya madini mara NICOL mara Serengeti yaani hapumziki DAH wazee hawa bana,.,, ama hakika nchi ina wenyewe
 
Mtu akianza bifu na huyu mzee anaweza kujikuta anapishana na uwaziri au hata ubunge hivi hivi, mnamkumbuka Wilson Masilingi na swaga la iliyokua Kilimanjaro hotel, nenda kwa mheshimiwa yule aliyekua mbunge wa Nyamagana, nina maana ya bwana Masha na swaga la kumfirisi mzee huyu? Sina hakika na hatima ya Adam Kighoma Ali Malima itakuaje kisiasa! Yangu macho!
 
Jamani hivi huyu Jaji Bomani yeye apumziki maana kila siku na vyeo kibao, mara bodi ya madini mara NICOL mara Serengeti yaani hapumziki DAH wazee hawa bana,.,, ama hakika nchi ina wenyewe

kamwambie akupishe kama una ubavu!

Angekuwa babako ungesema? uzee ni hazina na ayajuayo na kuyaweza hufukii hata robo, masatu mabole
 
Jana usiku kwenye taarufa ya habari ya saa mbili kampuni ya NICOL ilimsafisha R. Mengi kuwa hahusiki wala hakushinikiza ununuzi ununuzi wa kiwanda cha dawa cha mdogo wake. Baada ya kusafishwa, Mengi alisema sasa anafikiria hatua ya kuchukua juu ya naibu waziri aliyemchafua ingawa alisita kutaja jina. Naomba kuuliza kama kuna mwana JF anayemfahamu huyu mh. Mengi alidai kuwa huyu waziri anavuta umatemate toka kwa tajiri mmoja kwa lengo moja tu la kumchafua.

https://www.jamiiforums.com/habari-...1677-spika-atoa-uamuzi-wa-mengi-malima-2.html
 
9.0 UAMUZI (RULING)
9.1 Kwa kuzingatia matokeo ya uchunguzi na ushauri wa Kamati ya Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, na pia kwa kuzingatia ushauri wa wajumbe wawili wa Kamati hiyo waliotoa mawazo tofauti na pia uchambuzi na ufafanuzi nilioutoa hapo juu, na vile vile na kwa kuzingatia mwenendo wa suala lenyewe na yote yaliyojitokeza wakati Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikifanya uchunguzi wake;

9.2 Na kwa kuzingatia uzito wa tuhuma za Mhe. Malima dhidi ya Bw. Mengi zimemuathiri Bw. Mengi zenye athari ya kumgonganisha na viongozi wakuu wa nchi;

9.3 Na kwa kuwa, kitendo cha Bw. Mengi cha kukosea utaratibu kwa kutumia lugha ya kuudhi kukanusha matamshi ya Mhe. Malima kupitia vyombo vya habari na kuwa pia imemuathiri Mhe. Malima;

9.4 Na kwa kuwa, itakuwa ni kwa manufaa ya wahusika, ambao ni watu maarufu kwamba, suala hili limalizwe na kufikia mwisho wake;

9.5 Na kwa kuwa, linapotokea suala lolote Bungeni au kwenye Kamati ya Bunge, suala hilo linapaswa liamuliwe kwa mujibu wa utaratibu za Kibunge (Parliamentary usage and practice);

9.6 Na kwa kuzingatia kuwa, malalamiko husika hayakuwa ni ‘kesi' kati ya Mhe. Malima na Bw. Mengi, bali ni malalamiko ya wote wawili, kila mmoja akimlalamikia mwenzake, yaliyowasilishwa kwangu kwa utatuzi;

9.7 Na kwa kuwa, busara zangu zinanituma kwamba, njia nzuri na iliyo bora ya kuyashughulikia na kuyamaliza malalamiko ya watu hawa wawili, ni kwa usuluhishi (reconciliation) kati yao; kwa hiyo basi, ili kuleta suluhu hiyo, naelekeza kwamba:

(i) Katibu wa Bunge awasiliane na wahusika ili tukutane ofisini kwangu Dar es Salaam, kwa siku nitakayopanga na iliyo muafaka kwao tuweze kuongea pamoja kwa madhumuni ya kukubaliana nami, utaratibu muafaka, utakaojenga suluhu endelevu baina yao na kuepuka hatari ya suala hili kushamirisha makundi yaliyochomoza ambayo yameonekana kuibua masuala ya udini, rangi na tofauti za vipato katika jamii.

Uamuzi huu nimeutoa Dodoma leo tarehe 08 Februari, 2007.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WALAANI WALA RUSHWA NA MAFISADI

Samuel Sitta MB
 
kamwambie akupishe kama una ubavu!

Angekuwa babako ungesema? uzee ni hazina na ayajuayo na kuyaweza hufukii hata robo, masatu mabole

Unajua succession plan? Je, unafikiri hawa vikongwe kuendelea kukalia ofisi ni sahihi? Kwa maneno yako haya, inaonyesha una akili finyu kama katibu wako wa uenezi na fungasi zitakuwa zinakusumbua kichwani kama mwenyekiti wako.
 
Pamoja na yote bado sikuridhika na utetezi wa Mengi itakuwaje hakushirikishwa kununua kiwanda cha madawa ambacho kwa upande wa pili ana mahusiano nacho na wakati huo huo yeye yuko kwenye vikao vya maamuzi vya Nicol.

Navyofahamu kwa biashara za Tanzania ni vigumu kupata mkopo au kupata uwekezaji bila kuwa na watu wa ndani wa kukupigia debe.Kama aliona taratibu zimekiukwa kwa kutumia nafasi yake angeomba kufanyike uchunguzi ili kujua ukweli badala ya kukimbilia kujiuzulu wakati pesa za watu zimeshapotea.Hizi tuhuma ni za muda mrefu muda wote alikuwa wapi kukanusha.

Mchezo kama huu alishaufanya George Bush wakati alipouza hisa zake kwenye kampuni ya nishati muda mfupi kabla ile kampuni haijafilisika kwa hiyo huo ni mchezo alioufanya Mengi unafanyika sehemu nyingi duniani
 
Hatua inayofuatia inatakiwa kuwa ni kuhakikisha wachapakazi waliochanga pesa zao NICOL wanarudishiwa haki yao.
 
.....kiwanda chako,kampuni ya nicol yenu na wewe upo ktk management iamue kununua kiwanda chako bila ya wewe kujua huo ni utapeli wa mchana
Ukweli ni kuwa Kiwanda kilikuwa ni cha mdogo wake Mzee Mengi. Hapo sasa na wewe tukuiteje?
 
kumbe ile kumsaliti Felix Mosha ilikua ili asafishwe!!anasema eti kiwanda kilinunuliwa bila ya yeye kushirikishwa!huo ni uongo wa mchana kiwanda chako,kampuni ya nicol yenu na wewe upo ktk management iamue kununua kiwanda chako bila ya wewe kujua huo ni utapeli wa mchana
Kiwanda sio cha Mengi!!

Sasa nani ni mwongo??
 
Back
Top Bottom