Ni muda wa Watanzania kuamka kutoka usingizini

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,379
6,931
Namshukuru mwenyezi mungu kadri siku zinavyoenda watanzania wanazidi kuamka kutoka usingizini kwa mambo yafuatayo;

kwanza wamechoshwa na mfumo wa elimu ambao hauna manufaa japokua wanasoma tu bora liende huku watoto wa minority wanasoma shule nzuri za gharama huku minority wakidanganya kubadili badili kwa uongo uongo elimu ya majority kumbe kitu kile kile na kuchezea hela nyingi kutengeneza vitu fake.

Watanzania baadhi wameacha upuuzi wa kushabikia minority na kufanya ya kwao na hawana muda na selfish people of minority.

Baadhi wameacha kukariri wachezaji wa mpira wa ndani na nje kwamba wanalipwa shilingi ngapi na wanamiliki nini huku wakifanya yanayowahusu badala kushabikia mambo ambayo hayana faida.

Baadhi wanafuatilia vyombo vya habari kufuatilia haki zao za msingi na kizazi kijacho kama ilivyo minority wanavyosaini mikataba kandamizi itakayo athiri walio wengi kizazi hadi kizazi.

Wameacha kushabikia wanasiasa wanafiki ambayo wanaingiza mambo fulani fulani ya upuuzi ili msahau mambo ya msingi. Hongereni pinga urasimu wa kusaini mikabara itakayoingamiza tanzania. Tanzania sio ya watu wachache bali ni ya wote kizazi hadi kizazi.

Wameacha kubeti kwa kutambua kwamba hakuna cha bure lazima ufanye kazi ili upate (nothing is free, nothing is easy just work hard) kutegemea sana bahati kwa kucheza kamari na kumuomba mungu bila kufanya kazi unajiandalia umaskini wa kutaka wewe mwenyewe.

Wameacha kushabikia ujinga (yaani mambo ya kipuuzi na kufuatilia mambo ya msingi) mfano, kufuatilia na kufurahia jirani au ndugu anaposhindwa au kupatwa na janga (hapa mziki).

Asanteni mwenye nyongeza unaruhusiwa floor ni yako.
 
Watanzania wa wap hao wameacha betting?
๐ฐ๐š๐ง๐š๐ค๐ฎ๐ฃ๐š ๐ฐ๐š๐ฅ๐ข๐จ๐ฉ๐จ๐ญ๐ž๐ณ๐š ๐ฆ๐š๐ฆ๐ข๐ฅ๐ข๐จ๐ง ๐ฒ๐š ๐ก๐ž๐ฅ๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐ค๐ฎ๐ญ๐ž๐ ๐ž๐ง๐ž๐š ๐›๐š๐ก๐š๐ญ๐ข
 
Back
Top Bottom